IKULU: Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi

IKULU: Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi

One year later we celebrate the downfall of the two despots.
 
Rais Magufuli leo saa 3.00 asubuhi ananamuapisha Katibu mkuu kiongozi mteule Dr Bashiru Ally.

Tukio hili muhimu litakuwa mubashara katika luninga zote za ndani zikiwemo Upendo tv, ITV, TBC, Channel ten, Star tv nk

Karibu.

Updates:

Rais Magufuli ameshaingia ukumbini na Dr Bashiru anakula kiapo chake cha ubalozi na kitafuatia cha ukatibu mkuu kiongozi.

Na sasa Katibu mkuu kiongozi balozi Bashiru anakula kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Mwangesi ambaye ni Kamishna wa Tume ya Maadili!

===

Dkt. Bashiru Ally leo ameapishwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema alipata taarifa za uteuzi kupitia Mitandao ya Kijamii.

Akizungumza baada ya kula kiapo, ameeleza kuwa kwa maadili na utamaduni, kazi za Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi sio kazi za maneno bali ni za kusikiliza, kujifunza na kuchambua, kuamua na kutenda.

Amesema, "Wale waliotegemea kwamba nitazungumza tena kwa kweli nitazungumza kwa tahadhari na umakini kwasababu kiapo mmekisikia. Ni Katiba, Sheria, taratibu, mila, desturi".

Aidha, amezungumzia suala la umuhimu wa mawasiliano ndani ya Serikali na kati ya Serikali na Umma akisema watasimamia hilo

Congratulations
 
Back
Top Bottom