Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Katiba mpya ilitakiwa iwe imepatikana, ila rais huyu marehemu yeye na kundi lake akiwemo huyu mama makamo wa rais ndio waliihujumu.

Rais Magufuli yeye alivuka mipaka mpaka kusema katiba mpya sio ajenda yake akiamini yeye ndio nchi, na katiba ni suala la utashi wake! Acha aongoze huyu mama mwenye uwezo mdogo, ili kila mtu ajue katiba ni zaidi ya madaraka ya urais yanayotumika vibaya.
Je pia ndio atakuwa mwenyekiti wa chama?
 
Hoja ni nini? Ni udhaifu wa mwenza? au ni kuhisi hatoweza kuwa na imani kwa wananchi kwakuwa hawakumchagua kuwa rais moja kwa moja? Jibu la maswali yote hayo ni TUJIFUNZE KUPITIA HILI!
 
Kunaweza wekwa hata utaratibu mwingine wa bunge kuprndekeza jina la mrithi anaweza malizia miaka iliyosalia!
Lakini hiyo ya automatic kuwa makamu awe rais ni hatari mno
Ainisha/taja hizo hatari p'se.
 
Watu hatumuamini hatuna imani naye kwenye kiti cha urais. Ataweza pambana na mafisadi??
 
Maoni yapo tayali, na samia alikuwa mjumbe wa bunge la katiba! Hakuna kinachoshindikana
[emoji23] [emoji23] Unaweza kukuta hana hata habari kwamba kuna rasimu ya katiba ya jaji Warioba...
 
Wasiwasi wako nimzuri sana.hata Mimi hofu yangu unaweza kuta ndani yamwaka tena tunamwapisha makamu mwingine.
 
Suala la katiba lipewe kipaumbele sana.

Katiba ni uhai.

Yapo mengi ya hatari sana kwenye katiba hii.

Lakini hili la Mrithi wa rais anayefariki dunia, kuwa ni makamu wa rais (automated) ni hatari sana kwa marais endapo tukipata Makamu asiyemwaminifu.

Pia linachangia sana kumuweka mbali makamu wa rais kuwa karibu na rais kwa hofu ya kutoaminia! (Naturally internal conflict)

Kwa gharama yoyote naomba tuanze na katiba inafaida kwetu sote matajiri na masikini, viongozi na watawaliwa.
Naunga mkono hoja. Ni kama ukiandika wosia halafu ukawa umemwachia mali zote mkeo halafu akauona wosia wenyewe.........Katiba mpya ni suluhisho la mambo mengi, akipatikana wa kuimalizia atajenga msingi mzuri sana kwa Nchi hii.
 
Naunga mkono hoja. Ni kama ukiandika wosia halafu ukawa umemwachia mali zote mkeo halafu akauona wosia wenyewe.........Katiba mpya ni suluhisho la mambo mengi, akipatikana wa kuimalizia atajenga msingi mzuri sana kwa Nchi hii.
Kabisa mkuu
 
Suala la mabadiliko ya katiba limesemwa Sana na nadhani wajuvi wa sheria na katiba wanaweza kueleza sana maana huu ndo uga wao.

Binafsi katika marekebisho ya katiba ninayoyaona, baada ya kufariki Rais aliyeko madarakani, makamu wa Rais, awe kaimu Rais ndani ya muda utakaopendekezwa Ili baada ya hapo uchaguzi mpya wa Rais ufanyike.

Nchi nyingine kwa mfano Kaimu Rais ambaye obvious anakuwa ni makamu wa Rais anaweza kukaimu kwa muda wa miezi mitatu na wengine sita Ili kupisha uchaguzi mpya wa Rais.

Kuna mantic hapo. Maana ukweli wenyewe ukisemwa, watu huwa hawamchagui makamu wa Rais katika uchaguzi.
Uhalisia unaonyesha kwamba makamu wa Rais huwa tu amabebwa na mgombea urais. Hata sababu za kimantic zinaonyesha, ndo maana huitwa mgombea mwenza. Huyu huwa ni chaguo la pili kwa umaarufu kwa hiyo kumfanya awe Rais moja kwa moja huondoa imani kwa wananchi, niseme wengi kwa sababu huwa anaonekana ni second selection.

Lakini Jambo jingine ni uwezo. Tunaweza tisilione hili,lakini ukweli ni kwamba second selection mahali popote ina percentage za upungufu ktk Jambo lolote. Hivyo kumuacha awe Rais moja kwa moja kuna hatari ya kuwa na mtu asiye na uwezo wa kuongoza maana nafasi aliyokuwa nayo kama mgombea mwenza kwa wengi huwa ni ya dhuru nini maana wao nguvu kubwa huwekeza kwa mgombea Urais.

Hivyo napendekeza mabadiliko ya katiba Ili baada ya Rais kufa au kushindwa kufanya kazi zake kea sababu nyingine yoyote, makamu asiwe Rais moja kwa moja bali kuwa na uchaguzi mwingine wa kumchagua Rais.

Lakini hatari kubwa ni huyu mrithi kukosa kile kinachoitwa power of legitimacy. Najua makamu huchagiliwa kwa tiketi moja na Rais, lakini kama nilivyosema hapo juu, watu humchagua Rais hasa na makamu huwa ni suala la " pitisha tu".
Let us think on this.
Good idea
 
Lyndon Johnson ndiye rais wa Marekani wa mwisho kukalia kiti awamu ya 36 toka mwaka 1963 baada ya kuwa makamu wa rais. Je, nini kilifanyika mpaka leo, hakuna "died in office", tukajifunze?
 
Back
Top Bottom