IKULU mawasiliano inahitaji data analyst and propagandist, sio mwanahabari otherwise Rais atabadili sana. Mchukueni David Kafulila

Mimi nakuambia ukweli,kama hutaki siwezi kukulazimisha. Hili mlilolifanya mmemualibia sana badala ya kumjenga. Angalia hata comments za wadau. Wakati mwingine chawa mnaharibu badala ya kujenga
Nitaendelea kusema UKWELI Daima bila kuogopa.kuwa Mheshimiwa David Kafulila ni mtu mchapakazi sana na kiongozi mwenye uwezo mkubwa sana wa kiuongozi. Na kwa hakika atafaa sana ikiwa atapewa nafasi ya Ukurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu
 
🤣🤣🤣 Sisi tunaoandika hapa ndio CCM wenyewe na wewe unayebisha ni CHADEMA Sasa wapi na wapi hapo???
Ningekuwa CHADEMA ninge support hiyo nonsense. Ila ni uhakika CCM siyo wapuuzi kuruhusu mgeni kupata kitengo kwenye kitengo nyeti kama cha mawasiliano ikulu
 
Ningekuwa CHADEMA ninge support hiyo nonsense. Ila ni uhakika CCM siyo wapuuzi kuruhusu mgeni kupata kitengo kwenye kitengo nyeti kama cha mawasiliano ikulu
Mgeni ni wewe ila Sio Kafulila, Tanzania chama ni kimoja tu CCM hawa wengine ni uwanja wa mazoezi
 
Kafulila yes👏🏿👏🏿👏🏿
 
Ngoja tuone kama ni kweli atateuliwa ntajua kweli Mama Yuko serious
 
Huyu jamaa ni sawa IKULU inataka kijana mjanja janja sana
 
Binafsi nakubaliana na wewe kwasababu toka siku Zuhura alivyoteuliwa niliwaambia watu kuwa Mkurugenzi wa Ikulu hatakiwi kuwa "mwanahabari tu" lazima awe mbobevu wa siasa za ndani na nje na awe na weledi kupangalia mambo sio "kutoa habari tu"

Kafulila ana kipaji hicho kwasababu anajishughulisha sana kujua mambo mengi
 
Nakubaliana na wewe kwenye hili, Kafulila ndio mtu pekee anaweza ku-drive agenda kutoka IKULU kwenye Uraiani.
 
Naunga mkono hoja yako.kuwa nafasi hiyo itamfaa sana Mheshimiwa Kafulila na kusaidia sana katika kutolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mtambuka.
 
Ngoja tuone kama ni kweli atateuliwa ntajua kweli Mama Yuko serious
Tuendelee kumuombea .lakini nina imani kubwa sana na mheshimiwa Rais wetu na naamini anatambua kipawa na Karama ya uongozi na uwezo mkubwa wa kiuongozi alionao Mheshimiwa Kafulila
 
Ningekuwa CHADEMA ninge support hiyo nonsense. Ila ni uhakika CCM siyo wapuuzi kuruhusu mgeni kupata kitengo kwenye kitengo nyeti kama cha mawasiliano ikulu
Mheshimiwa Kafulila siyo mgeni.ni mtu mzalendo,mchapa kazi na muaminifu sana. Amekuwa Ras,Rc na sasa mkurugenzi wa PPP nafasi ambazo ni nyeti sana. Lakini kumbuka kuwa kwa sasa waziri wa mipango na uwekezaji Mheshimiwa Prof Kitila Mkumbo ametokea upinzani na ameaminiwa na kuwa waziri na hivyo kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri.sasa wewe huoni ni nafasi nyeti hiyo? Mheshimiwa Kafulila anazosifa zote za kutosha na kutekeleza vyema majukumu ya nafasi hiyo ya ukurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu
 
Kafulila ni mtu Sahihi ila kule PPP pia ni muhimu zaidi
Akiwa mkurugenzi wa PPP atafanya vizuri zaidi na kuiunganisha vyema serikali na wananchi kwa kuipa taarifa kwa kina zenye uchambuzi ndani yake,hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Mheshimiwa Kafulila anauelewa mkubwa sana wa masuala ya uchumi. Hivyo hataishia kutoa tu habari bali atafanya na uchambuzi wa kitakwimu.
 
Bora wamchukue manara
 
2025 Rais ni mmoja tu Mama Samia Suluhu Hassan.

Kafulila hana ndoto ya Urais ataomba ridhaa Kigoma Kask kuwa mbunge wao,
Tutarajie spana tu kwa wapinzani Bungeni.
Tuendelee kumuombea na kumuunga mkono kuhakikisha Mungu anamsaidia anaingia Bungeni hapo Mwakani,maana ni hazina kwa Taifa letu na mtu muhimu sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…