Uchaguzi 2020 Ikiwa Dkt. Magufuli atafanikiwa kushinda, aachane na agenda za kuminya Upinzani

Uchaguzi 2020 Ikiwa Dkt. Magufuli atafanikiwa kushinda, aachane na agenda za kuminya Upinzani

Maendeleo yakwao sio ya kwetu mana kwetu maendeleo hatujayaona

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Jomba usiseme maendeleo hatujayaona..sema wewe hujayaona..unaendelea kudanganyika..tu..endelea hivyohivyo jomba..kwanza tatizo kubwa nadhani ulitegemeaga biashara za madili..ambazo nyingi zimekufa..tafuta kazi ya kufanya jomba kuliko kuja na hoja zisizokuwa na mbele Wala nyuma..watakucheka watu. Umeandika jina lako Kama mkulima, hivi ni kweli hata kilimo kimekushinda...Basi wewe umeshindikana
 
Mimi kama mwana CCM moja ya matamanio yangu ni kuona CCM ikiendelea kushika dola ya Tanzania.

Ila kati ya jambo ninalotamani litokee kwenye muhula wa pili wa Rais Magufuli endapo akifanikiwa kushinda, ni kuacha kabisa kuwachokonoa wapinzani.

Wapinzani waachwe na kuishi maisha yao na ku play part yao kama kusudi la kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

Binafsi pamoja na kuegemea upande wa CCM ila sijafurahishwa kabisa na baadhi ya matukio ndani ya miaka mitano iliyopita ya kukandamiza upinzani.

Tukio la kupigwa risasi Lisu, hila za kununua viongozi wa upinzani, vitabaki kama doa lisilofutika kwa utawala wa kwanza wa Magufuli. Ni moja wapo ya mbinu chafu za kisiasa karne hii ya utandawazi.

Kwa hizi wiki chache za ujio wa Lissu na mapokeo yake, ni kama vile upinzani umekuwa na nguvu maradufu pamoja na hila zote hizo chafu.

Najua wanadamu hukosea, Magufuli rais wangu kweli hapo ni mahali alikosea, lakini ana uwezo wa kuparekebisha endapo akichaguliwa tena.

Awaache upinzani waishi maisha yao kama maana ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

Tatizo la JIWE anataka kufanya kila kitu yeye na kujifanya yeye yupo sahihi 100%,mtu kama huyo huwa hakubali kukosolewa kabisa na endapo ukimkosoa huenda yakakukuta makubwa......Umepewa nafasi ya kuongoza inatakiwa uongoze kwa mujibu wa sheria hakuna mtu anayeishi milele,tutende haki maana haki huinua taifa na amani ni tunda la haki(Balozi Mpemba).

Viongozi wa Dini kwenda kuomba Amani ni kujidanganya ,Tenda haki then Amani itakuja.
 
Mimi kama mwana CCM moja ya matamanio yangu ni kuona CCM ikiendelea kushika dola ya Tanzania.

Ila kati ya jambo ninalotamani litokee kwenye muhula wa pili wa Rais Magufuli endapo akifanikiwa kushinda, ni kuacha kabisa kuwachokonoa wapinzani.

Wapinzani waachwe na kuishi maisha yao na ku play part yao kama kusudi la kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

Binafsi pamoja na kuegemea upande wa CCM ila sijafurahishwa kabisa na baadhi ya matukio ndani ya miaka mitano iliyopita ya kukandamiza upinzani.

Tukio la kupigwa risasi Lisu, hila za kununua viongozi wa upinzani, vitabaki kama doa lisilofutika kwa utawala wa kwanza wa Magufuli. Ni moja wapo ya mbinu chafu za kisiasa karne hii ya utandawazi.

Kwa hizi wiki chache za ujio wa Lissu na mapokeo yake, ni kama vile upinzani umekuwa na nguvu maradufu pamoja na hila zote hizo chafu.

Najua wanadamu hukosea, Magufuli rais wangu kweli hapo ni mahali alikosea, lakini ana uwezo wa kuparekebisha endapo akichaguliwa tena.

Awaache upinzani waishi maisha yao kama maana ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

JPM hana sifa za kushinda. Labda atumie dola kama bashiru alivyosema.
 
Bas kusiwe na ballot papers za presidency
Namaanisha upinzani bado sana kishinda Urais wa Tanzania huo ndo ukweli mchungu japo hamtaki kuusikia ! Bado upinzani haujajipanga kimkakati kushinda Urais ndugu!
 
Namaanisha upinzani bado sana kishinda Urais wa Tanzania huo ndo ukweli mchungu japo hamtaki kuusikia ! Bado upinzani haujajipanga kimkakati kushinda Urais ndugu!
Je, CCM iko radhi kura zihesabiwe kwa uwazi kama ilivyofanya kwenye kura za maoni ya wagombea wake (japo u-rais huo ushindani ulipigwa stop)?
 
Je, CCM iko radhi kura zihesabiwe kwa uwazi kama ilivyofanya kwenye kura za maoni ya wagombea wake (japo u-rais huo ushindani ulipigwa stop)?
Nyie kura za maoni mlizihesabu wa uwazi? Hata zikihesabiwa kwa uwazi ukweli ni kwamba hamuwezi shinda !
 
Mimi kama mwana CCM moja ya matamanio yangu ni kuona CCM ikiendelea kushika dola ya Tanzania.

Ila kati ya jambo ninalotamani litokee kwenye muhula wa pili wa Rais Magufuli endapo akifanikiwa kushinda, ni kuacha kabisa kuwachokonoa wapinzani.

Wapinzani waachwe na kuishi maisha yao na ku play part yao kama kusudi la kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

Binafsi pamoja na kuegemea upande wa CCM ila sijafurahishwa kabisa na baadhi ya matukio ndani ya miaka mitano iliyopita ya kukandamiza upinzani.

Tukio la kupigwa risasi Lisu, hila za kununua viongozi wa upinzani, vitabaki kama doa lisilofutika kwa utawala wa kwanza wa Magufuli. Ni moja wapo ya mbinu chafu za kisiasa karne hii ya utandawazi.

Kwa hizi wiki chache za ujio wa Lissu na mapokeo yake, ni kama vile upinzani umekuwa na nguvu maradufu pamoja na hila zote hizo chafu.

Najua wanadamu hukosea, Magufuli rais wangu kweli hapo ni mahali alikosea, lakini ana uwezo wa kuparekebisha endapo akichaguliwa tena.

Awaache upinzani waishi maisha yao kama maana ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

Wapinzani ni nani ? wewe ambae unafikiri ni mpinzani mwekao pia anakuona mpinzani. Ni wingi na uchache ndio unaotoa upinzani.

Nini misingi ya upinzani?
Upinzani hauwezi kukua tuu kwa sababu watu wengi wamenda shule...........
Upinzani hauwezi kukua tuu kwa sababu watu wanahitaji mabadiliko ...........

Ni lazima nchi iwe na madaraji ya maisha ya wazi wazi, hapo ndio upinzani wa kweli utakuwepo.

Na Magufuli ndio Rais sahihi ambaye atachochea mabadiliko kama atabadilisha maisha ya watu.
Walikuwa hawana Umeme sasa wamepata lakini watauchoka,
Barabra nzuri nchi nzima watazichoka.
Hospital Nzuri nchi nzima watazichoka
Na huduma nyingi mbali mbali zikiwa zipo na watanzania watazichoka na hapo ndipo upinzani wa kweli utakuja.

KWA HIYO MABADILIKO YA CHAMA CHA UPINZANI KUINGIA MADARAKANI BAADO SANA , ILA VIONGOZI WA PANDE ZOTE MBILI WATABADILISHANA VITI TUU.
 
Moto ni uleule utapeli wa kwenda kwa wananchi baada ya uchaguzi kufanya mikutano ya hadhara na kuwachangisha fedha za maji, sijui mafuta ya chopa hauna nafasi tena Tanzania.
 
Mkuu ni kuwa na washauri wabovu.

Unafikiri angewaacha waendelee na harakati zao leo hii wangeongea nini!??

Sasa kinachotokea wanayo mengi ya kuongea waliyofungwa kwa miaka mitano.. Ukijumlisha na walivyokuwa missed.

Hatari tupu!!!

Saizi wanaongea nini cha maana ambacho wangalikiongea hapo kabla. Mikutano ya kisiasa baada ya uchaguzi kwa watakao kuwa wameshindwa ni kuruhusu utapeli wa kisiasa. Mbaya zaidi wengine wanatumia hiyo kama fursa ya kutumbua ruzuku za vyama na kuwachangisha wananchi fedha ya maji na mafuta ya chopa.
 
Tutaelewana.
 
Namaanisha upinzani bado sana kishinda Urais wa Tanzania huo ndo ukweli mchungu japo hamtaki kuusikia ! Bado upinzani haujajipanga kimkakati kushinda Urais ndugu!
Upo sahihi mkuu.
Pamoja na mapungufu yote ya aliye madarakani ambayo yameumiza na yanaendelea kuumiza watu wengi sana . Watanzania tungependa mabadiliko ya kweli yenye uelekeo wa kuchukua dola lakini km ulivyosema, upinzani wa Tanzania bado haujajipanga na mwaka huu pia hali ni Ile Ile ya miaka yote. Pamoja na kubanwa kwa vyama vya upinzani bado kuna mwanya wa kukiwezesha chama tawala kuendelea kushika Dola Kwa sababu zifuatazo:

- Kukosa umoja na maelewano kati ya vyama vya upinzani (Rejea UKAWA 2015). Chama tawala ni mbuyu na una mizizi mirefu bila muungano wa kweli haiwezekani kukitoa madarakani.

- Baadhi ya vyama vya upinzani havijitambui vina malengo gani. (Rejea kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kutaka kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na kingine kumpitisha kiongozi wa chama tawala unayempinga kuwa mgombea urais wa chama cha upinzani.) Aidha vyama vingine vya upinzani huonekana wakati wa uchaguzi mkuu tu. Hivi vyama vinafanya mzaha na taasisi ya Urais ama vina malengo gani.

- Watanzani hatutabiriki, wapiga kura ni wachache mno kulingana na takwimu zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi juzi. Hata hao waliojiandikisha bado si wote watakaopiga kura. Elimu / uelewa duni, elimu ya uraia ni duni pia. Zaidi ya 70% ya watanzania ni waathirika wa haya na wengi wao wapo maeneo ya vijijini na ndiyo wapiga kura wanaotegemewa na chama tawala. Bado tuna safari ndefu.

Lazima vyama vya upinzani vifanye jitihada za makusudi kuondoa ubinafsi wa viongozi wao, kuwa na mikakati na agenda endelevu ya kutaka kuchukua dola siyo kusubiri mikakati ya papo kwa papo kuelekea uchaguzi mkuu na kwa bahati mbaya sana tunaelekea uchaguzi mkuu bila Tume Huru ya Uchaguzi.

Kinachowezekana sasa ni kuweka nguvu kubwa kwenye ubunge na udiwani. Kwa mtazamo wangu, bado ni ngumu kukiondoa chama tawala madarakani. Huu ndiyo ukweli japo ni mchungu.

Ni hayo tu
 
Kama kuna mtu Magufuli na CCM wanapaswa kumlaani ni yule aliyetoa wazo la kumpiga risasi Lissu. Huyo ndo mwanaCCM Mpumbavu kuliko wote japokuwa wakati anatoa wazo lake la kipumbavu aliungwa mkono.
Ndio, wakati anatoa wazo alionekana bonge la genius kwenye viunga vya lumumba
 
Wapinzani ni watu, ni ndugu zako, ni rafiki zako na ni Watanzania wenzako. Ukitaka kuua upinzani ni kwamba uko tayari kuwaua Watanzania wenzako na kwa hilo jitihada zake zimeonekana, Watanzania wengi wameumizwa.

Awali Watanzania walikuwa watu wa amani na wakarimu na walijulikana hivyo duniani kote hadi mwaka 2015. Maisha yao yalipoanza kuwa hatarini kwa sababu ya kiongozi moja aliyetaka kuua upinzania, matokeo ndiyo haya.

Watanzania kwa umoja wao wamekataa hizo hila za kuwagawa na mwezi Oktoba nina hakika wataonesha kwa vitendo kwamba ukatili na uonevu si jadi yetu. Watakataa dhulma na ukandamizi kwa mgongo wa hapa kazi tu.

Watarudi kwa ile misingi aliyoianzisha baba wa taifa, Mwalimu Kambarage Julius Nyerere ya uhuru na kazi, uhuru na haki, uhuru na usawa. Madikteta uchwara na malimbukeni watapewa haki yao kwa kurudishwa wanakostahili.
Bahati nzuri au mbaya ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu mshindi ni Tundu Antipas Lissu na ndo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania 2020 - 2025
 
Mimi kama mwana CCM moja ya matamanio yangu ni kuona CCM ikiendelea kushika dola ya Tanzania.

Ila kati ya jambo ninalotamani litokee kwenye muhula wa pili wa Rais Magufuli endapo akifanikiwa kushinda, ni kuacha kabisa kuwachokonoa wapinzani...
Kumetokea wimbi la nyumbu kujifanya ccm halafu wanatoa ushauri.
 
Mimi nitaomba azidishe.

Mpaka wapinzani waingie barabarani. Aape kama rais wa Belarus kwa "labda mniue" .
 
Naenda moja kwa moja kwenye hii mada.

Kumekuwa na mihemko kutoka baadhi ya kundi la watu humu JF wamekuwa wanaandika mada mbalimbali zikimhusu TL, namna ambavyo anaandikwa humu utadhani kama vile TL ataweza kumng'oa mheshimiwa rais JPM au kama vile Chadema itaenda kuing'oa CCM hapo Oktoba panapo majaliwa.

Ukweli ni huu ndugu zanguni CCM haitang'oka wala JPM hatong'oka leo wala kesho wala hiyo Oktoba. Chadema hizi tambo za mitandaoni haziwezi kuwapa nchi, hii nchi haipo JF,FB,INSTA wala Twitter, endeleeni kupost tu kwa hizo ndoto zenu za Bunuwasi.

CCM haing'oki leo wala kesho.
 
Mkuu ukitaka kukiona cha moto, basi endekeza siasa kupitia tuita, jeiefu na in6gtamu.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
kushinda Urais sio kama kuokota nazi ndugu! , endeleeni kuota ,huu uchaguzi kwenye Urais msijidanganye , pambanieni ubunge tu!.. maan si vibaya kuishi kwa matumaini !.
Ana miaka 25 kuchukua nchi Mali
118241772_1733385620133126_8354986880821860104_o.jpg
 
Back
Top Bottom