IKULU CHAMWINO: Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu ya CCM Tanzania

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466
===
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Leo tarehe 12 Novemba 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Mama wa Taifa na Jasiri mwongoza njia Ndg Samia Suluhu Hassan akiwa kazini Leo, katika CC ya CCM-tanzania,


Wajumbe makini wa CC ya CCM -tanzania wakiendelea na Kikao Ikulu Leo,bila hawa kuwa makini nchi itayumba,


Katibu Mkuu wa ccm-tanzania Ndg Daniel Chongolo akiteta jambo na Mkt Wake Ndg Samia Suluhu Hassan Ikulu, Chamwino,

Makamu Mkt wa ccm-tanzania Ndg Abdurahman KINANA ambaae pia ndie Mkt wa Maadili akipitia makabrasha katika taarifa ya Katibu Mkuu Ndg Daniel Chongolo,


Katibu wa NEC Itikadi &Uenezi wa ccm-taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akifuatilia kwaumakini kikao cha CC na ndiye atakayetujuza nini kitajiri katika Vikao hivi,

#Stay tuned, nadhani mmeona makabrasha hapo juu,Kazi inaendeleaje
 
Hapa hawezi kutoka na independent decision! Aliweza Nyerere tu basi. hapa lazima wamburuze! Aseme hiki sitaki, never on earth!
 
Melekezo kutoka mgaso lazima wayafanyie kazi...hakuna jipya hapo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hairuhusiwi mkutano wa chama kufanyika kwenye jengo la serikali!!
 
Kwa nini kikao cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu ya CCM Tanzania kinafanyikia Ikulu ?

Je chadema nao wakiwa na kikao cha kamati kuu ya Halmashauri kuu wanaruhusiwa kufanyoa kikao Ikulu?
Je Ikulu ni mali ya nani? Nimeuliza tu.
 
Ikulu ni mali ya Watanzania waliomchagua Rais aliyeko madarakani pamoja na chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…