Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Dar Es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anapokea taarifa ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa leo tarehe 21 Machi 2022.
Pia soma > Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025
Baadhi ya NUKUU za Rais Samia
Kikosi kazi mmejihalalishia kuwa na kazi karibu miaka 9 yote iliyobaki na mimi hapa, na huku ndio kunaitwa kujiajiri wenyewe. Lengo letu ni kuwa na siasa zenye tija
Vyama vya siasa na vyombo vya habari tuwe na uhusiano mzuri, nanyi vyombo vya habari msiwe na maslahi na upande wowote, mnatakiwa kuwa kati kati"
Nitaendelea kukutana na vyama vya siasa kuwasikiliza wanataka maboresho yapi, lengo wote twende kwenye reli moja katika kufanya siasa zenye tija kwa nchi yetu"
Katika suala la kanuni za mikutano ya hadhara, sio tu kwamba ziwepo ili mikutano ianze, lakini pia kanuni zianishe atakayekiuka atafanywaje
Watu wetu hawana uelewa wa mambo ya siasa, uzalendo wala elimu ya uraia, watu wangekuwa na elimu ya uraia, uzalendo na elimu ya dunia, mauaji tunayoyashuhudia hii leo yasingekuwepo. Yote hayo hawana, ndio maana wanajifanyia tu
Tukisema tutatoa ruzuku kwa kila chama cha siasa, fedha hizo tutazitoa wapi, lakini tukikubali hilo tutakuwa kama nchi fulani kwamba kila baada ya siku 3 chama kipya cha siasa kinaundwa
Tujiulize kwa hicho tunachokitaka kwamba Tume Huru, tujifunze kwa majirani zetu, je pamoja na kuwa na hizo zinazoitwa Tume Huru hakuna migogoro? Hawatangazi matokeo na kukimbia nchi? Maana halisi ya tume huru ni hasa
Wanawake tusililie tu nafasi za uongozi, lakini tujue pia wajibu wetu kama wanawake,lolote linalotokea katika nchi sisi ndio wa kwanza tunaoumia pamoja na watoto wetu. Kuingiza wanawake katika uongozi wa siasa ni muhimu kwa kuwa sisi tuna ajenda za kuzisimamia
Nitawapa mfano katika mkoa ninaotoka, kuna mwanamke mmoja alipambana akaingia katika nafasi za uongozi, alipoingia tu alisema afadhali na mimi nitapata kununua madhahabu nijipambe, ina maana analoendea huko hakuna. Hii ni historia ya kweli
Uadilifu unaweza kurudi kwa ukali kwamba unakuwa mkali, Ukifanya hivi nitakutoa, hiyo ni nidhamu ya uoga. Tunataka uadilifu ujengwe katika mioyo na sio nidhamu ya uoga, kwamba mimi nafanya hili nisipofanya kuna mtu atakwenda kunichongea
#KaziIendelee
#TunaImaniNaSamia
---

- "PCCB (TAKUKURU) hawafanyi kazi vizuri ni kweli; tusiposema hatujengi nyumba nzuri; tutakaposema tutarekebisha na tutajenga nyumba nzuri."
- "Unaposema kila chama cha siasa kitapewa ruzuku tutakuwa kama Lesotho, kila baada ya siku mbili chama cha siasa kimeundwa watu wanataka ruzuku...hiyo haitawezekana...Unapounda chama cha siasa, umejipimaje? Utajiendeshaje?"
- "Uadilifu umepungua ni kweli; tufanyaje sasa? Ni elimu ya uraia, uzalendo ili kila mmoja alipo ajue anafanya nini ndiyo uadilifu utarudi katika hatua yake."
- "Uadilifu unaweza ukarudi kwa ukali lakini tunasema ni nidhamu ya woga. Tunataka uadilifu ujengwe kwenye mioyo na sio nidhamu ya woga."
- “Maboresho ya sheria na kanuni za uchaguzi, sawa mtatuambia vipengele gani vinauma, tutajadili kwa pamoja tuone pengine inawezekana tukifanya maboresho huku na mengine yote yatakayofanywa huko pengine lile kelele la Katiba likaishia kwa sababu zile kiu za watu wanapotaka Katiba ibadilishwe zilishafanyiwa kazi huku.”
- “Suala la rushwa ni jukumu letu wote, twendeni tukalifanyieni kazi, chaguzi zetu ziende vizuri. Sijui kama tunaweza kufanya 100% lakini tukianza kupunguza ndio tunaelekea huko, vinginevyo wasio kitu hawataingia kwenye nafasi zozote zile.”
- "Kuingiza wanawake ndani ya vyama vya siasa ni muhimu sana kwa sababu sisi ndiyo tuna ajenda ya kusimamia."
- "Kuna kazi kubwa kweli kufanya wanawake wasimame vizuri kwenye vyama vya siasa. Tusililie tu nafasi za kuingia, tujue na wajibu wetu pia tunapoingia kama wanawake."
- "Tuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye hili taifa kwa faida yetu (wanawake) na taifa letu kwa ujumla lakini kila siku mashaka yapo palepale."
- “Izo ‘codes of conduct’ za vyama vya siasa zisiwe za kukandamiza na vizuri mtakua wenyewe mnazitunga, zisikandamize, zisiue vyama vya siasa lakini zilete siasa zenye tija ndani ya nchi, isiwe kila siku tuko kwenye maBBC na CNN huko kila siku ukifungua BBC, CNN Tanzania imefanya hivi, sio ustaarabu kwa kweli, twende na siasa zenye tija.”