Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Binafsi katika marekebisho ya katiba ninayoyaona, baada ya kufariki Rais aliyeko madarakani, makamu wa Rais, awe kaimu Rais ndani ya muda utakaopendekezwa Ili baada ya hapo uchaguzi mpya wa Rais ufanyike.
huku ni kuhamisha magoli. hakuna hata mmoja aliyewahi kupendekeza hili mpaka la kutokea limetokea. yani ni kama vile hakukuwa na watu wenye vichwa vya kufikiria hilo kwa sababu yoyote. wote waliokuwepo pamoja na mleta mada walichukulia kuwa hakuna haja ya kujiangaisha na mgombea mwenza ambaye potentially angeweza kuja kuwa rais. mama ndie rahisi na inawafaa wenye akili kuanza kuishi na hilo. the least would be to give her the benefit of doubt. things are as should be.
Maana ukweli wenyewe ukisemwa, watu huwa hawamchagui makamu wa Rais katika uchaguzi.
Uhalisia unaonyesha kwamba makamu wa Rais huwa tu amabebwa na mgombea urais.
Toka lini umegundua hili. mnachokwenda kuishi nacho kwa uchungu mkubwa ni kuwa huyu mama atakuwa ndie rais wa JMT mpaka 2030, hapo asipoamua kutamani yale mambo ya 'tutamlazimisha akubali'
Lakini Jambo jingine ni uwezo. Tunaweza tisilione hili,lakini ukweli ni kwamba second selection mahali popote ina percentage za upungufu ktk Jambo lolote. Hivyo kumuacha awe Rais moja kwa moja kuna hatari ya kuwa na mtu asiye na uwezo wa kuongoza maana nafasi aliyokuwa nayo kama mgombea mwenza kwa wengi huwa ni ya dhuru nini maana wao nguvu kubwa huwekeza kwa mgombea Urais.
hakuna mahali paliposema makamu wa rais ni second selection. haya unayatunga wewe. mgombea mwenza huteuliwa na rais mtarajiwa kwa sababu anazoona zinafaa ambazo pia ni uwezo wa kuongoza nchi au vinginevyo. rais mtarajiwa humteua mgombea mwenza akiwa na full awareness kuwa anaweza kufa kabla ya kuondoka madarakani na huyo mgombea mwenza ndie atakayekuwa rais. kujaribu kuaminisha watu kuwa mama hana uwezo kutakutokea puani. utaishi na hilo mpaka 2030
Lakini hatari kubwa ni huyu mrithi kukosa kile kinachoitwa power of legitimacy. Najua makamu huchagiliwa kwa tiketi moja na Rais, lakini kama nilivyosema hapo juu, watu humchagua Rais hasa na makamu huwa ni suala la " pitisha tu".
Let us think on this.
mama ndie rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. huo muswada wa mabadiliko ya katiba lazima upite kwenye meza yake kabla haujaenda kokote. wako watu kibao wa kuwakokota wakamsaidia kuendesha nchi na chochote kisitokee.
 
Katiba mpya haitamuondoa mama samia. Labda kwa maraisi wajao. Kwa ss kunaliana na hali.
 
Kunaweza wekwa hata utaratibu mwingine wa bunge kuprndekeza jina la mrithi anaweza malizia miaka iliyosalia!
Lakini hiyo ya automatic kuwa makamu awe rais ni hatari mno
Nakuunga mkono, chombo cha kutunga sheria kwa maana ya bunge ndiyo lipitishe majina na wampendekeze mmoja atakae mrithi punde ikitokea amefariki, ipo sawa kabisa, mambo ya kuchukua makamu kuwa Rais ni utata
 
Kwamba una wasiwasi na SAMIA si ndio! Kwamba humuamini SAMIA si ndio!
Kwahiyo ulikua na VP ambae huamini katika uwezo wake wa kuongoza si ndio!




URAIS ni taasisi ... Nahisi kuna watu wana chuki tu na huyu Mama
Sijamuelewa kabisa huyu jamaa hoja yake
 
Kuna baadhi ya nchi hufanya hivyo. Ndani ya siku 90, uchaguzi wa Rais unafanyika tena. Ila kwa bahati mbaya nadhani sisi tumechukua mfumo wa nchi kama Marekani!

Kile kibabu Joe Biden kikatokea ghafla kikaanguka, na kwenyewe kutatokea tukio la kihistoria kwa Makamu wa Kwanza kabisa Mwanamama Camara Harris kukabidhiwa Nchi ya Kibeberu kuitawala
Lowasa aliitwa kibabu na mgonjwa na kwamba atafia Ikulu (by Nape and Co Ltd)... But now??
 
Hii ni lesson kubwa sana kwa wahusika. Next time pick ya VP iwe inafanyika kwa umakini mkubwa mno bila mihemuko maana huyu ni Rais in waiting.

Imagine sasa hivi. Tuna mama mpaka 2025, potentially mpaka 2030.
Tatizo pool ya kuchagua huyo VP ni ndogo sana..Lazima awe Mzanzibari
 
Ndugu watanzania napendekeza kipengele cha katiba ya Tanzania kinachompa Makamu wa Rais nafasi ya kurithi kiti cha Urais moja kwa moja kama ilivyotokea kwa Suluhu kibadilishwe haraka.

kwa sababu kipengele hicho kinahatarisha usalama wa Rais Makamu wa Rais anaweza kushawshika kumdhuru Rais ili yeye arithi nafasi hiyo. Kkundi cha watu wenye nia ovu na tamaa wanaweza kutumia mwanya huo ili kumuweka mtu wao.

Hivyo napendekeza kuwa mara baada ya kiti cha Urais kuwa wazi kwa sababu ya Kifo, maradhi au kuondolewa kwa sababu nyingine. Makamu wa Rais awe Rais wa mpito kwa muda na kuwe na uchaguzi mwingine hata kama nigharam
Kwani hawezi kumuua kisha anakaimu na kupanga mipango kiafrika na kushinda uchaguzi na kuwa raisi wa kuchaguliwa mifano mingi tunayo mtu anakaimu kisha anashinda uchaguzi.
 
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.

Katiba ni uhai.

Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.

Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.

Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.
Ulitaka rais akifariki mwingine apatikane vipi? Kwa uchaguzi mwingine wa rais?

Unajua maandalizi ya uchaguz wa rais na gharama zake?
 
Hawezi kuwa Mzanzibar. Haiwezekani Rais na VP wote wakawa Wazanzibar.
Kikawaida Rais wa TZ huwa anatokea bara, japo kutokea Zanzibar pia inawezekana lakini bara ndipo kwenye watu wengi na viongozi wengi wenye ushawishi na experience ya kuwa president. Hii inafanya mara nyingi VP kutokea Zanzibar ambako kuna watu wachache na wanasiasa wachache pia wenye uwezo na ushawishi
 
Mi
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.

Katiba ni uhai.

Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.

Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.

Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa
Ni kweli,makamu siku zote anaweza kuwa anamuombea mabaya bosi wake ili na yeye akwee.
 
Mimi naona kuna kitu Katiba imeachia hasa ikizingatiwa kuna Bara na Visiwani. Haipendezi Bara na Visiwani kuongozwa na Wanzazibar. Ingesema ikiwa VP ni Mzazibar endapo Rais atakufa /kujiuzulu apatikane VP toka Bara. Angeweza kuchaguliwa miongoni mwa Viongozi waandamizi Serikali I wanalijua Tz Bara nje na ndani.
Mbona magu na Majaliwa wote wanatoka bara?

Kuwa wote wazenji shida ni nini?
 
Binge la jobo lililokua ambapo jobo aliahidi kumlazimisha mtu kutawala maisha yote. Jobo imesambaratika
 
Ulitaka rais akifariki mwingine apatikane vipi? Kwa uchaguzi mwingine wa rais?

Unajua maandalizi ya uchaguz wa rais na gharama zake?
Unajua gharama za kuwa na Rais kimeo?
 
Back
Top Bottom