Ikiwa tarehe 23 August ni mapumziko, je karani atazifikia kaya zote kwa siku hiyo?

Ikiwa tarehe 23 August ni mapumziko, je karani atazifikia kaya zote kwa siku hiyo?

Hapana. Sikuhitaji kabisa.
Hiyo kazi si lelemama japo unapata kipato. Yaani jua lako, mvua yako. Unapandisha milima na mabonde. Unafika mahali unagonga hodi kwa nyumba ya watu...
Ni ya kidigitali ina mfumo maalum.

Hakuna mfumo unaochukua taarifa bila kuwa na mtu wa kuingiza..

Yaani taarifa zitoke tu mtaani ziense NBS, khaaa haiwezekani.
 
Tusiwe wepesi wakubeza Kila serikali inayolipanga, Bali tuwe mstari wa mbele kuchangia Nini kifanyike siku hiyo ya mapumnziko, mfano MKUU WA KAYA SIKU HIYO YA MAPUMNZIKO anaweza akachukua karatasi akaandika majina YOTE ya wanakaya yake waliolala usiku was kuamkia 23 kuanzia yeye,MWENZA wake HALAFU watoto wake na miaka yao.

Kwa Kila MMOJA na ndugu wengine au watu wengine waliolala kwake,ili hata kama karani asipofika siku hiyo akute Kuna TAARIFA za kutosha katika mji huo. Tusiwe wa kubeza TU Kila serikali isemalo, SERIKALI Ni watu na Ni BINADAMU TUSHAURI NINI KIFANYIKE SIKU HIYO.

Naunga mkono wazo la kupumnzika ila MKUU WA KAYA AORODHESHE MAJINA,UMRI JINSI, NA NAMBA ZA VITAMBULISHO VYA NIDA na aviache kwa mtu yeyote atakayebaki nyumbani ili hata KARANI akifika siku nne BAADAE akute TAARIFA za kutosha. Lakini pia mkuu wa KAYA anaweza akaandaa familia yake kwa zoezi la sensa.
 
Ukweli ni kwamba, huwezi kuwa na kazi yako ya maana au biashara zako zinakupa kipato, ukaenda kubanana kwenye ajira za sensa tena ukarani!

Yaani kufight kwenye hizi ajira ni kiashiria cha wazi kabisa cha namna watanzania tulivyo na hali ngumu kiuchumi.
Just imagine umebeba begi lina vitendea kazi, umevaa laba miguuni (ukivaa viatu vya wazi jiandae kujaa vumbi au viatu kukatika) unazunguka nyumba moja baada ya nyingine, unaanza kuuliza maswali takribani 100+ then unajaza taarifa na kutuma mahali husika. Nikwambie tu, hii ni kazi ya kizalendo haihitaji ubrothermen au usister do! Ni kazi ya kikomavu!
Wapo watumishi wa umma, sekta binafsi wamepambana na wametamani sana kufanya kazi hii.

Wapo wake, watoto wa vigogo wamewekwa kufanya kazi hii.

Ni wewe pekee au mko wachache sana msiotaka kazi hii.
 
Itakuwa ni siku ya kuandaa majawabu sahihi na kuyaacha nyumbani ili hata makarani wakija kwa kuchelewa watayakuta. Usijipe stress za bureeeeee!
Unafahamu idadi ya maswali kwenye dodoso?
Wanasema ni 100 !!!
 
Makarani ehh
Vyovyote iwavyo
Mje mmeshiba
Niliwapikia leo na hamkutokea
 
Tija ipo sana, labda kwako wewe usiyejua, mapumziko yamelenga kwa wananchi wala sio makalani.
sengobad vipi ulihesabiwa siku uliyopumzika?
Tujitahidi kwwnye haya maisha kuheshimu mawazo ya great thinkers hata kama hawana cheo au umaarufu.

Nilipotuma hii hoja nilijua nini namaanisha. Hadi leo kaya nyingi hazijahesabiwa. Hakukuwa na haja ya mapumziko!
 
sengobad vipi ulihesabiwa siku uliyopumzika?
Tujitahidi kwwnye haya maisha kuheshimu mawazo ya great thinkers hata kama hawana cheo au umaarufu.

Nilipotuma hii hoja nilijua nini namaanisha. Hadi leo kaya nyingi hazijahesabiwa. Hakukuwa na haja ya mapumziko!
Naheshimu sana mawazo yako mkuu, lkn je kuna karani aliyekwama kwa sababu ya kukosa wanakaya ?
 
Back
Top Bottom