Ikitokea TEC na Gwajima wakashirikiana, kishindo chake kitakuwaje kuelekea uchaguzi Mkuu?

Wakaungana kwenye nini sasa? Kugombea Urais au Ubunge? Wapewe na nani sasa? Mimi ni Mkatoliki niliyepokea Sakramenti zote tano bado Sakramenti ya Mpako Mtakatifu wa Wagongwa tu, lakini SIWEZI kuwapa kura wakigombea maana sio kazi yao!
Umeelewa kweli?
 
TEC sio wanasiasa hawawezi kuungana kwani wanagombea jimbo gani TEC!!!! Gwajimq ni mwanasiasa anapaswa asimame mwenyewe sio sahihi kuingiza dini.
 
TEC sio wanasiasa hawawezi kuungana kwani wanagombea jimbo gani TEC!!!! Gwajimq ni mwanasiasa anapaswa asimame mwenyewe sio sahihi kuingiza dini.
Kuungana kutokomeza Wasiojulikana na agenda zingine zingine πŸ˜ƒ
 
Kuungana kutokomeza Wasiojulikana na agenda zingine zingine πŸ˜ƒ
Nadhani hiyo ni kazi ya jeshi la polisi ,kanisa kazi yake kuhubiri injili watu waache maovu. Sasa kama police wameshindwa hapo ndio mtihani kwetu kama taifa. Lakini nadhani tulipofikia police watajitahidi kufanya kazi yao kwa weledi hebu tuwape nafasi maana kelele zimekua nyingi naona watachukua hatua.
 
TEC au gwajima sio vyama vya siasa japo wana watu. Sasa hicho kishindo wanakitolea wapi.
 
TEC au gwajima sio vyama vya siasa japo wana watu. Sasa hicho kishindo wanakitolea wapi.
Kuwatokomeza Wasiojulikana,

Nchi ikatulia, CDM ikarudi ulingoni,

Tukifanya uchaguzi murua bin haki,

Tunapata kiongozi mkuu mpya Mlawi.

Hicho ni kishindo kidogo?
 
bahati mbaya hilo halitakuja kutokea, ni kama sunni na shia, si unaona wasuni wanavyofurahi iran kupigwa, ndivyo ilivyo kwa wakatoliki na walokole. pamoja na kwamba wote wanaumizwa ila kila mtu anafurahia mwenzake anavyoumizwa, hawawezi kushirikiana. ajabu sana.
 
Lisingewezekana kwa wanadamu,

Kwa Mungu linawezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…