Uchaguzi 2020 Ikiwa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA ulikuwa ule, basi muacheni Lowassa aitwe Lowassa

Uchaguzi 2020 Ikiwa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA ulikuwa ule, basi muacheni Lowassa aitwe Lowassa

Kejuu

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
645
Reaction score
906
Ndugu Watanzania wenzangu,

Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kutupa uzima na kuiona siku hii ya leo.

Kwa kifupi sana, naamini jana wote tulijionea hali halisi ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA, na hii imetudhihirisha kuwa mzee Lowassa ilikuwa namba nyingine kabisa, na hatakuja kutokea mtu mwingine wa mvuto wa kisiasa kama mzee yule katika chaguzi za hivi karibuni. Katika nyuzi zangu, niliwahi kudokeza kuwa Mh. Tundu Lissu hawezi kufikia hata nusu ya mzee Lowassa, yule mzee alikuwa si mtu wa kawaida.

Aidha, kwa mliokuwa mkifuatilia kampeni za 2015, uzinduzi wa kampeni za UKAWA pale Jangwani, naamini ulipeleka taharuki kubwa sana kwa CMM, lakini kwa nilichokiona jana, basi nadiriki kusema kuwa, uzinduzi huu umepeleka taarifa ya ushindi mkubwa sana kwa CCM na kuwaona CHADEMA safari hii mko DHAIFU MNO AND POORLY ORGANIZED.

Kosa kubwa kwa CHADEMA jana, wamekosa kuchukulia ile siku ya jana kuwa very seriously, huku wakishindwa kujua kuwa NYUMBA IMARA INATOKANA NA MSINGI IMARA, THAT IS, FIRST IMPRESSION MATTER A LOT. Kwa maoni yangu, nadhani uzi wa Salary slip uliokuwa unawashauri wasinzindue kampeni badala yake wafuatilie suala la wagombea wao walioenguliwa, nadhani hii ndiyo boko ya kwanza kutoa. Kama kungekuwa na think tanks wa kueleweka wangefanya mambo yafuatayo ili kunusuru siku ya kuzindua kampeni kwa kufanaya jambo jingine kabisa, ambayo ni kinyume na matarajio ya watanzania wengi:
  1. Uongozi wa cdm ungeita wanahabari asubuhi na mapema kuongelea suala hilo la kuenguliwa kwa wagombea wao
  2. Press hii ingeambatana na uongozi wote wa cdm na baadhi ya wabunge mashuhuri wa CDM ili kuonyesha wako serious na hii kitu
  3. Uzinduzi wa ilani ulikuwa unatakiwa ufanyike siku ya jana hiyo hiyo na siyo kusubiri siku nyingine tena.
Kilichotokea jana pale Mbagala kitakuwa kimeacha maswali mengi sana kwa umma watanzania kama ifuataavyo:
  1. Kuna uwezekano mkubwa CDM kampeni plan yao inakosa mathink tanks kama ilivyokuwa 2015, ambayo ilikuwa na akina Kingunge, Sumaye, Lowasa, etc.
  2. Kuna uwezekano ndani ya CDM kulikuwa na kutoelewana nini kifanyike katika siku ya jana
  3. Uzi wa Salary Slip ulicompromise siku ya jana
Kuna haja ya CDM kujipanga sana katika siku zijazo, la sivyo mgombea wao atapoteana sana. Sambamba na hilo, kipindi kile TL ilikuwa one man show wakati wa kutafuta wadhamini, saizi kuna utitiri wa vyama unakuja, na wazee wa kazi CCM wanazindua leo, angalieni itakavyokuwa mjifunze kutoka kwenye chama kikongwe barani Africa.

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu
 
Yaan hivi hata Lissu mwenyewe alikuwa ajui kilichokuwa kinaendelea alishangaa tuu kuona mbona mambo yana badilika wakati akipitia hotuba aliyokuwa ameiandaa. Mbowe alivyoingia tu alipanic baada ya kukuta hamna watu. Yule MC pia hakuamini kilichotokea. yaan wako disorganised kabisa. Wanaenda na upepo. Wachungaji na mashehe waliofungua niliona wakiinamisha kichwa chini wakisema nimetoka wapi na huu usanii.
 
Acha kukariri,Sasa hivi watu wanafatilia michakato mtandanoni,ni ccm imebaki kusafirisha watu toka mbali kujaza uwanja.
Kama mnajiamini achilieni tume iwe huru muone.
 
CDM kwakweli ukiwasikiliza humu ndani ya jamvi unaweza ona wapo serious, ukiangalia mlolongo mziwa wa jana kwakweli umenifikirisha hivi hawa ni watu ambao wapo serious na wanachokifanya, hii ni sawa na kuonja sumu na kujiaminisha ni asali, hata body language ya mboye haikuwa sawa, jukwaa lenyewe ni kama la kigodoro poor CDM.
 
Acha kukariri,Sasa hivi watu wanafatilia michakato mtandanoni,ni ccm imebaki kusafirisha watu toka mbali kujaza uwanja.
Kama mnajiamini achilieni tume iwe huru muone.
Mtandaoni ee! aya jidanganye. had mwananchi wa kijijin kule yuko mtandaon. Juz alivyokua akizunguka masokon na barabaran na vijana wa pikipiki sisi tulikuwa tunashanga matukio tu.
 
Assessment yangu ya haraka kwa mkutano wa Jana ni kuwa Chadema hawana fedha za kuendesha kampeni ya viwango.

Dunia nzima unahitaji fedha kufanya kampeni za viwango.

Kila kitu kilikuwa duni, na ndio hapo utaona namna fedha za Lowasa zilivyoipa nguvu Chadema kwa wakati ule.
 
Tumieni hata logical reasoning

Enthusiasm ya mbagala ilichangiwa na vitu vingi.

1. Uzinduzi sehemu nyingi.
Kwahiyo watu wa kawe na maeneo ya jirani wanasubiri kwao, hawakwenda mbagala.
2. Pale ni CHADEMA Tu na sio UKAWA
3. Hakuna wasanii

mbona hesabu ni simple.

2015 uwingi wa watu walichangiwa na wasanii+ lowasa(CHADEMA +CCM)+ Seif+NCCR+CUF +NLD

This time vyote hivyo havipo ni CDM plainly sasa unataka waweje?
 
Yaan hiv hata Lissu mwenyewe alikuwa ajui kilichokuwa kinaendelea alishangaa tuu kuona mbona mambo yana badilika wakati.akipitia hotuba aliyokuwa ameiandaa. Mbowe alivyoingia tuu alipanic baada ya kukuta hamna watu. Yule Mc pia hakuamini kilichotokea. yaan wako disorganised kabisa. wanaenda na upepo. Wachungaji na mashehe waliofungua niliona wakiinamisha kichwa chini wakisema nimetoka wap na huu usanii
Wakiambiwa ukweli, huwa hawakubali hawa jamaa, ngoja tuone.
 
Kimkakati Uongozi wa CDM ulishafeli ,labda tuone leo! Ila ki ukweli upinzani bado sana na haupo makini na uchaguzi! Matokeo watakayo yapata oktoba wasimtafute mchawi nani!. Sisi tutaendelea kuwapa ukweli tu , japo mchungu kwao!.
Halafu waje waseme wameibiwa kura. Kwa kampein ile ya jana hata asilimia tano ya kura hawatapata.
 
Acha kukariri,Sasa hivi watu wanafatilia michakato mtandanoni,ni ccm imebaki kusafirisha watu toka mbali kujaza uwanja.
Kama mnajiamini achilieni tume iwe huru muone.
Michakato mtandaoni my foot whith less than 2k viewers on live stream🤣🤣🤣
 
Katika kujaza viwanja mji huu wa dar sijui kama itatokea ujazo wa cuf ya lipumba og,sasahivi hata yeye lipumba robo ya ile yazamani hawezi fikisha
 
Kimkakati Uongozi wa CDM ulishafeli ,labda tuone leo! Ila ki ukweli upinzani bado sana na haupo makini na uchaguzi! Matokeo watakayo yapata oktoba wasimtafute mchawi nani!. Sisi tutaendelea kuwapa ukweli tu , japo mchungu kwao!.
Shule lazima tuwape ndugu wetu hawa
 
Katika kujaza viwanja mji huu wa dar sijui kama itatokea ujazo wa cuf ya lipumba og,sasahivi hata yeye lipumba robo ya ile yazamani hawezi fikisha
Game liko taiti mno safari hii
 
Assessment yangu ya haraka kwa mkutano wa Jana ni kuwa Chadema hawana fedha za kuendesha kampeni ya viwango.

Dunia nzima unahitaji fedha kufanya kampeni za viwango.

Kila kitu kilikuwa duni, na ndio hapo utaona namna fedha za Lowasa zilivyoipa nguvu Chadema kwa wakati ule.
Uko sahihi mkuu, sasa zile pesa walikuwa wanakatana zilikuwa za nini sasa?
 
Acha kukariri,Sasa hivi watu wanafatilia michakato mtandanoni,ni ccm imebaki kusafirisha watu toka mbali kujaza uwanja.
Kama mnajiamini achilieni tume iwe huru muone.
Nimeona viewers elfu 10, ukichanganya na wale 100(pengine hawakutimia) tunapata kura 10100

Kuna chama cha upinzani wanaamini wataingia ikulu kwa kura hizo
 
CDM kwakweli ukiwasikiliza humu ndani ya jamvi unaweza ona wapo serious, ukiangalia mlolongo mziwa wa jana kwakweli umenifikirisha hivi hawa ni watu ambao wapo serious na wanachokifanya, hii ni sawa na kuonja sumu na kujiaminisha ni asali, hata body language ya mboye haikuwa sawa, jukwaa lenyewe ni kama la kigodoro poor CDM.
Completely poor organized campaign plan
 
Back
Top Bottom