Hilo zoezi la sensa litaendelea kwa siku sita kulingana na nilivyosikia mwanzo, na kila siku hapo karani wa sensa atakuwa na majukumu tofauti, kuna kujua hesabu ya watu waliolala kwenye kaya husika, kujua idadi na wazee, vijana, wanawake, watoto, na wanaume, n.k
Naona kama wamelirefusha hilo zoezi makusudi ili angalau makarani wa sensa wawe busy, ili watakapokuja kulipwa, ionekane kweli walikuwa kazini.
Otherwise hilo zoezi naona lingeweza kuchukua hata siku moja likamilike, hii siku moja ya mapumziko kwangu ni kama siku ya kusherehekea kuanza kwa sensa Tanzania.