Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Kwa mtazamo wangu nadhani maamuzi mengine yanahitaji fikra yakinifu na si msukumo wa wadau.
Ikiwa wametangaza siku ya sensa kuwa siku ya mapumziko, na kwa nijuavyo si rahisi karani kuzifikia kaya zote kwa siku moja.
Labda kama mapumziko hayo yangekuwa ya wiki nzima. Ama sivyo, watumishi wangepewa siku moja maalum ya kupumzika kwa kuwasiliana na karani au mwenyekiti wa eneo lake kwa siku ambayo karani atafika kwenye kaya yake.
Maana lengo kuu ni kupata taarifa sahihi kutoka kwa wahusika. Sasa hili la siku moja ya mapumziko lina tija kweli?