Chief Ortambo Ikumenye
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 247
- 503
Mimi kama mwana CCM moja ya matamanio yangu ni kuona CCM ikiendelea kushika dola ya Tanzania.
Ila kati ya jambo ninalotamani litokee kwenye muhula wa pili wa Rais Magufuli endapo akifanikiwa kushinda, ni kuacha kabisa kuwachokonoa wapinzani.
Wapinzani waachwe na kuishi maisha yao na ku play part yao kama kusudi la kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.
Binafsi pamoja na kuegemea upande wa CCM ila sijafurahishwa kabisa na baadhi ya matukio ndani ya miaka mitano iliyopita ya kukandamiza upinzani.
Tukio la kupigwa risasi Lisu, hila za kununua viongozi wa upinzani, vitabaki kama doa lisilofutika kwa utawala wa kwanza wa Magufuli. Ni moja wapo ya mbinu chafu za kisiasa karne hii ya utandawazi.
Kwa hizi wiki chache za ujio wa Lissu na mapokeo yake, ni kama vile upinzani umekuwa na nguvu maradufu pamoja na hila zote hizo chafu.
Najua wanadamu hukosea, Magufuli rais wangu kweli hapo ni mahali alikosea, lakini ana uwezo wa kuparekebisha endapo akichaguliwa tena.
Awaache upinzani waishi maisha yao kama maana ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.