Ikulu mnaalika watu wenye heshima kijanja kisha mnawazodoa

Itamfaiidia nini Sasa kuupata ulimwengu wote huku akiicha nafsi yake iangamie na moto wa milele. Dini na siasa wapi na wapi. Hata yesu alisema huwezi kuwatumikia mabwana wawili
 
I'd like to differ, it was just a coincidence, hakuna nia ovu yoyote!.
Haikuwa coincidence kwasababu katika kutawala na siasa kila linalofanywa linaweza kuwa na 'connotation' katika public court of opinion.

Ni hatari sana kama vyombo vya dola havijui implication ya kufanya mambo hovyo.

Sidhani ni hovyo! ni makusudi ili kufunika mjadala wa Bandari ambao ukiuangalia una uovu. Mikataba iliyosainiwa siyo kinacholalamikiwa na kilichopelekwa Bungeni.
Hivi DAB alitumika kufunika uovu , watu wawe na lesser of two evils, DP vs DAB
Waandishi wa habari wanaitwa wakati wowote na hawahitaji kujua nini kinatokea, ni nature ya kazi yao.

Wageni kama akina Kitima walioitwa kwa kadi na si wito binafsi wanapaswa kujua wanaitiwa nini.

Kwavile suala zima lilikuwa ni uovu, wakatumiwa mwaliko tu kwa kisingizo watapata habari wakifika.

Well, Mrisho Mpoto kawapa taarifa rasmi hii hapa
''Wameacha kazi ya kuchunga kondoo wapo katika siasa na wapo hapa kubugia Pilau'' .
Au shughuli fulani mgeni rasmi ni Rais, hadi backdrops banners zimeandaliwa, unaambiwa ujio wa rais ni siri for security reasons. Hivyo Ikulu wako right kutoa mwaliko bila kusema ni mwaliko wa nini!.
Ukimwita mtu Ikulu unatarajia nini? Hakuna cha security, kilichofanyaika ni kuficha uovu.

Kilichojadilia si kile kilichokwenda Bungeni, wanajua hilo na wanajua hawawezi kuvunja ule mkataba wa awali.
Wameamua kuuza au kugawa Bandari za Tanganyika , tena walikuwepo wote !

Yes walikuwepo wote kwasababu suala la Bandari Wazanzibar wamesema si la Muungano sasa ilikuwaje:
Rais Mwinyi alikuwepo
Spika wa Baraza la Wawakilishi

Kitendo cha kuitwa na the highest authority hata bila kuambiwa unaitiwa nini, justifies wewe kuitika mwito huo!.
Mtu mwenye busara hauzi uhai au heshima yake bila tafakuri na Busara. Mungu ni mkuu lakini watu bado wana mhalifu seuse mwanadamu mwenye nyama! Yuko wapi aliyedhani anamiliki Tanzania na ana kila nguvu!
I'd like to differ, ukiitwa na a trusted source, the highest authority, huhitaji kutumia busara yoyote kujiuliza uende au usiede!, ni unakwenda fasta!.
Of course usipotumia busara yanakukuta ya Father Kitima wa TEC kuadhiriwa mbele ya kadamnasi.
Mpoto kasema , sasa kama ni yake au alitumwa hayo yametokea IKulu na ikulu lazima iwe responsible

JokaKuu
 
Kilichofanywa ni na wale wahuni ni aibu sasna kwa Ikulu!
Na hii tabia ya Ikulu kualika wahuni na vishoka ktk shughuli mbalimbali na kuwapa airtime inaonyesha namna ambavyo kuna tatizo kubwa ktk Uongozi wetu wa awamu ya 5 na sita.
Uongozi wa awamu ya 5 unahusikaje halo au unawashwa
 
Nae uroho wa ubwabwa wa ikulu umemponza, mtu umetoka kumzodoa juzi tu leo anakualika halafu bila kujiuliza we huyo kufuata ubwabwa.
Ni muhimu tuelewe kwamba katika kujadili mambo ya faida ya jamii na taifa kwa ujumla, hakuna kuzodoana bali ni maoni kinzani yenye lengo la kujenga na siyo kubomoa.
Tuyatazame mawazo ya wenzetu kwa upande chanya, tuyachakate, tuchanganye na yetu tupate zao bora kwa faida ya jamii zote na taifa kwa ujumla.
Kwa hali ilivyo sasa, makundi ya kijamii na kisiasa yanajenga uhasimu ambao unaweza kusababisha kutafuta ushindi kwa jambo lolote kwa njia za kihuni na hata za kijinga bila hoja zenye nguvu na ushawishi.
 
Ikulu inafanya uhuni mkubwa hivi.

Huo mchele waliosimangiwa ni kodi zetu.

Au upande wa pili huwa ni lazima wacheze ngoma kabla ya kula?

Hiyo ikulu hivi haina mwenyewe wa kuona waalikwa wako kwenye staha ?

Mialiko mingine achaneni nayo, Hii ni fedheha.

Walifanywa kama Yuda kwenye ile karamu ya Bwana. Aliitwa msaliti, hao watumishi wa Bwana waliitwa wasaliti na Mpoto kwa maagizo.

Sasa ni kipindi cha kufunga na kuomba tuone huyo msanii asovaa viatu ana nguvu gani.
 
Naona kama hii nchi imelaaniwa!
 
Nilishangaa kilichofanyika na sisi CCM tumeona ni sawa tu!

Hii nchi imeshagawanyika kidini, kiukabila nk na hata sisi CCM tumeshagawanyika.
 
Nilishangaa kilichofanyika na hao CCM wameona ni sawa tu!

Hii nchi imeshagawanyika kidini, kiukabila nk na hata sisi CCM tumeshagawanyika.
Nchi inauzwa kijanja kijanja, namlaumu mwendazake haya yote alisababisha yeye.

Mungu angamwacha tu amalize muhula wake ndo amchukue.

Kweli Mungu hapangiwi, lakini hapa alituingiza choo cha ukweni.
 
Nilishangaa kilichofanyika na sisi CCM tumeona ni sawa tu!

Hii nchi imeshagawanyika kidini, kiukabila nk na hata sisi CCM tumeshagawanyika.
Wangefanya ccm, yani kwenye chama, wala tusingeshangaa; lakini imefanya IKULU! Hicho ndicho mimi kinanishangaza na kuugusa moyo wangu. Yani Ikulu kabisa? Rais na Amiri Jeshi Mkuu anahusishwa kwenye mialiko ya kihuni!? Tena wanaoalikwa na Watumishi wa Mungu: Watiwa Mafuta wa Bwana!!
Siyo kualikwa kihuni tu, bali na kudhihakiwa na kudharirishwa juu!!
Hakika Mungu Aishie hataliacha hili lipite bila kuwakingia kifua watumishi wake.
 
Itamfaiidia nini Sasa kuupata ulimwengu wote huku akiicha nafsi yake iangamie na moto wa milele. Dini na siasa wapi na wapi. Hata yesu alisema huwezi kuwatumikia mabwana wawili
Kwani dini yenyewe sio siasa? Unatambua siasa ni nini hasa? Usiimbishwe kama kasuku!
 
Mkuu Nguruvi3 hapa umeonyesha ukongwe wako ndani ya JF. Hii ndio mijadala asilia ya Jamiiforums ilivyokuwa awali kabla haijapoteza mvuto kabla ya kuvamiwa na "wahuni" na kuwafanya wenye hekima mkae pembeni.
Tunapaswa kujitafakari tufanyeje ili JF ile iliyokuwa inahofiwa na Ikulu, Bungeni na serikalini kwa mawazo positive inarudi na huu uhuni uliojaa sasa hivi unaenda kwenye majukwaa yake husika.
 
Watu wenye akili hapa JF ni wawili tu, Nguruvi3 na Kitimoto

Cc. FaizaFoxy
 
Wanazuoni kama plato na galileo walikuwa tayari kufa kulinda heshima zao, sasa huyu alivyosikia state invitation havaa kanvu harakaharaka hatakama angekuta kuna harusi angefungisha ndoa
Mbio mbio akaenda,akajua kaheshimiwaaa.jamani,hivi hata kusema naumwa nashindwa ili asifike.makubwaaa
 
Walikimbilia ubwabwa wa bure wakakuta za uso zinawangojea.

Na vibandiko vyao vya rangi rangi, sura ziliwaparama.

Watu wengine wako kimya, wakijibu hujibu kwa vitendo tu.

Pale hata Mpoto asingesema lolote, kile kitendo tu cha kusaini mikataba lilikuwa ni makofi makali sana kwa wale wa rangi rangi.
 
Walimuita kijanja ili wamtumie yule zumbukuku kumzodoa yeye na wapingaji wengine wa vipengele vya mkataba
Mkuu tatizo sio mwaliko, tatizo ni kejeli ya mrisho mpoto,

wapo wana music wenye heshima kama mwanaFA na Vicky Kamata kwanini wasutumike kutumbuiza dhima za taifa? Ndio maana ujio wa obama cia walisimamia kila kitu hadi media caverage, hakyamungu kuna siku Fr Kitima atanenguliwa na zuchu mbele ya kadamnasi kama hatutachukua tahadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…