Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Ndugu watanzania napendekeza kipengele cha katiba ya Tanzania kinachompa Makamu wa Rais nafasi ya kurithi kiti cha Urais moja kwa moja kama ilivyotokea kwa Suluhu kibadilishwe haraka.

kwa sababu kipengele hicho kinahatarisha usalama wa Rais Makamu wa Rais anaweza kushawshika kumdhuru Rais ili yeye arithi nafasi hiyo. Kkundi cha watu wenye nia ovu na tamaa wanaweza kutumia mwanya huo ili kumuweka mtu wao.

Hivyo napendekeza kuwa mara baada ya kiti cha Urais kuwa wazi kwa sababu ya Kifo, maradhi au kuondolewa kwa sababu nyingine. Makamu wa Rais awe Rais wa mpito kwa muda na kuwe na uchaguzi mwingine hata kama ni gharama.
Miaka 60 ya uhuru hakijaleta madhara, leo kibadirishwe? Walioweka wanaakili nadhani tungekuwa tunaenda kwenye uchaguzi tena ndiyo ingekuwa changamoto sana nchi ingekuwa inapitia kipindi kigumu zaidi........sema vyama vya siasa visiweke wagombea wenza kutimiza wajibu tu,wawe serious kwenye selection ya candidates wao.

Tumwache mama kwasasa
 
Hata mtu aliye nje ya mfumo wa utawala anaweza kumdhuru Rais aliye madarakani ama kwa nia ya moja kwa moja au kupitia wasaidizi wa Rais.

Nia yako ni kwamba pindi nafasi ya Urais inapokuwa wazi kwa sababu zozote ikiwemo kifo unataka uchaguzi mpya uitishwe.

Sio kweli kwamba hilo wazo lako halikuwemo kwenye moja ya uwezekano wa kuwekwa kwenye katiba lakini hatimaye kifungu kilicho salama zaidi ndicho kilichowekwa kuepusha mambo mengi oambayo yangesababisha matumizi ya gharama, vurugu, kukosa utulivu.

Sijui umewaza nini mpaka kufuikia hatua ya kutoa pendekezo hilo finye ambalo halijafikiria hasara na faida kisha ukaziweka kwenye mizania.

Wanasiasa ndio mnamatamanio ya kutaka uchaguzi ufanyike ili mpate manufaa yenu binafsi na sio wananchi. Una wasiwasi gani makamu wa Rais kuchukua nafasi hiyo ya juu kabisa ya utawala wa nchi?
Ndio hivyo yaani wanasiasai wao wanawazaga madaraka tu amna lingine lengo Leo ili kutengenez vuta ni kuvuta mara utasikia maridhiano ya kitaifa mara kuliunganisha taifa ili mradi wao wawemo katika point flani
 
Kwamba una wasiwasi na SAMIA si ndio! Kwamba humuamini SAMIA si ndio!
Kwahiyo ulikua na VP ambae huamini katika uwezo wake wa kuongoza si ndio!




URAIS ni taasisi ... Nahisi kuna watu wana chuki tu na huyu Mama
Tena Bora ibaki hivihivi
Huyu mama mungu kamshushia cheo tuheshimu Hilo
Ni Bora kuwa na Samia kuliko akina ndugai
 
Kunaweza wekwa hata utaratibu mwingine wa bunge kuprndekeza jina la mrithi anaweza malizia miaka iliyosalia!
Lakini hiyo ya automatic kuwa makamu awe rais ni hatari mno
Kila kitu kina faida na hasara, huko unakovutia kwenyewe kuna hasara zake.
 
Shida ni nature ya wabunge waliopo mule ndani, woooote ni kwa hisani ya mzee so wenye maono na maslahi kwa nchi ni wachache sana mle ndani.
Kwani mzee unakusudia katiba Mpya au ile tulioipitisha wenyewe CCM? Kama ni katiba mpya tunamaanisha mchakato mpya na Bunge jipya la katiba ile hatuitambui
 
Kwani kwa mujibu wa rasimu ya warioba endapo Rais angefariki si hayahaya yangetokea au ni kujitoa ufahamu tu
 
Nafsi yangu inaniambia samia hatamaliza muda wake salama. Na kila nikichungulia Twitter nazidi kuogopa
Endelea kuchungulia na kupiga ramli ila mama anamaliza mitano.


We endelea kupiga ramli.
 
Katiba mpya iwe kwa kila kitu sio kurithishana madaraka tu.
Kwani kwa mujibu wa rasimu ya warioba endapo Rais angefariki si hayahaya yangetokea au ni kujitoa ufahamu tu
 
Waanze na sura ya kwanza hadi 6 kisha waipitie na hiyo 37 (5)
 
Ujue hiyo 37 (5) haijatumika toka Tanganyika ianze. Wahuni wameshaiona, wataitumia kabla miaka mitano haiajapita.
 
Back
Top Bottom