Ikiwa ajira za uarabuni zinalipa, watoto wa viongozi Waoneshe mfano Kwa vitendo

Ikiwa ajira za uarabuni zinalipa, watoto wa viongozi Waoneshe mfano Kwa vitendo

Tuliowapa mamlaka yakutuongoza inaonekana kuna mushkeli kwenye kufikiri..

Yaani wameshindwa kutumia resources tulizonazo na kuifanya jamii ya watanzania kuwa moja ya jamii bora duniani..

Leo hii eti tunashabikia watu wetu kwenda kufanya kazi za majumbani uarabuni kwa mishahara ya 500k to 1m.

Yaani tumeshindwa kukifanya kipato cha kila mtanzania kwa mwezi kiwe minimum usd 800 hii kwa wasio kuwa na kazi rasmi au wasio na kazi kabisa?
Na mikataba walosainishana mbona ni Siri?

What if wakienda kutolewa Figo huko!!
 
Unaenda mzima unarudi bila rinda hata moja.
Mateso wanayosimulia waliowahi kwenda kufanya KAZI uarabuni hayaelezeki,

Halafu Leo wanasaini mikataba KABISA kana kwamba wanauziana ng'ombe!!

Nani ameshirikishwa?

Na je KILIMO Si UTI wa mgongo wa uchumi wetu tena, Bali Utumwa Kwa WAARABU?
 
Nilishawahi kusema humu hizi safari nyingi za huyu Mama huko Uarabuni iko siku tutauzwa Utumwani.
 
Ni vyema, ungeanza wewe kutushawishi kulima kwa kuonyesha kwa vitendo umefanikiwa wapi kwa kilimo hicho na unafanya wapi harakati zako za kilimo! watanzania tutaendelea kuwa watazamaji wakati wenzetu wanapiga hatua na kuendeleza nchi zao! Kenya inapeleka wafanyakazi wengi sana katika nchi hizo unazosema wanaenda kufanywa utumwa na wanarudisha nyumbani fedha nyingi sana ambazo zinaingia kwenye uchumi moja kwa moja! Endelea kuongeza ujinga kwenye upumbavu
Ndo tunataka viongozi wetu wawatangulize watoto wao Ili tujue Kweli Utumwa unalipa uarabuni!!
 
Nchi ya Nigeria na Kenya baada ya uingereza kuweka sheria ya skills pull Nigeria na Kenya wamemwaga manurse na madaktari wa kutosha. Kazi wanazofanya zinawawezesha kununua nyumba uingereza ambazo thamani yake ni wastani wa Billion ya kitanzania japo ni mortgage wanayokupa kwa muda nrefu lakini ni investment inayowezesha generation zao kunufaika .tuko busy kuwapeleka uarabuni ujifika unakabidhi passport na huruhusiwi kupata uraia . Serikali iweke sawa elimu yetu na watu wetu wawe na uwezo kama wakenya na wanigeria hizo takataka za uarabuni subirini miaka kadhaa mtasema in exchange to your ports and forests
 
Haulazimishwi mkuu. Kama unaona mashamba yanipa piga jembe.

Wanao ona fursa uarabuni waende.

Kupanga ni kuchagua
 
Nchi ya Nigeria na Kenya baada ya uingereza kuweka sheria ya skills pull Nigeria na Kenya wamemwaga manurse na madaktari wa kutosha. Kazi wanazofanya zinawawezesha kununua nyumba uingereza ambazo thamani yake ni wastani wa Billion ya kitanzania japo ni mortgage wanayokupa kwa muda nrefu lakini ni investment inayowezesha generation zao kunufaika .tuko busy kuwapeleka uarabuni ujifika unakabidhi passport na huruhusiwi kupata uraia . Serikali iweke sawa elimu yetu na watu wetu wawe na uwezo kama wakenya na wanigeria hizo takataka za uarabuni subirini miaka kadhaa mtasema in exchange to your ports and forests
Ikiwa kidato Cha nne wanamakiza hata barua ya kuomba KAZI hawawezi kuandika,

Wataajirika vipi, kukwepa kuwajibika, ndo wanakuja na ajira hizi za kitumwa!!
 
Halafu, mbona fursa za middle east ndio wanazikubali kirahisi na kushawishi sana watu waende, mbona fursa za western countries wanawekaga ugumu na uzibe fulani hivi
Mkuu western si kwamba hakuna fursa . We are not competent enough ila kwa Kasi ya ugawaji wa rasilimali kama wangedhamiria kuweka deal na credible countries uingereza recently imegawa nafasi za kutosha Kwa wakenya na wanigeria .so many young boys and girls ndo wanaendesha health care kwa sasa. Benefit ni kubwa Sana ya kufanya kazi kama uingereza you will then be accepted Australia au US kiurahisi. Tatizo nadhani ni elimu tunayipewa na viongozi kutanguliza matumbo.jambo la kujiuliza Kenya wamefanyaje mpaka vijana wake kumwagwa kwa kiwango ninachokiona
 
Chukua Tangazo hilo wahi deadline usije ukaachwa.
20231220_183235.jpg
20231220_183238.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam, Shalom!!

Mwalimu Nyerere alipotuambia KILIMO ni UTI wa mgongo, alionyesha Kwa vitendo Kwa kuwachukua watoto wake kina madaraka , na ndugu na kwenda nao shambani.

Uongozi ni vitendo Si maneno, mvua zinanyesha sasa, viongozi wanatwambia watoto na ndugu zetu waache mashamba Eti waende uarabuni wakawe house boys na house girls Kwa Waarabu ,Eti Kuna dau nono!!

Nasema hivi, viongozi watangulize watoto wao huko Ili tuamini kama kunalipa.

Yaani waarabu wanakuja Afrika kutafuta fursa za KILIMO, misitu ,Dhahabu, sisi tuondoke Tanzania kwenda kuwatunza wazee uarabuni?

By the way, mnataka tuache ardhi ya URITHI na mashamba yetu Ili mfanye nayo nini?

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
Sawa kabisa hatutaki kuona yakina Joshua mollel watoto wa wanyonge kujakuteswa huko
 
Kafala System watu hawaijui unapigishwa deki mpaka alfajiri hamna sehemu ya kushitaki.

Foreigners hawana HAKI chini ya Kafala System.
 
Back
Top Bottom