Ndugu Watanzania wenzangu,
Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kutupa uzima na kuiona siku hii ya leo.
Kwa kifupi sana, naamini jana wote tulijionea hali halisi ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA, na hii imetudhihirisha kuwa mzee Lowassa ilikuwa namba nyingine kabisa, na hatakuja kutokea mtu mwingine wa mvuto wa kisiasa kama mzee yule katika chaguzi za hivi karibuni. Katika nyuzi zangu, niliwahi kudokeza kuwa Mh. Tundu Lissu hawezi kufikia hata nusu ya mzee Lowassa, yule mzee alikuwa si mtu wa kawaida.
Aidha, kwa mliokuwa mkifuatilia kampeni za 2015, uzinduzi wa kampeni za UKAWA pale Jangwani, naamini ulipeleka taharuki kubwa sana kwa CMM, lakini kwa nilichokiona jana, basi nadiriki kusema kuwa, uzinduzi huu umepeleka taarifa ya ushindi mkubwa sana kwa CCM na kuwaona CHADEMA safari hii mko DHAIFU MNO AND POORLY ORGANIZED.
Kosa kubwa kwa CHADEMA jana, wamekosa kuchukulia ile siku ya jana kuwa very seriously, huku wakishindwa kujua kuwa NYUMBA IMARA INATOKANA NA MSINGI IMARA, THAT IS, FIRST IMPRESSION MATTER A LOT. Kwa maoni yangu, nadhani uzi wa Salary slip uliokuwa unawashauri wasinzindue kampeni badala yake wafuatilie suala la wagombea wao walioenguliwa, nadhani hii ndiyo boko ya kwanza kutoa. Kama kungekuwa na think tanks wa kueleweka wangefanya mambo yafuatayo ili kunusuru siku ya kuzindua kampeni kwa kufanaya jambo jingine kabisa, ambayo ni kinyume na matarajio ya watanzania wengi:
Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu

- Uongozi wa cdm ungeita wanahabari asubuhi na mapema kuongelea suala hilo la kuenguliwa kwa wagombea wao
- Press hii ingeambatana na uongozi wote wa cdm na baadhi ya wabunge mashuhuri wa CDM ili kuonyesha wako serious na hii kitu
- Uzinduzi wa ilani ulikuwa unatakiwa ufanyike siku ya jana hiyo hiyo na siyo kusubiri siku nyingine tena.
- Kuna uwezekano mkubwa CDM kampeni plan yao inakosa mathink tanks kama ilivyokuwa 2015, ambayo ilikuwa na akina Kingunge, Sumaye, Lowasa, etc.
- Kuna uwezekano ndani ya CDM kulikuwa na kutoelewana nini kifanyike katika siku ya jana
- Uzi wa Salary Slip ulicompromise siku ya jana
Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu