Ikiwa Kanisa lina mlinzi ambaye ni mwanadamu iweje Watu waombe Ulinzi kwa mungu aliyeshindwa kulinda nyumba yake?


Basi hata huko anakoishi huyo mungu wenu hakuna usalama.
Kama mwanadamu anaweza kulinda nyumba ya mungu wake hiyo inatoa picha kuwa huyo mungu ni dhaifu
 

Hujui ulichoandika.
Nenda kamfuatilie Daudi na Suleiman Mungu aliwaambia nini kuhusu nyumba yake ambayo unasema Mungu hana nyumba
 
Chungeni kauli zenu zisije kuwaponza siku moja.
 
Kwa hii comment
Uzi ufungwe
 
Kwa kuwekewa ulinzi kanisani ina maana moja kubwa sana.
Pamekuwa sehemu ya kukutanikia wahalifu wasiotaka kubadilika, yaani wauaji, wazinzi, majambazi, malaya, waongo, walozi na wadhambi wengine kwa minajili ya kufanya money loundry kwa kumsingizia Mungu ambaye alisema tutoe tuwape maskini. Sasa wananunua vitu vya thamani na kuvificha humo wakiamini wamemnunulia Mungu ambaye ni mmiliki wa vyote.

Neno langu halikuja nitakavyo bali nimevuviwa.

Mwenye akili na afahamu
 
Kama mungu analinda kiroho na si kimwili. Huoni anafeli?

Embu assume hapo wanapolinda watu wawe wanavamia mara kwa mara au chukulia zile nchi ambazo waasi wanavamia na kuua watu kanisani.

Tunasikiliza vipi hilo meno huku tukijua maisha yetu yapo hatarini na mungu huyo yeye kazi yake kulinda kiroho?

Embu fikiria tena na wewe?
 
Uko sahihi kusema MUNGU hahitaji nyumba, yeye ni Roho, kwenye agano jipya yeye hukaa ndani yetu. Mwili ni hekalu lake.

Kuhusu ujenzi wa Nyumba za ibada ni kurahisisha kutaniko la waumini! Na ulinzi unatakiwa kimwili na kiroho, hata nyumbani kwako huwezi kuacha mlango wazi.

Kiranga anazidi kujipatia wafuasi!!
 
Ndugu, Kanisa ni watu wa Mungu ambao bado wanaishi duniani. Watakapoenda mbinguni kukaa na Mungu huko ndo hawatahitaji walinzi lakini duniani bado shetani ana ufalme wake na anaweza kufanya madhara kwa watu wa Mungu akipewa nafasi.

Waefeso 4:27 "wala msimpe Ibilisi nafasi."
Kama watu wataacha mali za kanisa bila ulinzi wowote huku wakijua wako duniani ambamo kuna wezi, majambazi, waporaji n.k. huko ni kumpa Ibilisi nafasi.

Ukumbuke Mungu ni Mfalme, huwezi kumwacha akufanyie vitu ambavyo viko katika uwezo wako kuvifanya. Hata hivyo bado atakulinda na kukulindia mali zako kama alivyoahidi kwa namna ambayo bila msaada wake usingeweza kulinda.

Zaburi 127:1 "Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure."
Kwa neno hili maana yake sio vibaya kuweka walinzi, lakini lazima Mungu apewe nafasi yake na watu watambue yuko Mungu anayelinda kwa namna yake isiyoonekana kwa macho ya kibinadamu. Kama shetani angeruhusiwa au angepata nafasi ya kumdhuru mtu wa Mungu yanaweza kutokea kama yaliyomtokea Ayubu.

Ayubu1:9-10 "Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.

Kwenye hayo maandiko shetani anamwambia Mungu kuwa ni kwa sababu ya ulinzi wake ndo maana Ayubu anamcha Mungu, la sivyo asingemcha. Kama ukisoma zaidi utaona Mungu alimruhusu shetani kumshambulia Ayubu kwa kuondoa ulinzi wake na kilichotokea nadhani wengi tunakifahamu.

Hivyo Mungu analinda watu wake lakini sio katika namna ambayo inaonekana kwa macho ya kibinadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…