Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

Mimi sishauriwi, ukinishauri ndio umeharibu kabisa, ashukuriwe Mungu kwa kutuondolea mzimu ule haya yote tusingekuwa tunayaona, Tundu Lissu na wenzake wangeozea ukimbizini, kwa mwendelezo huu ninamuona Lissu na wenzake wakirudi nchini mwao kama raia huru.
Lissu na wengine wengi tungebaki kwenye vitabu vya kumbukumbu...!
Hii nchi ilielekezwa njia ya kuzimu kwa spidi kubwa sana.
 
Ninachojiuliza ..kwa Nini Samia ametumia mda mrefu hivi ...Jambo hili likachukua mda wore huo...!?
ALITAKA KUMLEGEZA MPINZANI,,,,,,,,,,AWE LAINI KIDOGO.
Si unaona mbowe amekuja kwa mama mikono nyuma?
kiburi na ujeuri vyote kaviacha celo. 😁😁😁
 
Naona Mama anafuata nyao za Uhuru hapo kenya, ya nini kugombana njoo tukae tuzungumze na tuelewane ilimradi mambo yaende vizuri.
 
Kuna Mpambanao wa Uchawa Mkubwa Kati ya Cdm na Act-w, acha Tuone Huu Mpambanao Wao. Bwana Nyepesi Hapo Roho itakuwa inamuuma Sana [emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Mama ni mkatili hata mseme sijui Mzanzibari, sijui Muislamu, nk. Ongea yake tu anaonekana ana dharau, chuki na kiburi Sana lakini Wananchi tukisimama zaidi kiburi chake kitaisha.
 
Mimi sishauriwi, ukinishauri ndio umeharibu kabisa, ashukuriwe Mungu kwa kutuondolea mzimu ule haya yote tusingekuwa tunayaona, Tundu Lissu na wenzake wangeozea ukimbizini, kwa mwendelezo huu ninamuona Lissu na wenzake wakirudi nchini mwao kama raia huru.
Kweli kabisa Mkuu

Mama SSH anajenga Tanzania bora sana....ni vema washauri wake wajitafakari na wasimpotoshe....Amani ndio msingi wa maendeleo...madaraja na fly over bila amani ni sawa na bure.
 
Huyu Mama ni mkatili hata mseme sijui Mzanzibari, sijui Muislamu, nk. Ongea yake tu anaonekana ana dharau, chuki na kiburi Sana lakini Wananchi tukisimama zaidi kiburi chake kitaisha.
Mi naona si kweli, Mama hayupo hivyo.
Bi, Mkubwa yupo fresh tu,,,,,,, ana sura angavu yenye mvuto,,,,,, ana macho mazuri yenye kukufanya upate kiu ya maji kila uyaonapo.
Kauli zake ni Thabiti, zenye kukufanya UTII bila shuruti.
Mungu anajua ni kwanini Mama anatufaa kwa awamu hii na si mwingine.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bwashee ile tu kwenda ikulu ni kumsujudia hangaya!



Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Siyo kweli kwamba Mbowe kukubali kwenda ikulu ni kuomba msamaha.

Tangu mwanzo hata kabla ya kubambikiwa kesi Mbowe hakuwahi kuona tatizo yeye kukutana na Rais. Rejea kauli zake za kutaka mardhiano ya kitaifa.

Lakini pia kwa nini usifikiri kwamba hata Rais anaweza kumwomba msamaha Mbowe "personally" màana kwa hakika tayari ameshagundua kuwa alidanganywa kuongea uongo bbc.

Mbowe angetaka kuomba msamaha angeomba tangu mwanzo hata kabla ya kukaa muda wote huo,

Mbona hujaongelea sanaa walizofanya serikali kupitia kwa Zitto, na dini ili kuficha aibu ya kesi ambayo kwa namna ilipokuwa imefika ilikuwa imeshaivua nguo serikali na zaidi ilikuwa inamuumiza Hangaya hivyo alikuwa akisaka "nitoke vipi"
 
DPP, Mahakama, TISS, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ufanyanyaji kazi wake ni sawa na taasisi zingine za serikali zilizo independent kama TANESCO, halmashauri, mkoa, Bandari, Uhamiaji, TPDC, EWURA, PPRA, NSSF and so forth.

Hizo taasisi zote ni independent on books; lakini raisi anaweza influence sio kwa katiba ila kwa maslahi ya nchi au yake.

Magufuli angetaka kumfungulia case Mbowe kwa ushahidi uliotumika chini ya admin angefanya ivyo ndani ya muda wake, J.K angetaka kumfungulia case Mbowe ya mabomu Arusha na kuitisha maandamano ya vurugu angefanya ivyo. Hayo makosa yote yapo katika orodha ya penal codes na sheria zake.

Maana yake nini Mbowe akushitakiwa kwa J.K na Magufuli ni kwa sababu itakuwa walizuia tu.

Vinginevyo TISS, DPP, Mahakama, TAKUKURU bila ya kuingiliwa na wana siasa can do a lot of damage.

Given the evidence Mbowe kashitakiwa na vyombo husika wala mama Samia ahusiki na mashtaka, siasa zimeingia kuzima kesi tu kwa mustakabali mpana wa nchi. Na hakuna mtu anaewatuma kufanya kazi za undercover ni sehemu ya majukumu yao kuzuia uhalifu na kushitaki, sasa CDM viongozi wao wakikutwa na hatia wanaingiza siasa as if hizi taasisi za ulinzi zipo kama majina tu.

Lakini kwa ushahidi uliotumika Magufuli angekuwa na nia nae hiyo kesi angeigiza zamani

Vyombo vingine pia vinamamlaka ya kulinda nchi kwa sheria zilizozianzisha ivyo vyombo kwa hiyo sio kila hatua zao ni siasa.

Wakikuona unatumika na watu wa nje wakafanya yao sio lazima wametumwa na mwanasiasa au raisi ni katika majuku yao tu.

That is to say based on evidence kwenye case ya Mbowe jamuhuri ilithibitisha there was enough evidence of ‘mens rea’ ndio maana mahakama ikaona kuna kesi ya kujibu.

Muhimu hapa ni kuacha kujiongopea mtu kama ni invisible katika mipango ya ovyo jamaa wakiamua kufanya yao mziki keshauona; bila ya msamaha wa nyuma ya pazia wa kisiasa taasisi zingine zingemmaliza Mbowe kwa mipango yake ya kipuuzi with evidence.

Tueshimu sheria za nchi, usivinje halafu ulaumu wanasiasa kama ilivyo kwa wafuasi wa CDM, hope Mbowe kajifunza somo lake.
Hakuna cha kujifunza kwenye upuuzi ule ulioitwa 'kesi' na ndiyo maana kila mwenye utimamu wa akili aliita 'kesi ya mchongo', kuna vitu vinakuwa obvious mpaka vinatia aibu serikali kama ilivyokuwa kesi ya Mbowe.
Huo utoto wa kwamba eti vyombo vya dola viko free labda hayo aambiwe mtoto aliyezaliwa jana, tokea phase ya Mchonga ilikuwa ikijionyesha vyombo vya ulinzi na usalama hasa TISS na polisi ufanyaji kazi wao hu-reflect msimamo wa rais aliyeko madarakani.
Rais ambaye hakuwa na utu na wala hakuthamini uhai wa mtu yoyote aliyetofautina naye kiitikadi kama alivyokuwa Magu polisi walikuwa brutal sana na TISS walipoteza sana watu, kwa phase hii dalili zinavyoonyesha hakutakuwa na kutunguana hadharani kama ilivyotokea kwa Lissu kule Dodoma mchana kweupe huku walinzi(security guards) na polisi wakiondolewa eneo la tukio ili 'zoezi' lifanyike au watu kupotezwa kama ilivyotokea kwa Ben Saanane au kutekwa, kuteswa na kutupwa vichakani kama ilivyotokea kwa Mdude Nyangali. Jinai ziende mahakamani si kutekana na kutesana kisa posts za mitandaoni.
Maelezo yako hayana mashiko hata kidogo.
 
Mungu wa mbinguni ni mwema!

Akina Swila na wale waliomnyima chakula Mbowe kwa miezi 5 wakiona hii picha sijui hata wanawazaje!

IMG_20220304_154503_924.jpg
 
Mungu wa mbinguni ni mwema!

Akina Swila na wale waliomnyima chakula Mbowe kwa miezi 5 wakiona hii picha sijui hata wanawazaje!
na wale akina Erythrocyte waliokuwa hawataki atoke kwa huruma mpaka kesi iishe sijui wanajisikiaje mbowe akikiri k uacha fujo mbele ya rais na watanzania wote wakimsikiliza?
 

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe Ikulu Mkoani Dar Es Salaam.

Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.

Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

====

Picha Mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022

Bado natafakari ya mbwa wangu watatu. S S na K yaani Sirro Slaa na Kigogo2014. Hivi wataweza kubweka tena""
 
Back
Top Bottom