Ikiwa tumekufa tutaweza kutambua kama tumekufa?

Ikiwa tumekufa tutaweza kutambua kama tumekufa?

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Habarini wana JF,

Leo nimekaa nimewaza sana na kujiuliza maswali mengi ambayo nimependa kushare nanyi.

Je, roho itakapotoka tutakua na hisia kua tumeshafariki?

Tutaweza kuona matukio yanayoendelea hali ya kua macho yameshafumba?

Vipi kuhusu vilio vya wapendwa wetu tutaweza kuvisikia?
 
Yohana 11:11 Baada ya kusema haya Yesu aliongezea kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”

12 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bila shaka atapona.” 13 Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa. Walidhani amesema Lazaro amelala usingizi. 14 Kwa hiyo Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa.

Mhubiri 9:5​

Screenshot 2024-04-19 122807.png
 
Maswali mingine jamani😂😂😂kama mtu unataka kujinyonga vile
Hapana ndugu inafikirisha.
Imagine that feeling kama utakua unaweza sikia ndugu wakilia lakini huna uwezo wa kuwaona.
 
hii injili usipoijua utaabudu shetani ukidhani unashughulika na ndugu zako waliokufa
mtu akifa hakuna chochote kinaendelea, kama kipo ni Mungu mwenyewe anajua
 
yani ufe halafu utambue umekufa!! hivi kifo mnakichukuliaje nyie nyumbu..?
acheni kudanganyana kufa ni sawasawa na kama vile kabla yakuzaliwa kwako!. wewe unaehisi hali zote huo ndio ufahamu na ndio uhai huo nje na hapo nothing!.
yasikudanganye hayo mavitabu toka huko ughaibuni hizo ni fikra na utamaduni
 
Kwa kifupi tulikuwa hatupo, tumewepo na hatimae hatutokuwepo tena.

Uuonavyo mchicha ndivvyo mwanadamu alivyo...

Katika mbegu nyingi za mchicha kuna ambazo zinaota na nyingine kupotea pasipo kumea. Sasa katika mbegu zilizomea na ambazo hazikumea, ziliwezekana kuwepo kupitia mambo mengi ikiwemo wazazi wao/mchicha uliotoa hizo mbegu.

Hivyo basi kama wewe upo, inamaanisha kuna vingi vimewezesha wewe kuwepo lakini vitu hivyo havina utambuzi wala haviwezi kukufanya uendelee kuwepo milele sababu navyo havina uwezo wala utambuzi wa kufanya hivyo.
Sasa utambuzi wako kiduchu ukiuchanganya na tambuzi za wengine zisikupige upovu usahau kwamba maisha ni sasa.

Ukitoka nje ya wakati uliopo maana yake unabeba jukumu ambalo sio lako!.
Simaanishi tusitoke nje ya wakati uliopo kwasababu tunaposhikamana na nyakati zote 3, ndipo tunatengeneza future ya wanadamu wengine hasa wale wajao japo hawatuhusu hata kidogo.

Maisha yanaeleweka sana sema ujuaji wetu ndio unayafanya maisha yawe marefu kitu ambacho kila mwenye kuunusa ukweli wa uwepo wetu hapa ameshaelewa maisha hayana maana yoyote.

Yeyote anaesoma comment yangu ajue maisha yake hayana faida yoyote kwake bali wanaonufaika naye ni waliotengeneza mnyororo wa uhai wake japo kwa 99+ hatujulikani kwenye mamlaka zenyewe ingali faida zetu ndizo zinawafanya waogelee kwenye furaha.
 
Ukishakufa ndiyo utajua, kwa sasa hakuna mwenye kufahamu kwa sababu tu hai.
 
Ukifa unajua kama umekufa na kupitia roho yako ambayo inakuwa imeuacha mwili.

Inakuwa inaona kila kitu.
Kama ndiyo hivyo basi hakuna kitu kinachoitwa kifo kwa mwanadamu sasa.

Kifo = kukoma kwa uhai
 
Habarini wana JF,

Leo nimekaa nimewaza sana na kujiuliza maswali mengi ambayo nimependa kushare nanyi.

Je, roho itakapotoka tutakua na hisia kua tumeshafariki?

Tutaweza kuona matukio yanayoendelea hali ya kua macho yameshafumba?

Vipi kuhusu vilio vya wapendwa wetu tutaweza kuvisikia?
Mtu anapokufa roho yake inatoka ndani ya kava lake yaani mwili na inaenda aidha kwa Mungu au kwa Shetani kwa hiyo utajua kabisa umekufa by the way zile seconds chache wakati roho inatoka kwenye mwili ni kama vile roho inaamka na kuanza maisha ya rohoni so unajua kabisa.
Kuhusu kuona matukio au kutokuona sidhan maana kumbuka wewe wakati huo unakuwa haupo tena duniani kilichopo ni mwili wako ambao hauna tena muunganuko na roho yako na infact mwili huo umeshokosa kabisa 100% ya kufanya kazi.
Vilio vya wapendwa wala hutovisikia.
 
Ukifa unaridi ulikotoka, ambapo wote hatupajui ila wale walokufa tu. Hakuna jibu jingine zaidi ya hilo.

Ishi maisha yako kikamilifu.
 
Kwahiyo usikute tumekufa hii ni simulation tu
 
Habarini wana JF,

Leo nimekaa nimewaza sana na kujiuliza maswali mengi ambayo nimependa kushare nanyi.

Je, roho itakapotoka tutakua na hisia kua tumeshafariki?

Tutaweza kuona matukio yanayoendelea hali ya kua macho yameshafumba?

Vipi kuhusu vilio vya wapendwa wetu tutaweza kuvisikia?
Nikuulize swali rahisi. Kabla hujazaliwa ulikuwa unajua bado hujazaliwa? Hata bado ukiwa mimba ulikuwa unajua kuwa wakati ule wewe ni mimba?
 
Back
Top Bottom