Ikiwa Mazishi ni Ibada, basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao

Ikiwa Mazishi ni Ibada, basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao

Nyama msibani inafanyaje?kwani imefanyiwa tambiko lolote?
Baadhi/Wengi wasiookoka, ingawa Si wote,,wenye kushika Mila mbovu,katika misiba Hasa ktk arobaini, huchanganya na kipande Cha nyama ya mfu au maji au uchafu wa marehemu kimazingara sufuriani Ili mshiriki chakula kama IBADA na mfu.

Ni vizuri kutakasa chakula kabla ya kula, bt kuondoa sintofahamu Kwa tahadhari epuka kula nyama misibani.

Magonjwa mengi ya kuoza mwilini au kansa ni matokeo ya kula nyama au uchafu wa wafu.

Misibani Huwa ni Mahali spesho wachawi huwatafuta watu kupitia vyakula. Sababu katika msiba wenye watu 100 Kwa Mfano, uwe na HAKIKA hutakosa wachawi 20 au zaidi.

Sorry kukwambia mambo ambayo yaeza kuwa beyond your expectation.
 
Ikiwa Mazishi ni Ibada , Basi Usiingilie Ibada za Wafu . Waache Wafu Wawazike Wafu Wenzao..
💫💫💫💫💫

©️Mwl. Makungu m.s
0743781910

Wana Heri wafu wafao katika Bwana. Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa Matendo yao yafuatana nao ( ufunuo 14:13).

Maana wafu wote wanalo tumaini ya kuwa Siku moja watatafufuliwa . Lakini ni wafu wachache walio na uhakika wa wapi wataelekea baada ya kufufuliwa.

Ni utamaduni wetu wa kuziosha maiti na kuzisafisha na kuzivalisha suti au sanda . Lkn yote hayo ni maandalizi ya kuzifukia chini ya udongo.

Nenda kaizike maiti , lkn usiingilie ibada za wafu.
Huwa tunazika maiti, lkn hatuziki wafu. Wafu hawafi. Wafu wanaishi . Pengine hujanielewa Bado . Ni hivi , huwa tunazika miili ya wafu lkn hatuwaziki wafu. tunazika mwili lkn hatuziki nafsi . Nafsi haifi.

Umepata kusoma kisa cha Lazaro na tajiri ktk Biblia? Wote wawili walikuwa wafu . Miili yao iliishazikwa zamani duniani . Lakini wanaonekana wako mahali fulani tofauti wakiwa hai wanajadiliana . Mmoja anastarehe mwingine anataabika. Miili inakufa ,maiti zinazikwa , lakini Wafu wanaishi.

Ufunuo wa Yohana 6:9 " Na alipoifungua muhuri ya tano , nikaona chini ya madhabau roho zao waliochinjwa kwaajili ya neno la Mungu , na kwaajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema , Ee Mola , Mtakatifu , Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu , Wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi ? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu , nyeupe , wakaambiwa wastarehe Bado muda mchache , hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na Ndugu zao , watakaouawa vile vile Kama wao."

Ukisoma hapo juu unapata picha gani juu ya wafu ? Kuna Wafu wapo hai wanastarehe.

Unakumbuka Yesu alitokewa na Nani pale mlimani wakati akiomba? Alitokewa na wafu, nabii Musa na nabii Elia wakazungumza nae. Kwa lugha ya kiswahili sanifu Tunasema alitokewa na mizimu( yaani watu waliowahi kuishi katika hii dunia na baadae wakafa au wakaondoka ktk hii dunia) . Mzimu wa Musa na mzimu wa Elia . Wafu hawafi , wafu wanaishi. Inayokufa ni miili..

Yule Mwanamke mwenye pepo wa utambuzi ( mchawi/ mganga) anamwambia mfalme Sauli je! Ni Nani nitakayekupandishia? Naye akasema , Nipandishie Samweli ( nabii ambaye amekwishakufa na kuzikwa) . Yule mwanamke akampandisha Samwel kutoka ktk nchi ( ardhi/ kuzimu) . Nao nabii Samwel ( mzimu) na mfalme Sauli wakazungumza ..

Japo wanatheolojia wengine huwa wanasema kuwa Samwel aliyepandishwa toka kuzimu siyo Samwel . Ni pepo , jini au shetani lililojivika mwili wa Samweli. Lakini ukilisoma andiko hili ktk Biblia Hakuna mahali wala mstari wowote pameandikwa kukanusha kuwa yule alikuwa ni Samwel wa uongo, pepo , jini au shetani aliyezuka. Hili la Samwel wa uongo au wa ukweli siyo somo langu kwa leo . Leo nataka tu kukwambia kuwa * wafu wanaishi* .. Wanaishi katika dunia yao . Wanaishi katika ulimwengu wa roho. Wapo walio kuzimu na wapo waliokwisha tangulia peponi. Wanaishi maisha yao .

Kama wewe Bado mwili wako una uhai na uzima Basi usiingilie maisha ya wafu.

Lakini ktk Injili Yesu anakuja kutuonesha kitu cha tofauti kbs . Siyo tu kwamba Wafu wapo kuzimu na peponi tu , bali kuna wafu wapo duniani. Tupo nao tunaishi nao .

Yesu anamwambia mtu aliyemuomba akamzike baba yake, "waache wafu wawazike wafu wenzao" .

Huyu mtu anamuomba Yesu aende akauzike mwili wa baba yake , lkn Yesu anamwambia waache wafu wawazike wafu wenzao.
Hapa tunaona ya kuwa Kumbe Kuna Wafu wapo duniani ,wanatembea, wanaongea , wanakula , na pengine wanaongoza watu. Maana wafu waliokufa mwili wasingeweza kwenda kuuzika mwili wa mfu mwenzao .
Hii tafsiri yake ni kwamba , mwili huu wa mfu aliyetakiwa kwenda kuzikwa ulienda kuzikwa na watu wafu ambao hawajakufa mwili. Wamekufa rohoni na akilini. Nielewe vizuri hapa , hawajakufa roho Wala hawajakufa akili ,Bali wamekufa rohoni na akilini.
Miili yao ipo hai. Roho zao zipo hai . Akili zao zipo hai . Lkn Matendo yao ya mwili yanayoongozwa na roho na akili siyo Matendo yanayostahili kuwa ya mtu aliye hai rohoni ..
Wanahesabika kuwa wamekufa ktk ulimwengu wa roho..

Ikiwa mazishi ni ibada . Basi usiingilie ibada za wafu waache wafu wawazike wafu wenzao.

Kuna watu tupo nao tunaishi nso lkn waliishakufa tyr . Ni wafu . Matendo yao machafu , ya kinyama hayastahili kuwa ya Binadamu aliye hai.
Mtu akiishakufa amekufa . Ameondoka ktk ulimwengu huu .
Japo ni utamaduni, lkn Hata tukijitahidi kuuosha, kuusafisha, kuutakasa na kuuvalisha vizuri mwili wake, Haiondoi ukweli ya kuwa anakwenda kufukiwa na udongo chini ya ardhi.

Kwanini unahangaika kuwasafisha wafu ( sijasema maiti) . Unatumia gharama kubwa , muda wako na nguvu zako bure kuwasafisha wafu na unajua ya kuwa huwezi kubadilisha ukweli kuwa wanaenda kufukiwa na udongo chini ya ardhi!!??

Usiingilie ibada za wafu waache wafu wawazike wafu wenzao.

Wafu wanaelewana vizuri . Wanapata na muda Wanapiga story zao km Lazaro na tajiri. Wewe unaingilia story zao ambazo hazikuhusu. Unataka kumsafisha tajiri mfu . Mfu ni mfu tu . Haibadilishi ukweli hata Kama akitokea km mzimu wa Musa na Elia. Aliishakufa. Hayupo ktk dunia hii.

Ukihangaika kumsafisha mfu iwe ni bure au kwa gharama nawe unageuka kuwa mfu unayetembea . Wote mnakuwa wafu. Mmekufa kiroho na kiakili..

Je! Unaishi na mfu? Unafanya kazi na mfu? Unasoma na mfu ? Unaongozwa na mfu ? Unaongoza wafu?

Kuwa makini . Wafu wanaotembea wamekufa kiroho na kiakili . Ni wabaya wachafu kuliko wafu waliokufa kimwili .

Mungu JEHOVA wasamehe wafu wanaotembea maana hawajui walitendalo . Lkn wasaidie Sana wahangaikao kuwasafisha wafu maana hawajui kuwa wanageuka kuwa wafu wa kiakili . .

Ikiwa mazishi ni ibada Basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao.

Makungu m.s
0743781910
23 April 2023
Uongo
 
Siku ukinielewa dini yako haitakuwa Ukristo au uislam, Bali itakuwa Upendo, Haki, ukweli na Akili.
Utawapenda Watu bila kujali tofauti zao/zenu.
Utawaweka Watu katika makundi Yao ili usije ukawadhulumu Haki zao.

Karibu Sana Tibeli
Pamoja na matendo hayo yote mema,

Kama hujamkiri Yesu kuwa mwokozi wa maisha Yako, wewe ni Kuni ilotunzwa Kwa moto wa Jehanum,

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Baadhi/Wengi wasiookoka, ingawa Si wote,,wenye kushika Mila mbovu,katika misiba Hasa ktk arobaini, huchanganya na kipande Cha nyama ya mfu au maji au uchafu wa marehemu kimazingara sufuriani Ili mshiriki chakula kama IBADA na mfu.

Ni vizuri kutakasa chakula kabla ya kula, bt kuondoa sintofahamu Kwa tahadhari epuka kula nyama misibani.

Magonjwa mengi ya kuoza mwilini au kansa ni matokeo ya kula nyama au uchafu wa wafu.

Misibani Huwa ni Mahali spesho wachawi huwatafuta watu kupitia vyakula.

Sorry kukwambia mambo ambayo yaeza kuwa beyond your expectation.
Duh,Kwa hiyo mfu anakatwa kipande cha mwili wake?
Hapo kwenye Kansa pana ukakasi,umeongea kama layman.....tafute muda ujifunze
 
Duh,Kwa hiyo mfu anakatwa kipande cha mwili wake?
Hapo kwenye Kansa pana ukakasi,umeongea kama layman.....tafute muda ujifunze
Si Kila kansa au uvumbe hutokana na niliyoyaandika,

Mm naongea ktk perspective ya kiroho,

Kama huamini hiyo ni case ingine.

Omba Uzima, ukitoboa miaka 60+ utakuwa shuhuda mzuri wa niliyoandika Kwa experience kabisa,

Maana kuishi kwingi ni kuona mengi.

Bt pia okoka kama hujafanya hivyo, utapata ulinzi wa direct, utaambiwa nini Cha kufanya uwapo ktk risk.

Sawa mkuu
 
Siku ukinielewa dini yako haitakuwa Ukristo au uislam, Bali itakuwa Upendo, Haki, ukweli na Akili.
Utawapenda Watu bila kujali tofauti zao/zenu.
Utawaweka Watu katika makundi Yao ili usije ukawadhulumu Haki zao.

Karibu Sana Tibeli
Na akikuelewa atakuwa Freemason.

Freemason ndiyo upendo, haki, ukweli, maarifa na undugu wa kusaidiana ili kupinga habari za uongo wa kidini.

Hawawezi kuelewa freemason kwasababu ni dhana ambayo imejengewa conspiracy theories nyingo kiasi kwamba huwezi pata ukweli wake.

Yaani ni hearsey tu za wafia dini.
 
Kumbe uko chama la masonry, Upumbavu huo ni Mzigo mzito sana.

Maybe utafunguliwa, who knows!!
 
Wakristo someni Biblia,
Mpate kuijua kweli,
Nayo kweli itawaweka huru,
Mtoa mada katoa neno,
Ila linaukakasi,
Mimi binafsi sikubaliani na tafsiri ya mtoa mada.
Kuutafuta ukweli kwenye biblia ni sawa kabisa na kutafuta mwanamke mrembo mwenye uume mrefu.
 
Kumbe uko chama la masonry, Upumbavu huo ni Mzigo mzito sana.

Maybe utafunguliwa, who knows!!
Ndo hawa watu ambao ninawalenga.

Ufinyu wa akili na kujifungia milango ya uelewa.
Akili zote umeshikiliziwa.

Hutaki kujifunza.

Yote ya yote nmeongea hoja zangu vzuri, lakini zimetukanwa bila kupanguliwa.

Akili yako inauwezo mkubwa zaidi ya hapo ulipo sasa.
 
Pamoja na matendo hayo yote mema,

Kama hujamkiri Yesu kuwa mwokozi wa maisha Yako, wewe ni Kuni ilotunzwa Kwa moto wa Jehanum,

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
Kwamba mpaka umkiri yesu ni mwokozi wa maisha?

Ukimkiri hautokufa?
Ukimkiri utapona kwenye ajari?

Mwokozi wa maisha yapi wewe unayaongelea.

Kwanini huyo Mungu Mjuzi wa yote na muweza wa yote na mwenye upendo wote anachezea watu michezo mibaya?
Anachezea watu michezo mibaya kwasababu kila baya ambalo anataka umkiri akuokoe, yeye ndiye kalitengeneza/kalipanga litokee.
Unaelewa hata hilo?
 
Baadhi/Wengi wasiookoka, ingawa Si wote,,wenye kushika Mila mbovu,katika misiba Hasa ktk arobaini, huchanganya na kipande Cha nyama ya mfu au maji au uchafu wa marehemu kimazingara sufuriani Ili mshiriki chakula kama IBADA na mfu.

Ni vizuri kutakasa chakula kabla ya kula, bt kuondoa sintofahamu Kwa tahadhari epuka kula nyama misibani.

Magonjwa mengi ya kuoza mwilini au kansa ni matokeo ya kula nyama au uchafu wa wafu.

Misibani Huwa ni Mahali spesho wachawi huwatafuta watu kupitia vyakula. Sababu katika msiba wenye watu 100 Kwa Mfano, uwe na HAKIKA hutakosa wachawi 20 au zaidi.

Sorry kukwambia mambo ambayo yaeza kuwa beyond your expectation.
Mauongo uongo tu.

Hzo ni Imani zako potofu.

Kama unabisha thibitisha habari za misibani kula vyakula vyenye maji yalooshewa maiti
 
Biblia ni neno la Mungu,na Biblia inasema "Heri WAFU WAFAO katika bwana"

Wewe unasema huwa tunazika maiti,hatuziki wafu....WAFU HAWAFI wafu wanaishi.....
Maelezo yako ya mwanzo yamejikita kuelezea kwamba unaokufa ni mwili,ila nafsi inaishi,,,hivyo WAFU wanaishi.

Paragraph za chini unatilia mkazo,Hakuna haja ya kuhangaika na WAFU,mfu ni mfu haijalishi utamsafisha kiasi gani haitabadilisha ukweli umeshakufa na anaenda kufukiwa na udongo.

Sasa Huoni unaleta mkanganyiko hapo,,, paragraph ya juu ulituambia WAFU HAWAFI, paragraph ya chini unatuambia WAFU WAKIFA WAMEKUFA.....Sasa hapa ndio kwenye mkanganyiko which is which?
Ukiangalia kwa umakini utaona Nimezungumzia wafu wa aina . Wafu ambao miili yao iliishazikwa na wafu ambao wako hai kimwili lkn wamekufa ktk utu wao rohoni /nafsini .
 
Kwa hiyo kama watu wa Mungu,ambao ndio tunaiga mfano kwao walikuwa wanaheshimu wafu mababu zao waliotangulia,Kwa nini sisi unatusisitizia tuachane na mambo Yao?
Kuna tofauti Kati ya kuheshimu na kuingilia . Lkn pia ukiangalia kwa umakini utaona Nimezungumzia wafu wa aina mbili . Wafu ambao miili yao iliishazikwa na wafu ambao wako hai kimwili lkn wamekufa ktk utu wao rohoni nafsini.. Ni falsafa hiyo isome kwa umakini
 
A
Umechambua vizuri hoja Yako,ila Mimi natatizwa sana na wewe unapopendaga kubadilisha maandiko na kuassume mambo Yako.
Hapo kwenye kisa Cha sauli Kwa Nini umekazania kusema yule muonaji alimdanganya Sauli?Kwa ufahamu wangu biblia ni kitabu kipo straight sana,kama alimdanganya kingesema pia,wewe huu mpango wa kubadilibadili mambo umekaa vipi?
Ahsante sana
 
Duuuu
Kwamba mpaka umkiri yesu ni mwokozi wa maisha?

Ukimkiri hautokufa?
Ukimkiri utapona kwenye ajari?

Mwokozi wa maisha yapi wewe unayaongelea.

Kwanini huyo Mungu Mjuzi wa yote na muweza wa yote na mwenye upendo wote anachezea watu michezo mibaya?
Anachezea watu michezo mibaya kwasababu kila baya ambalo anataka umkiri akuokoe, yeye ndiye kalitengeneza/kalipanga litokee.
Unaelewa hata hilo?
Duuuu
 
Siku ukinielewa dini yako haitakuwa Ukristo au uislam, Bali itakuwa Upendo, Haki, ukweli na Akili.
Utawapenda Watu bila kujali tofauti zao/zenu.
Utawaweka Watu katika makundi Yao ili usije ukawadhulumu Haki zao.

Karibu Sana Tibeli
Ukristo ni all about love, no judging anybody, the greatest commandment in Christianity in LOVE TO YOUR CREATOR and to your NEIGHBOR...... Ukristo SIO dini ni Uhusiano wa Wanadamu na Mungu kupitia Yesu.....
 
Utibeli hi mambo haya manne
1. Upendo,
2. Haki
3. Ukweli
4. Akili

Ukristo unaupungufu wa hayo Matatu yaliyobakia.
 
Back
Top Bottom