Ni vizuri kuangalia kila hatua inayosemekana ni unyanyasaji wa upinzani kwa kina, na kufanya hivyo tutaona michango ya upinzani ina manufaa au laa na wapi.
Hatua yeyote ile lazima tujenge uwezo wa kuangalia kwa muono na utafakarishi wa Hypothesis na synthesis analysis.
Kwa kufuata hali hiyo ndio kila kisemwacho au kifanywacho na pande zote ama upinzani au uongozi wa Magufuli utaweza kupata picha halisi kuwa yafanywayo ni sawa au hapana.
Wakosefu au wauwaji wanapo hukumiwa au kifungo kirefu au kifo haipendezi, lakini kufanyika huko kunaweza kuwa ku- deter kurudiwa rudiwa kwa makosa yasio pendeza.
Mkuu Joka kuu, tupo ambao telikuwa waumini wa upinzani wa kweli kwa miaka kadhaa na tukawa viongozi katika ngazi zetu mbali mbali kichama.
Tukitaka kutapika tuna weza ikaonekana kama tunahalalisha matendo ya Magufuli- lakini sisi pia upinzani lazima tujitahidi kutengeneza matendo ya heshima na tabia ambazo CCM wanaweza kutuona katika sura ya utuu. Ikitiliwa maanani demokrasia yetu bado changa.
kWA MFANO: Nakiri bila kushawishiwa serikali ya awamu ya tano kuna vitu vingi vizuri na vya kimaendeleo wamefanya kwa taifa hili.
Tunaposema hawafanya kitu chochote au tunabadilisha maneno kuonyesha kila wafanyayo hayana thamani kwa watu wetu, jee unategemea Magufuli akushangilie kwa kubalisha ukweli wakati umesema uongo?
Kwa maamuzi ya haraka haraka kwa kubadilisha au kudhihaki kila afanyalo Magufuli anaona bora atunyanyase kwa kuwa analipa tunacho mfanyia. Kumdhihaki hata anapofanya kizuri.
Lazima tuabadilike pia ili nao tuwashawishi wabadilike. CROSS CUTTING.
..imepita miaka 4+ tangu Jpm aingie madarakani.
..nadhani tunaweza ku-conclude kwamba Jpm si kiongozi anayeweza ku-co-exist na vyama vya upinzani.
..nimeeleza kwamba binafsi nilianza kuona viashiria vya Jpm kutokukubaliana na demokrasia ya vyama vingi tangu alipokuwa waziri ktk serikali ya Jpm.
..Yapo matamko yake ktk nyakati mbalimbali ambayo yalikuwa yana viashiria vya mambo mabaya ambayo tunayashuhudia leo hii yakiwatokea wapinzani.
..jambo lingine unalopaswa kuangalia ni aina ya kampeni za uchaguzi ambazo Jpm alifanya mwaka 2015. kampeni zile zilijaa MATUSI makubwa-makubwa dhidi ya mpinzani wake, na kwa msingi huo ziliacha MADONDA/MAJERAHA kwa wadau wa uchaguzi ule.
..mshindi mwenye busara, na ukomavu wa kisiasa, alipaswa kuhakikisha kwamba anatibu madonda/majeraha ya kipindi cha kampeni za uchaguzi. Jpm hakushughulika na jambo hilo badala yake alitangaza VITA dhidi ya vyama vya upinzani nchini.
Kuhusu Wapinzani kumsifia / kutomsifia Jpm:
..mimi nadhani wapinzani wakitoa kasoro na mapungufu ya kila aina ndipo tutakapopata nafasi ya kum-appreciate Jpm genuinely.
..wapinzani wasipokuwa "gado" au vigilant, au wakaingia ktk mkumbo wa kusifia na kuabudu, mambo yakiharibika wataingia ktk lawama, kwasababu ni wajibu wao kuikagua na kuikosoa serikali wakati wote.
..Kukosoa maana yake kuna mambo yamefanyika. Jpm angekuwa hajafanya jambo lolote hakuna ambaye angemkosoa.