Maanake ni kwamba hiyo siku karani atahesabu kaya kadhaa, kisha ataendelea kwa siku inayofuata. Je, mapumziko yataendelea kwa kaya amabazo hazikufikiwa???
Kwenye hili, ilikuwa rahisi zaidi kwa mwenyekiti au mtendaji wa mtaa/kijiji kwa kushirikiana na karani, kumtaarifu mhusika awepo nyumbani kwa siku husika. Uzuri ni kwamba wenyeviti wanawajua watu wao.
Sasa tija ya mapumziko ya siku moja ipo kweli? Karani atatembelea kaya zote kwa siku hiyo? Kwani 2012, ilikuwaje? Watu walipumzika?
Washauri wa rais wamsaidie kitaalam zaidi na si kwa mhemko! Kwa kifupi hayo mapumziko hayana tija!