Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Binafsi katika marekebisho ya katiba ninayoyaona, baada ya kufariki Rais aliyeko madarakani, makamu wa Rais, awe kaimu Rais ndani ya muda utakaopendekezwa Ili baada ya hapo uchaguzi mpya wa Rais ufanyike.
huku ni kuhamisha magoli. hakuna hata mmoja aliyewahi kupendekeza hili mpaka la kutokea limetokea. yani ni kama vile hakukuwa na watu wenye vichwa vya kufikiria hilo kwa sababu yoyote. wote waliokuwepo pamoja na mleta mada walichukulia kuwa hakuna haja ya kujiangaisha na mgombea mwenza ambaye potentially angeweza kuja kuwa rais. mama ndie rahisi na inawafaa wenye akili kuanza kuishi na hilo. the least would be to give her the benefit of doubt. things are as should be.
Maana ukweli wenyewe ukisemwa, watu huwa hawamchagui makamu wa Rais katika uchaguzi.
Uhalisia unaonyesha kwamba makamu wa Rais huwa tu amabebwa na mgombea urais.
Toka lini umegundua hili. mnachokwenda kuishi nacho kwa uchungu mkubwa ni kuwa huyu mama atakuwa ndie rais wa JMT mpaka 2030, hapo asipoamua kutamani yale mambo ya 'tutamlazimisha akubali'
hakuna mahali paliposema makamu wa rais ni second selection. haya unayatunga wewe. mgombea mwenza huteuliwa na rais mtarajiwa kwa sababu anazoona zinafaa ambazo pia ni uwezo wa kuongoza nchi au vinginevyo. rais mtarajiwa humteua mgombea mwenza akiwa na full awareness kuwa anaweza kufa kabla ya kuondoka madarakani na huyo mgombea mwenza ndie atakayekuwa rais. kujaribu kuaminisha watu kuwa mama hana uwezo kutakutokea puani. utaishi na hilo mpaka 2030
mama ndie rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. huo muswada wa mabadiliko ya katiba lazima upite kwenye meza yake kabla haujaenda kokote. wako watu kibao wa kuwakokota wakamsaidia kuendesha nchi na chochote kisitokee.
 
Katiba mpya haitamuondoa mama samia. Labda kwa maraisi wajao. Kwa ss kunaliana na hali.
 
Kunaweza wekwa hata utaratibu mwingine wa bunge kuprndekeza jina la mrithi anaweza malizia miaka iliyosalia!
Lakini hiyo ya automatic kuwa makamu awe rais ni hatari mno
Nakuunga mkono, chombo cha kutunga sheria kwa maana ya bunge ndiyo lipitishe majina na wampendekeze mmoja atakae mrithi punde ikitokea amefariki, ipo sawa kabisa, mambo ya kuchukua makamu kuwa Rais ni utata
 
Kwamba una wasiwasi na SAMIA si ndio! Kwamba humuamini SAMIA si ndio!
Kwahiyo ulikua na VP ambae huamini katika uwezo wake wa kuongoza si ndio!




URAIS ni taasisi ... Nahisi kuna watu wana chuki tu na huyu Mama
Sijamuelewa kabisa huyu jamaa hoja yake
 
Lowasa aliitwa kibabu na mgonjwa na kwamba atafia Ikulu (by Nape and Co Ltd)... But now??
 
Hii ni lesson kubwa sana kwa wahusika. Next time pick ya VP iwe inafanyika kwa umakini mkubwa mno bila mihemuko maana huyu ni Rais in waiting.

Imagine sasa hivi. Tuna mama mpaka 2025, potentially mpaka 2030.
Tatizo pool ya kuchagua huyo VP ni ndogo sana..Lazima awe Mzanzibari
 
Kwani hawezi kumuua kisha anakaimu na kupanga mipango kiafrika na kushinda uchaguzi na kuwa raisi wa kuchaguliwa mifano mingi tunayo mtu anakaimu kisha anashinda uchaguzi.
 
Ulitaka rais akifariki mwingine apatikane vipi? Kwa uchaguzi mwingine wa rais?

Unajua maandalizi ya uchaguz wa rais na gharama zake?
 
Hawezi kuwa Mzanzibar. Haiwezekani Rais na VP wote wakawa Wazanzibar.
Kikawaida Rais wa TZ huwa anatokea bara, japo kutokea Zanzibar pia inawezekana lakini bara ndipo kwenye watu wengi na viongozi wengi wenye ushawishi na experience ya kuwa president. Hii inafanya mara nyingi VP kutokea Zanzibar ambako kuna watu wachache na wanasiasa wachache pia wenye uwezo na ushawishi
 
Mi
Ni kweli,makamu siku zote anaweza kuwa anamuombea mabaya bosi wake ili na yeye akwee.
 
Mbona magu na Majaliwa wote wanatoka bara?

Kuwa wote wazenji shida ni nini?
 
Binge la jobo lililokua ambapo jobo aliahidi kumlazimisha mtu kutawala maisha yote. Jobo imesambaratika
 
Ulitaka rais akifariki mwingine apatikane vipi? Kwa uchaguzi mwingine wa rais?

Unajua maandalizi ya uchaguz wa rais na gharama zake?
Unajua gharama za kuwa na Rais kimeo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…