Ikulu, Dodoma: Makabidhiano ya Ripoti ya CAG - Machi 28, 2021

Ikulu, Dodoma: Makabidhiano ya Ripoti ya CAG - Machi 28, 2021

Nasema hivi, upinzani ndio unazikwa rasmi sasa kama huelewi muazime lissu akili akusaidie..wewe tukana upendavyo...
Acha uchama wewe, angalia kazi nzuri ya rais, kwani upinzani ukimsifia rais kwa kazi nzuri kuna shida gani?, nyie ndio watu unaowaponza viongozi wetu . Namshauri rais akae mbali kabisa na watu wa aina yako.
 
Mkuu kama hutajali ukiachana na id fake ingekuwa inawezakana tungekutana au tufanye mdahalo humuhumu wowote itangejulikana
Kutofikia malengo ya faida ndio unaita hasara?
Unajua faida au hasara inapatikanaje, vipi unajua kuhusu break even.
 
Mkuu haswa japo huwa haiwekwi wazi toka umeanza kusikia tanesco kuna mwaka imepata faida mbona haifi kama huamini fatilia
TANESCO itaendeshwa na ruzuku kama haina faida, hutokaa usikie imefirisika serikali sio kichaa iache nchi gizani na viwanda visimame isipate kodi. Kuna biashara zinaendeshwa ili kusaidia biashara nyingine, unahisi kwa nini Qatar wanakomaa na Qatar Airways au UAE wanakomaa na Fly Emirates wakati nchi kama USA na UK hazina national carrier wakati wana makampuni ya kutengeneza ndege.
 
kwa mazingira ya ATCL yalivyokuwa mwanzo hali ilikuwa mbaya zaidi.
Je tumeweza kujiuliza ATCL kabla ya hizi ndege ilikuwa inatengeneza hasara kiasi gani?
lakini ifahamike kuwa upo uwezekano walikuwa na variable cost nyingi kwa kuwa lilishashindwa kujiendesha.
pia tukumbuke matarajio mengine ya kipato yalitegemewa kutokana na safari za nje ambazo zilikufa kutokana na Korona wakati shirika lilishalipia vibari na kufanya promotion kwa safari hizi na hazikufanyika.
haya ni machache ambayo mimi kwa uelewa mdogo naweza kueleza japo yapo mengi tu ikiwemo ununuaji wa samani zinazoweza kufanana na huduma tarajiwa ikiwemo pia utengenezaji wa mifumo ya IT.
kwa hiyo ni sawa sana tu.
Ni sawa kabisa....inashangaza kwa tuliamini hakuna mambo hayo
 
Unategemea shirika lililofufuka 2018 kutengeneza faida?

Hata fleet ya ATCL bado changa sana. Mpango wa ATCL ulikuwa ni kuanza kutengeneza faida 2022 baada ya kupata ndege zote zilizotarajiwa. Hali ya covid-19 huenda ikarudisha nyuma mipango hiyo.

Ngoja wakianza safari nyingi za kimataifa ndiyo tuwahukumu. ATCL ilikuwa mahututi huwezi kutegemea watengeneze faida ndani ya miaka miwili.
Tell that to your choir praise team, wamekua wakisema it has been profitable all year through
 
kwa mazingira ya ATCL yalivyokuwa mwanzo hali ilikuwa mbaya zaidi.
Je tumeweza kujiuliza ATCL kabla ya hizi ndege ilikuwa inatengeneza hasara kiasi gani?
lakini ifahamike kuwa upo uwezekano walikuwa na variable cost nyingi kwa kuwa lilishashindwa kujiendesha.
pia tukumbuke matarajio mengine ya kipato yalitegemewa kutokana na safari za nje ambazo zilikufa kutokana na Korona wakati shirika lilishalipia vibari na kufanya promotion kwa safari hizi na hazikufanyika.
haya ni machache ambayo mimi kwa uelewa mdogo naweza kueleza japo yapo mengi tu ikiwemo ununuaji wa samani zinazoweza kufanana na huduma tarajiwa ikiwemo pia utengenezaji wa mifumo ya IT.
kwa hiyo ni sawa sana tu.
Kwaiyo kwa maoni yako corona imesaidia kupunguza hasara.
 
Yaani tulivyo shuhudia Prof. Assad alivyo furumishwa unceremonously kutoka ofisini, akawa humiliated further na Spika wa Bunge, one could sense kulikuwa kumejengeka uadui mkubwa baina ya Spika Ndugai, baadhi ya wabunge dhidi ya Prof. Assad wa watu.

Kilicho mponza Prof. Assad ni kusema ukweli bila ya kumungunya maneno, ni hicho tu na wala hakuna kingine.

Rai yangu kwa Mh. Rais S.S. Hassan, tafadhali mrudishe fasta Mzalendo wa kweli Prof. Assad kwenye wadhifa wa CAG, Prof. Assad ni jasiri sana, anajali sana ethics za kazi yake, aogopi kusema ukweli lets what comes may, ali-train ma auditors kwa kiwango cha juu, hana makuu na ni mvumilivu sana.

Tunayasema haya kwa nia njema tu, tunakuwa wakweli hapa ni hivi: Prof. Assad ndiye atakusaidia sana kuwashukia kama mwewe wezi na wabadhirifu walio kubuhu Serikalini na kwenye mashirika ya UMMA - mama huna haja ya kumkumbusha CAG kwamba awe muwazi zaidi - hiyo ndio kazi yake i.e to call a spade a spade na sio kuletewa report ambayo sehemu nyingine haiko transparent ikiwa ni mbinu za kutaka kuwalinda waharifu kiaina - please recall Prof. Assad.
Prof Assad pekee ndiyo anaweza kumsaidia huyu Mh. Rais Wetu Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na mijizi. Ikimpendeza tunaomba amrejeshe Assad kuwa CAG. Yaani au hata ampe special task kwa kazi hiyo ila UCAG ndiyo safi. Huyu CAG aliyesimikwa na yule mpenda Ukanda na Ukabila hana lolote zaidi ilikuwa ni kulinda mambo yake ya miradi pendeleo. Mungu ndiyo Kiboko yetu sote aisee. Tutende tu kwa haki.
 
CAG aliyepita prof Assad alitoa ripoti mbaya ya ununuzi wa hizo ndege matokeo yake Ndungai akamvalia njuga hadi akatolewa, na Mara zote mkuu aliyepita alitangaza faida ya hizi ndege. Mkaguzi Kichere atuambie ni kweli hii ndiyo taarifa aliandaa kumpelekea JPM au ameiedit baada ya kugundua kuwa anaepelekewa siyo JPM tena.

I have every reason to believe that the CAG report has been edited to suit the new circumstances. There is no way Kachele would have included the report on the financial performance of ATCL if the report was to be presented to Magufuli! Kama mtakumbuka kuwa mahesabu yote ya ATCL yalikuwa yanafichwa yasionekane na Wananchi!.
 
CAG aliyepita prof Assad alitoa ripoti mbaya ya ununuzi wa hizo ndege matokeo yake Ndungai akamvalia njuga hadi akatolewa, na Mara zote mkuu aliyepita alitangaza faida ya hizi ndege. Mkaguzi Kichere atuambie ni kweli hii ndiyo taarifa aliandaa kumpelekea JPM au ameiedit baada ya kugundua kuwa anaepelekewa siyo JPM tena.
Ripoti ndo hiyohiyo hakuna nyingine.
 
Hii ripoti haikusubiri hata utengano wa nyonga na tumbo vya marehemu.

Yaani km angeweza kushuhudia haya yanayoanza kujidhihirisha nae km Mpenzi mtazamaji amini nawaambia tumbo la uharo lingemkumba maiti huyo.
Ripoti inatakiwa kukabidhiwa kabla ya tarehe 29 mwezi March ba ndio maana imeingizwa fasta hapohapo hakukuwa na namna na vyote vilikuwa kwenye ratiba tayar.
 
Unajua kama usipokuwa na akili ya Mataga Mataga, kunamambo mepesi sana kuyajua hata kama CAG hakuyasema, wewe ujiulize hv ndege tukizonunua ni zipi zinazofanya route za kimataifa na mara ngapi kwa wiki au kwa mwezi mbona unapata jibu
 
Kuna madini aliyafinyia kwa ndani ila baada ya mchezo kubadilika akakesha na kuyarejesha kwenye report.
Mama pia amempa moyo CAG na amemsisitiza afunguke asifiche-fiche mautopolo.
 
Back
Top Bottom