Uzuri leo hujatumia kiingereza chako kile😃.
My love,simkandamizi mwanamke wala simshushi mwanamke na kumuinua mwanaume ila ukweli ni kwamba tayari mwanaume yuko juu hata nisiposema tayari mwanaume yupo juu.
Yupo juu kwa sababu,wote tunajua wanaume ndio wanahudumia wanawake.Ni dunia nzima ila Afrika ni zaidi.
Mwanaume anaanza kuwa juu yako kwa kukulipia mahari(kama kakununua fulani hivi uwe property yake) then anatafuta makazi anakua kama anakufuga kwa kukulisha na kukupa huduma zote mpaka siku utakayozeeka ubakie na jino moja la mbele.Mpaka hapo nani yuko juu?
Na wanawake wote tunajua kuwa mwanaume ndo anatakiwa awe juu ndo mana mashoga zetu wanaohudumia wanaume tunawacheka na kuwakalia vikao vya umbea .Utasikia mwenzangu nasikia ile ingejimenti ringi kanunua bibie..Heheee,usinambie halooo.😃.Kwanini tuone ajabu?
Siku zote mwanaume ndo mtoaji ndo mana hakuna makahaba wa kiume wanaojiuza barabarani sababu wasingepata wateja ambao ni wanawake sababu wanawake hatujazoea kutoa hela zetu kwa wanaume.Ila makahaba wa kike hadi wanajenga na kusomesha kwa hela za wanaume.
Binafsi naona niko sahihi kuwa ukimsaliti mtu anayekupambania ataumia zaidi ya wewe ukisalitiwa na anayekuhudumia.
Hapa nimeongelea maumivu,
Sisapoti usaliti na ninqjua kuna magonjwa ila incase usaliti umetokea huu ndo mtazamo wangu.