Background Check
JF-Expert Member
- Jun 28, 2019
- 341
- 498
Salam ndugu zangu | JF na watanzania kwa ujumla 🇹🇿
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote kwa kutujalia nafasi ya kuwa hapa siku ya leo. 28 March 2021. Pia nipende kutoa pole kwa ndugu zangu watanzania wote kwa msiba wa Hayati Dr. John Pombe Magufuli, roho yake ilazwe mahala pema.
___________
Leo Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, alikuwa napokea taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) pamoja na ile ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuwia Rushwa (TAKUKURU).
Hafla hiyo imefanyika Ikulu ya Chamwino – Dodoma.
Nampongeza Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa hatua ambazo ambazo ameanza kuchukua dhidi ya watu ambao, kwa kiasi kikubwa bado wanatumia nafasi/ofisi zao kupiga madili. Imani yangu kwa Rais imeongezeka baada ya kumsimamisha mara moja Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, Eng. Deusdedit Kakoko.
Kimoyomoyo; nimefurahi pale niliposikia kalipio la Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Selemani Jafo. Hii ni kutokana na taarifa ya CAG kuwa moja ya mamlaka za serikali zilizo chini ya wizara yake zina hati chafu ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Hili Mh. Jafo anatakiwa kulichukulia serious ili kumsaidia Mh. Rais kuiongoza nchi vyema.
Ujue sauti ya Mama Samia ni sauti ya upole lakini kwa wataalamu wa sauti watakubaliana na mimi kuwa sauti yake haimaanishi upole inamaanisha kufanya kazi kwa kwa bidii bila kuficha maovu. “naomba sasa ulimi wako usiwe na utata” ni sauti ya Mh. Rais akimweleza CAG kuwa kwa taarifa nyingine akiwasilisha basi asifichefiche kitu aeleze wazi ili serikali ichukue hatua mathubuti.
Pongezi pia kwa CAG amekuja na njia mpya ya ukaguzi wa hesabu katika miradi inayoendelea kutekezwa njia hii inaitwa Real Time Auditing, njia ambayo inatoa nafasi kukaguliwa kwa miradi ikiwa inaendelea, njia hii inaruhusu mabadiliko ya haraka ya namna ya kudhibiti ufujaji wa pesa za umma kabla hata ya mradi kukamilika.
Ni njia bora kwahili pongezi kwa CAG na jopo lake, sema wanatakiwa waongeze juhudi isije kuwa ni maneno tu ya kwenye runinga, wajikite zaidi katika utekelezaji wa mbinu hii na mbinu nyingine za kisayansi zaidi.
Kuhusu Shirika la ndege nchini (ATCL) limeendelea kuingiza hasara, hii nadhani waendelee kuweka nguvu kuhakikisha kuwa shirika hili haliwi mzigo na wala haliingizi hasara kwa siku za usoni. Ndege haziwezi kuingiza faida ndani ya miaka hii michache. Hakuna biashara inayoanza kuingiza faida ndani ya muda mfupi baada ya kuanzishwa kwake tulipe muda. Lakini wasitumie kama njia ya kujipigia pesa eti kwa sababu shirika ndo linaanza kujiimarisha.
Kesi zisizo na dalili ya serikali kushinda zifutwe, hii nadhani pia hata hayati aliwahi kuligusia, serikali ina kuwa na kesi nyingi halafu inashinda kesi ndogo sana, haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma lakini pia ni kupoteza muda ambao ulitakiwa utumiwe kutatua kesi nyingine za wanyonge. Kwahili pia Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan nipende kusema wewe ni kuongozi mwenye maono mazuri na taifa letu litasonga mbele zaidi na zaidi.
MAONI KWA WAFANYAKAZI WA IKULU
Nashauri kuwa wafanyakazi wa Ikulu nadhani ni kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ama wengine wanao husika maana sijui wanaitwaje ambao huwa wanaada hafla kama hii ya leo. Wanatakiwa wawe ‘very smart and informed’.
Mfano; wanafahamu wazungumzaji wakuu wa leo kuwa alitakiwa kuzungumza CAG na Mkurugenzi wa TAKUKURU pamoja na Mh. Rais. Nafikiri wangewawekea zile wireless mic kabla ya kwenda kumkabidhi Mh. Rais vile vitabu vya taarifa, kwa dakika moja hivi hatukusikia sauti hadi pale mtu alipoeda kushikiria mic ili sauti ya CAG isikike akiwa anakabidhi.
Yangu kwa leo ni hayo tu!!
Machepele wa Tanzania🇹🇿
28/03/2021
________________
Kwa anayeweza kufafanua kuhusu haya hapa chini atakuwa amenisaidia kujijibu maswali yangu yanayozunguka kwenye akili yangu.
1. Ni nani anafanya ukaguzi kwa (ofisi ya)/mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali?
2. Hivi Mh. RAIS anasoma vitabu vyote hivyo vya taarifa zilizotolewa leo? Au huwa kuna division ya usomaji kweye cabiet ya wasaidizi wa Rais?.
3. Rushwa ya ngono itaisha lini kwenye taasisi ya elimu ya juu? Na ni lini itakoma tabia ya akina dada ya kufanya ushawishi wa kigono kwa wahadhiri? Na je kwa nini wasiwe wana adhibiwa wote mtoaji wa rushwa ya ngono na mpokeaji ili hawa wadada wasiwe wanafanya ushawishi?
Tamisemi haiwezi kugawanywa? maana naona ni wizara kubwa sana