Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha mfumo Dume.Upo sahihi kabsa ...lkn kuongozwa na mwanamke nalo pia n tatzo automatically
50/50Upo sahihi kabsa ...lkn kuongozwa na mwanamke nalo pia n tatzo automatically
Je pia ndio atakuwa mwenyekiti wa chama?Katiba mpya ilitakiwa iwe imepatikana, ila rais huyu marehemu yeye na kundi lake akiwemo huyu mama makamo wa rais ndio waliihujumu.
Rais Magufuli yeye alivuka mipaka mpaka kusema katiba mpya sio ajenda yake akiamini yeye ndio nchi, na katiba ni suala la utashi wake! Acha aongoze huyu mama mwenye uwezo mdogo, ili kila mtu ajue katiba ni zaidi ya madaraka ya urais yanayotumika vibaya.
je pia ndio atakuwa mwenyekiti wa chama?
Ainisha/taja hizo hatari p'se.Kunaweza wekwa hata utaratibu mwingine wa bunge kuprndekeza jina la mrithi anaweza malizia miaka iliyosalia!
Lakini hiyo ya automatic kuwa makamu awe rais ni hatari mno
Hatari kivipi? Funguka...Kusema nchi iingie kwenye uchaguzi ASAP baada ya kifo cha raisi ndo hatari zaidi.
[emoji23] [emoji23] Unaweza kukuta hana hata habari kwamba kuna rasimu ya katiba ya jaji Warioba...Maoni yapo tayali, na samia alikuwa mjumbe wa bunge la katiba! Hakuna kinachoshindikana
Naunga mkono hoja. Ni kama ukiandika wosia halafu ukawa umemwachia mali zote mkeo halafu akauona wosia wenyewe.........Katiba mpya ni suluhisho la mambo mengi, akipatikana wa kuimalizia atajenga msingi mzuri sana kwa Nchi hii.Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.
Katiba ni uhai.
Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.
Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.
Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)
Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.
Kwamba una wasiwasi na SAMIA si ndio! Kwamba humuamini SAMIA si ndio!
Kwahiyo ulikua na VP ambae huamini katika uwezo wake wa kuongoza si ndio!
URAIS ni taasisi ... Nahisi kuna watu wana chuki tu na huyu Mama
Kabisa mkuuNaunga mkono hoja. Ni kama ukiandika wosia halafu ukawa umemwachia mali zote mkeo halafu akauona wosia wenyewe.........Katiba mpya ni suluhisho la mambo mengi, akipatikana wa kuimalizia atajenga msingi mzuri sana kwa Nchi hii.
Good ideaSuala la mabadiliko ya katiba limesemwa Sana na nadhani wajuvi wa sheria na katiba wanaweza kueleza sana maana huu ndo uga wao.
Binafsi katika marekebisho ya katiba ninayoyaona, baada ya kufariki Rais aliyeko madarakani, makamu wa Rais, awe kaimu Rais ndani ya muda utakaopendekezwa Ili baada ya hapo uchaguzi mpya wa Rais ufanyike.
Nchi nyingine kwa mfano Kaimu Rais ambaye obvious anakuwa ni makamu wa Rais anaweza kukaimu kwa muda wa miezi mitatu na wengine sita Ili kupisha uchaguzi mpya wa Rais.
Kuna mantic hapo. Maana ukweli wenyewe ukisemwa, watu huwa hawamchagui makamu wa Rais katika uchaguzi.
Uhalisia unaonyesha kwamba makamu wa Rais huwa tu amabebwa na mgombea urais. Hata sababu za kimantic zinaonyesha, ndo maana huitwa mgombea mwenza. Huyu huwa ni chaguo la pili kwa umaarufu kwa hiyo kumfanya awe Rais moja kwa moja huondoa imani kwa wananchi, niseme wengi kwa sababu huwa anaonekana ni second selection.
Lakini Jambo jingine ni uwezo. Tunaweza tisilione hili,lakini ukweli ni kwamba second selection mahali popote ina percentage za upungufu ktk Jambo lolote. Hivyo kumuacha awe Rais moja kwa moja kuna hatari ya kuwa na mtu asiye na uwezo wa kuongoza maana nafasi aliyokuwa nayo kama mgombea mwenza kwa wengi huwa ni ya dhuru nini maana wao nguvu kubwa huwekeza kwa mgombea Urais.
Hivyo napendekeza mabadiliko ya katiba Ili baada ya Rais kufa au kushindwa kufanya kazi zake kea sababu nyingine yoyote, makamu asiwe Rais moja kwa moja bali kuwa na uchaguzi mwingine wa kumchagua Rais.
Lakini hatari kubwa ni huyu mrithi kukosa kile kinachoitwa power of legitimacy. Najua makamu huchagiliwa kwa tiketi moja na Rais, lakini kama nilivyosema hapo juu, watu humchagua Rais hasa na makamu huwa ni suala la " pitisha tu".
Let us think on this.