Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe Ikulu Mkoani Dar Es Salaam.

Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.

Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

====

Picha Mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022

Ninatabiri mengi mema yatajitokeza "including" Katiba Mpya.
 
Waliosema mbowe ni gaidi wanaficha wapi sura zao? Yu wapi Dr. Mihogo?
 
Kwenda direct Ikulu kutabadilisha kwa kiasi kikubwa hotuba atakayotoa kwa wana Chadema na waandishi wa habari. Bila shaka hotuba yake itaondoa maneno makali ambayo angetoa kama asingekwenda.
Uko sahihi kabisa
 
Unaishi Tanzania kweli?
zito alimuombea msamaha mbowe alijibiwa nini?
Alikuwa crushed kwa kuwa those people who know him well could read through him, alijiaibisha na walimkana hadharani mnafiki yule. Kama kuna watu bado wanawasikiliza sellouts kama Zitto inafikirisha sana.
 
Ndivyo ilivyo mkuu.
Na ndio hapo tunaona wazi kwamba, tatizo sio chama fulani kukaa madarakani kwa muda mrefu bali tatizo ni wale wanaoongoza. Nadhani hii ni hoja pana sana na inahitaji mjadala. Je, siasa za hapa nchini, tatizo ni chama tawala au kiongozi? Kama samia anaonekana mwema na mwingine alionekana mbaya, ilihali wote wanatokana na chama kimoja; je tatizo ni mtu au chama?[emoji848]
Hata chama kinaweza kuwa tatizo kwa kujipa hati miliki bandia ya kuongoza nchi. Wakati mwingine chama kimoja kinaweza kuzuia au kupunguza uhuru wa kutoa maoni na kufanya siasa, hivyo kuwepo kwa vyama vingi vyenye sera tofauti vinatoa nafasi pana zaidi kwa wananchi kushiriki katika uongozi wa Taifa lao.
 
Tunategemea chadema itaendelea na mapambano ya kudai Haki na uhuru wa vyama vingi hili likishindikana basi tena tujiunge wote na ccm tu hakuna namna. Kwahiyo mwenyekiti pamoja na yote mliyozungumza na Rais samia leo baada ya kutoka gerezani hilo naomba uliweke akilini.
Bila kusahau katiba mpya
 
Huyu baba ilibidi apumzike yaani katoka leo safari Ikulu
Wewe ukiitwa ikulu unaweza kusema subiri nitakuja.kwasababu hiyo ni dhahiri Rais ndiye aliyemuita mbowe.sasa ni nani anayeweza kukataa au kuhairisha wito wa rais wa nchi ata kwa dakika moja.labda kama hujipendi.
 
Katiba mpya na Tume Huru ya uchaguzi ndio mzizi wa mjadala ule
TATIZO LAKO NA WEWE nemsema mbowe akisema kwa sasa tusubiri tunajipanga baada ya muda ndiyo tutaanza kudai katiba mpya mtasema sawa mkuu maana mbowe hakoseagi na kila akisemacho lazima mkubali?
 
Wewe ukiitwa ikulu unaweza kusema subiri nitakuja.kwasababu hiyo ni dhahiri Rais ndiye aliyemuita mbowe.sasa ni nani anayeweza kukataa au kuhairisha wito wa rais wa nchi ata kwa dakika moja.labda kama hujipendi.
Duh nidhamu ya uwoga naipinga vikali na kwa bahati nzuri sina
 
Serikali imetumia timing mbaya kumkamata na kumuachia MBOWE kwa kifupi serikali imejidhalilisha.....
 
Mwenyekiti ameshakuwa na adabu
Alikuwa crushed kwa kuwa those people who know him well could read through him, alijiaibisha na walimkana hadharani mnafiki yule. Kama kuna watu bado wanawasikiliza sellouts kama Zitto inafikirisha sana.
 
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe Ikulu Mkoani Dar Es Salaam.

Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.

Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

====

Picha Mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022

"Gaidi"anaporuhusiwa Kufika Ikulu kuona na amiri jeshi mkuu!!
Watu kama Siro,na polisi wote walioshiriki kutengeneza huu mchongo wakiona hivi,wanajisikiaje?
Mishuzi,kiu
 
Back
Top Bottom