Ikulu, Dar es Salaam: Rais Samia apokea taarifa ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa

-Bunge la Katiba,lilipitisha Katiba Mpya(Katiba Pendekezwa )Mwaka 2014.

-Kilichobaki ilikuwa kuletwa kwa Wananchi kupigiwa kura.

-Au mchakato wa Katiba Mpya unaanza upya kwa mabilioni mengine.?

-Katiba Mpya ifanyiwe marekebisho/maboresho machache,kutoa elimu ya masuala ya katiba kwa wananchi

-kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa2024,

-Mchakato wa Katiba Mpya umefika advanced stage na kwa kufanya hivi serikali itapunguza gharama na Serikali ya awamu 6, itakuwa champion of democracy
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Dar Es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anapokea taarifa ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa leo tarehe 21 Machi 2022.

Pia soma > Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Baadhi ya NUKUU za Rais Samia

Kikosi kazi mmejihalalishia kuwa na kazi karibu miaka 9 yote iliyobaki na mimi hapa, na huku ndio kunaitwa kujiajiri wenyewe. Lengo letu ni kuwa na siasa zenye tija

Vyama vya siasa na vyombo vya habari tuwe na uhusiano mzuri, nanyi vyombo vya habari msiwe na maslahi na upande wowote, mnatakiwa kuwa kati kati"

Nitaendelea kukutana na vyama vya siasa kuwasikiliza wanataka maboresho yapi, lengo wote twende kwenye reli moja katika kufanya siasa zenye tija kwa nchi yetu"

Katika suala la kanuni za mikutano ya hadhara, sio tu kwamba ziwepo ili mikutano ianze, lakini pia kanuni zianishe atakayekiuka atafanywaje

Watu wetu hawana uelewa wa mambo ya siasa, uzalendo wala elimu ya uraia, watu wangekuwa na elimu ya uraia, uzalendo na elimu ya dunia, mauaji tunayoyashuhudia hii leo yasingekuwepo. Yote hayo hawana, ndio maana wanajifanyia tu

Tukisema tutatoa ruzuku kwa kila chama cha siasa, fedha hizo tutazitoa wapi, lakini tukikubali hilo tutakuwa kama nchi fulani kwamba kila baada ya siku 3 chama kipya cha siasa kinaundwa

Tujiulize kwa hicho tunachokitaka kwamba Tume Huru, tujifunze kwa majirani zetu, je pamoja na kuwa na hizo zinazoitwa Tume Huru hakuna migogoro? Hawatangazi matokeo na kukimbia nchi? Maana halisi ya tume huru ni hasa

Wanawake tusililie tu nafasi za uongozi, lakini tujue pia wajibu wetu kama wanawake,lolote linalotokea katika nchi sisi ndio wa kwanza tunaoumia pamoja na watoto wetu. Kuingiza wanawake katika uongozi wa siasa ni muhimu kwa kuwa sisi tuna ajenda za kuzisimamia

Nitawapa mfano katika mkoa ninaotoka, kuna mwanamke mmoja alipambana akaingia katika nafasi za uongozi, alipoingia tu alisema afadhali na mimi nitapata kununua madhahabu nijipambe, ina maana analoendea huko hakuna. Hii ni historia ya kweli

Uadilifu unaweza kurudi kwa ukali kwamba unakuwa mkali, Ukifanya hivi nitakutoa, hiyo ni nidhamu ya uoga. Tunataka uadilifu ujengwe katika mioyo na sio nidhamu ya uoga, kwamba mimi nafanya hili nisipofanya kuna mtu atakwenda kunichongea

#KaziIendelee
#TunaImaniNaSamia

---
  1. "PCCB (TAKUKURU) hawafanyi kazi vizuri ni kweli; tusiposema hatujengi nyumba nzuri; tutakaposema tutarekebisha na tutajenga nyumba nzuri."
  2. "Unaposema kila chama cha siasa kitapewa ruzuku tutakuwa kama Lesotho, kila baada ya siku mbili chama cha siasa kimeundwa watu wanataka ruzuku...hiyo haitawezekana...Unapounda chama cha siasa, umejipimaje? Utajiendeshaje?"
  3. "Uadilifu umepungua ni kweli; tufanyaje sasa? Ni elimu ya uraia, uzalendo ili kila mmoja alipo ajue anafanya nini ndiyo uadilifu utarudi katika hatua yake."
  4. "Uadilifu unaweza ukarudi kwa ukali lakini tunasema ni nidhamu ya woga. Tunataka uadilifu ujengwe kwenye mioyo na sio nidhamu ya woga."
  5. “Maboresho ya sheria na kanuni za uchaguzi, sawa mtatuambia vipengele gani vinauma, tutajadili kwa pamoja tuone pengine inawezekana tukifanya maboresho huku na mengine yote yatakayofanywa huko pengine lile kelele la Katiba likaishia kwa sababu zile kiu za watu wanapotaka Katiba ibadilishwe zilishafanyiwa kazi huku.”
  6. “Suala la rushwa ni jukumu letu wote, twendeni tukalifanyieni kazi, chaguzi zetu ziende vizuri. Sijui kama tunaweza kufanya 100% lakini tukianza kupunguza ndio tunaelekea huko, vinginevyo wasio kitu hawataingia kwenye nafasi zozote zile.”
  7. "Kuingiza wanawake ndani ya vyama vya siasa ni muhimu sana kwa sababu sisi ndiyo tuna ajenda ya kusimamia."
  8. "Kuna kazi kubwa kweli kufanya wanawake wasimame vizuri kwenye vyama vya siasa. Tusililie tu nafasi za kuingia, tujue na wajibu wetu pia tunapoingia kama wanawake."
  9. "Tuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye hili taifa kwa faida yetu (wanawake) na taifa letu kwa ujumla lakini kila siku mashaka yapo palepale."
  10. “Izo ‘codes of conduct’ za vyama vya siasa zisiwe za kukandamiza na vizuri mtakua wenyewe mnazitunga, zisikandamize, zisiue vyama vya siasa lakini zilete siasa zenye tija ndani ya nchi, isiwe kila siku tuko kwenye maBBC na CNN huko kila siku ukifungua BBC, CNN Tanzania imefanya hivi, sio ustaarabu kwa kweli, twende na siasa zenye tija.”
Kila mmoja atabeba mzigo wa matendo yake, je ndugu Samia uadilifu na uzalendo huletwa na nini na nani?, ni mazingira gani yanaleta huo huo uadilifu na uzalendo?, what are the fundamental enablers or pre-requisite as dimensions on the same.

Samia ameskip vitu very fundamental kuviongea, statehouse ongezeni class ya presidency. The World is speedy kwa Urais wa aina hii hongereni sana back office mnaongoza ikulu
 
Kati ya utumbo unaotia kichefuchefu ni huu anaoufanya yule mama. Demokrasia ya vyama vingi inaratibiwa na sheria ya vyama vya siasa ambayo iko wazi kabisa. Mijitu imekosa hoja za kushawishi watu inaanza kuzuia vyama vingine visifanye mikutano, kuvuruga uchaguzi na kubambikia watu kesi za kipuuzi.

Baadae mijitu ile ile inakuja na hoja za kijinga eti tutoe maoni!!!! Vyama vya siasa vilisharuhusiwa na sheria kufanya shughuli zao viacheni. Acheni kuvuruga uchaguzi, acheni watu wafanye siasa kwa mujibu wa sheria iliyopo, acheni wivu.

CCM wameshindwa hata kutayarisha vijana na viongozi wenye kujenga hoja za ushawishi kwa wananchi maana wamekua tegemezi kwa polisi na tume ya uchaguzi. Hawajiamini na ukitaka kujua hilo muulize mwana CCM yoyote kuhusi mambo mazito ya kitaifa uone utakavyoambulia matusi.
 
Ile kamati haikuzingaita yafuatayo ndio maana maneno yamekuwa mengi sana.

1. Umri. Vijawa walitupiliwa mbali sana hivyo maoni yale ni ya watu wa umri wa kati na wazee.

2. Wahitaji. Wenye uremavu mbalibali. Kuna haja siku nyingine wakifanya hizi makati ziweze kuzingatia haya matakwa ili kutoa nafasi ya uwakilishi.

3. Wanasiasa wa vyama vyote. Hawa nao hawajazingatiwa wote.

Hata hivyo hiyo kamati ni ya Rais, lakini kwa sasabu inasimama kwa ajli ya wnanchi ni vyema ikazingatia.
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Dar Es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anapokea taarifa ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa leo tarehe 21 Machi 2022.

Pia soma > Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Baadhi ya NUKUU za Rais Samia

Kikosi kazi mmejihalalishia kuwa na kazi karibu miaka 9 yote iliyobaki na mimi hapa, na huku ndio kunaitwa kujiajiri wenyewe. Lengo letu ni kuwa na siasa zenye tija

Vyama vya siasa na vyombo vya habari tuwe na uhusiano mzuri, nanyi vyombo vya habari msiwe na maslahi na upande wowote, mnatakiwa kuwa kati kati"

Nitaendelea kukutana na vyama vya siasa kuwasikiliza wanataka maboresho yapi, lengo wote twende kwenye reli moja katika kufanya siasa zenye tija kwa nchi yetu"

Katika suala la kanuni za mikutano ya hadhara, sio tu kwamba ziwepo ili mikutano ianze, lakini pia kanuni zianishe atakayekiuka atafanywaje

Watu wetu hawana uelewa wa mambo ya siasa, uzalendo wala elimu ya uraia, watu wangekuwa na elimu ya uraia, uzalendo na elimu ya dunia, mauaji tunayoyashuhudia hii leo yasingekuwepo. Yote hayo hawana, ndio maana wanajifanyia tu

Tukisema tutatoa ruzuku kwa kila chama cha siasa, fedha hizo tutazitoa wapi, lakini tukikubali hilo tutakuwa kama nchi fulani kwamba kila baada ya siku 3 chama kipya cha siasa kinaundwa

Tujiulize kwa hicho tunachokitaka kwamba Tume Huru, tujifunze kwa majirani zetu, je pamoja na kuwa na hizo zinazoitwa Tume Huru hakuna migogoro? Hawatangazi matokeo na kukimbia nchi? Maana halisi ya tume huru ni hasa

Wanawake tusililie tu nafasi za uongozi, lakini tujue pia wajibu wetu kama wanawake,lolote linalotokea katika nchi sisi ndio wa kwanza tunaoumia pamoja na watoto wetu. Kuingiza wanawake katika uongozi wa siasa ni muhimu kwa kuwa sisi tuna ajenda za kuzisimamia

Nitawapa mfano katika mkoa ninaotoka, kuna mwanamke mmoja alipambana akaingia katika nafasi za uongozi, alipoingia tu alisema afadhali na mimi nitapata kununua madhahabu nijipambe, ina maana analoendea huko hakuna. Hii ni historia ya kweli

Uadilifu unaweza kurudi kwa ukali kwamba unakuwa mkali, Ukifanya hivi nitakutoa, hiyo ni nidhamu ya uoga. Tunataka uadilifu ujengwe katika mioyo na sio nidhamu ya uoga, kwamba mimi nafanya hili nisipofanya kuna mtu atakwenda kunichongea

#KaziIendelee
#TunaImaniNaSamia

---
  1. "PCCB (TAKUKURU) hawafanyi kazi vizuri ni kweli; tusiposema hatujengi nyumba nzuri; tutakaposema tutarekebisha na tutajenga nyumba nzuri."
  2. "Unaposema kila chama cha siasa kitapewa ruzuku tutakuwa kama Lesotho, kila baada ya siku mbili chama cha siasa kimeundwa watu wanataka ruzuku...hiyo haitawezekana...Unapounda chama cha siasa, umejipimaje? Utajiendeshaje?"
  3. "Uadilifu umepungua ni kweli; tufanyaje sasa? Ni elimu ya uraia, uzalendo ili kila mmoja alipo ajue anafanya nini ndiyo uadilifu utarudi katika hatua yake."
  4. "Uadilifu unaweza ukarudi kwa ukali lakini tunasema ni nidhamu ya woga. Tunataka uadilifu ujengwe kwenye mioyo na sio nidhamu ya woga."
  5. “Maboresho ya sheria na kanuni za uchaguzi, sawa mtatuambia vipengele gani vinauma, tutajadili kwa pamoja tuone pengine inawezekana tukifanya maboresho huku na mengine yote yatakayofanywa huko pengine lile kelele la Katiba likaishia kwa sababu zile kiu za watu wanapotaka Katiba ibadilishwe zilishafanyiwa kazi huku.”
  6. “Suala la rushwa ni jukumu letu wote, twendeni tukalifanyieni kazi, chaguzi zetu ziende vizuri. Sijui kama tunaweza kufanya 100% lakini tukianza kupunguza ndio tunaelekea huko, vinginevyo wasio kitu hawataingia kwenye nafasi zozote zile.”
  7. "Kuingiza wanawake ndani ya vyama vya siasa ni muhimu sana kwa sababu sisi ndiyo tuna ajenda ya kusimamia."
  8. "Kuna kazi kubwa kweli kufanya wanawake wasimame vizuri kwenye vyama vya siasa. Tusililie tu nafasi za kuingia, tujue na wajibu wetu pia tunapoingia kama wanawake."
  9. "Tuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye hili taifa kwa faida yetu (wanawake) na taifa letu kwa ujumla lakini kila siku mashaka yapo palepale."
  10. “Izo ‘codes of conduct’ za vyama vya siasa zisiwe za kukandamiza na vizuri mtakua wenyewe mnazitunga, zisikandamize, zisiue vyama vya siasa lakini zilete siasa zenye tija ndani ya nchi, isiwe kila siku tuko kwenye maBBC na CNN huko kila siku ukifungua BBC, CNN Tanzania imefanya hivi, sio ustaarabu kwa kweli, twende na siasa zenye tija.”
Naweza kusema kitu kimoja kikosi kazi kimefanya kazi nzuri ila kwa uoga au maelekezo fulani hii ni kama white paper unaambiwa ni white paper huku kuna maelekezo anuwai kuwa fanya hiki na hiki.hiki kiwe hivi ,hiki usiguse kabisa.

Humu nchini kuna watu hata kama watafanya Maamuzi mazuri kiasi gani hawaaminiki hata kidogo na wakijumuishwa ktk group fulani Watu wote wanaonekana wa hovyo.

Pia humu kwenye nchi kuna watu wanaaminika sana hata kama watatoa mapendekezo ya hovyo bado Watu watawaunga mkono . Mfano kama Warioba. Swala lolote la kisiasa kwanza linaongozwa na utashi je hao Watu ni wakweli ,pili Dhamira je hawo Watu lengo lako nini?

Kwahiyo watu wakishaona tu majina fulani kwenye swala fulani hapohapo wanajenga Taswira ya utashi na dhamira ya Muhusika.kwamfano mimi nilipoona hili kundi lililochaguliwa kufanya huu mchakato moja kwa moja nilireflect kwenye haya haya majibu yao.kwasababu ni Watu wanaojulikana dhamira zao.

Mimi kwa upande wangu niseme wamefanya kazi kubwa lakini bado haijakidhi hata 1% ya matarajio ya watanzania kikubwa tu ninachoweza kusema Watu wamepata pakuanzia,huu ni mwanzo mzuri wamichakato mingine itakayo kuja.

Siku zote wanasiasa huwa wanataka maamuzi ya kukidhi leo na viongozi waliopo madarakani wanataka maamuzi yakulinda madaraka yao.huku wananchi wakitaka maisha bora.Bila makundi haya matatu kukaa pamoja nakupata muafaka siku zote tutapata katiba ya zima moto,ambayo haitawafaa viongozi,wala wanasiasa wala wananchi,wote watakuwa watumwa wakutojua kesho yao.

kwahiyo pamoja mimi kuwapa 1% ila bado nawapongeza at least tunaona mwanga kidogo huko tuendako.
 
  1. “Izo ‘codes of conduct’ za vyama vya siasa zisiwe za kukandamiza na vizuri mtakua wenyewe mnazitunga, zisikandamize, zisiue vyama vya siasa lakini zilete siasa zenye tija ndani ya nchi, isiwe kila siku tuko kwenye maBBC na CNN huko kila siku ukifungua BBC, CNN Tanzania imefanya hivi, sio ustaarabu kwa kweli, twende na siasa zenye tija.”
Mtoto huwa analia pale mahitaji yake yasipotimizwa. Kama mama hataki mtoto alie CNN na BBC basi atimiziwe mahitaji yake.
 
Back
Top Bottom