IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

..what is the point ya kumteua Dr.Bashiru kuwa balozi?

..mbona watangulizi kama Dunstan Omari, Joseph Namata, Dickson Nkembo, Timothy Apiyo, hawakuwa mabalozi?

Inawezekana ilikuwa necessary procedural maneuver ya kumuingiza kwanza kwenye civil service kabla ya kumteua kuwa Chief Secretary.

All in all, it’s none of our business; ubalozi wake una absolutely no impact on us as long as he’s Chief Secretary!
 
Kwangu mimi nataka niwaze tofauti na wengine kabisa. Misimamo ya Dr Bashir kuhusu suala la Rais kuongezewa muda wa kusalia madarakani ilikua wazi kama mtendaji mkuu wa chama, hili jambo la kutaka Rais aungezewe muda ni lazima lichokozwe na wanachama wenye, inavyoonekana kikwazo lingetokea kwa katibu mkuu ana misimamo yake.

Ili kumweka kando ni lazima ipatikane nafasi ya kazi nje ya siasa asihisike kabisa na jambo hili.Ubalozi ni stahili yake tena angekua ughaibuniii. Hakuna ajuaye kesho yake kifo kikamuondoa mzee wetu Dr Kijazi na Dr Bashiri kwa uaminifu wake kiti cha marehemu kimemfaa.

Sasa Dr Bashir yupo kwenye utumishi hatakua na nafasi tena kufanya mambo ya chama, Katibu mkuu mpya ni lazima apatikane na endane na matakwa ya wanachama au Makada wenye kiu ya kuona Mukulu ansongezewa muda. Kwa fikra zangu za mbali na ni kama mission is on to be completed.

Haya ni maoni na mawazo yangu binafsi lakini muda utaongea zaidi.
 
Hivi amesha achia ukatibu wa ccm? Kqma nado sheria inasemaje mtumishi wa umma kujihusisha na siasa?
 
Wishful thinking amongst the treasonous brethren. Walipanga Kijaziatakufa. Walipanga Nancy Pelosi hatauliwa. Walipanga Maalim ataishi milele. Na tundulissu walipanga atamkwaa Askofu Mwanani. What a drag, nauseating to be quite sure!
 
Most probably Bashiru ataishia kwenye ubalozi, hii ya katibu kiongozi ni zuga tu!

Maana hakukuwa na sababu zozote za kumteua kuwa balozi bila kuwa na nia ya kupangia kituo cha kazi cha ubalozi

Bashiru anapinga Jiwe kuendelea na uraisi baada ya muda wake kwa hiyo it seems jiwe alitaka amtoe kwenye chama aweke watakaokubali agenda yake ya kuongeza mihula
 
..asante.

..mimi nilikuwa naujua ukweli huo.

..lakini mchangiaji niliyekuwa namjibu nadhani alijua kuwa amekosea lakini akaendelea kung'ang'ania msimamo wake.
For sure I was ignorant of this; japo najua kuwa kuna mihimili, ila inapokuja kwenye institutions i.e governance being part it wasnt clear how it goes ...Na kweli sheria siyo cup of my tea...
 
Most probably Bashiru ataishia kwenye ubalozi, hii ya katibu kiongozi ni zuga tu!

Maana hakukuwa na sababu zozote za kumteua kuwa balozi bila kuwa na nia ya kupangia kituo cha kazi cha ubalozi

Bashiru anapinga Jiwe kuendelea na uraisi baada ya muda wake kwa hiyo it seems jiwe alitaka amtoe kwenye chama aweke watakaokubali agenda yake ya kuongeza mihula
Bashiru alikosea kukubali kuwa KM. Njiwa kuruka na kunguru! Haijatokea. Alisemwa kuwa mwanaCUF. Hilo badala ya kumnyima ukatibu mkuu ndilo likampatia.
Dikteta ni hatari kuliko maelezo. Anawajua sana wabaya wa dhamira yake. Ana njia kibao za kuwaondoa. Hitler alijua hawezi kutawala dunia Wayahudi wakiwa hai. Holocaust. Wajerumani aliishawadhibiti kisawasawa.
Warioba aliishadundwa. Mzee baba atajiondokea mwenyewe. Mvungi mapanga yaliishamuondoa. Kabudi alikuwa tayari nje ya jalala. Polepole karudi ujanani kimwonekano. Tundu katunduliwa licha ya kifo kugoma kumchukua. Hata hivyo anaishi ughaibuni.
Bashiru zao la Bana lililobadilika. Uchambuzi wao wa siasa za Tanzania kama hawajuani. Utafikiri ni Joshua na wale wengine. Akisimama ukumbi wa Nkrumah mwalimu wake Bana haingii. Ataharibu vijana. Chambo kikawekwa. Ndoano ikavua.
Uchafuzi wa mitaa Bashiru aliigiza kuzungumzia matokeo yake. Uchafuzi wa 2020 kama hakuwepo. Kama Mlowola kawa balozi. Huko ikulu kaenda ili atumbuliwe vizuri. Amuulize mtangulizi wa Kijazi(rip). Wake sio uteuzi ni utenguzi!
 
Acha upumbavu soma katiba.
View attachment 1713028
Tunaelekezwa kwenye katiba (soma kiambata) kua katibu mkuu kiongozi anatakiwa ateuliwe kutoka kwa maafisa waandamizi.
Chukua kamusi, soma tafsiri ya afisa mwandamizi, halafu jiulize, katibu mkuu CCM ni afisa mwandamizi?
Basi Kama wwe unaona Raisi kavunja Katiba,kwa Nini usimshitaki Mahakamani!?
 
Bashiru ameondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu, kama alivyoondolewa Nchimbi kwenye nafasi za Chama, kwa sababu ni kikwazo.

Bashiru pamoja na kuwa kwenye zizi la waovu, dhamira yake imeendelea kumshtaki, na mara kadhaa ameonekana ni mtu ambaye angependa katiba ifuatwe japo hana uwezo wa kulazimishwa.

Alichopewa siyo promotion bali kuondolewa kwenye chama.
Na yeye amesma kuwa jakuwa consulted kupewa hiyo nafasi. Ili lengo la Rais Magufuli litimie, subirisheni aina ya mtu atakayeteuliwa kuwa KM wa CCM.

Amefanikiwa kuondoa vizingiti vya nje (vyama vya upinzani) vya kumzuia kuongeza muda, sasa anahangaika na kuondoa vizingiti vua ndani.
 
Dr. Bashiru anaandaliwa kuwa Rais ajae. Ameteuliwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu kiongozi ili;

1) Awe karibu na serikali ili ajue inavyoendeshwa.

2) CV yake ikamilike kwamba aliwahi kuwa na post serikalini kama kiongozi wa Makatibu Wakuu.

3) Aanze kuwa karibu na Boss, ili ajue mienendo na matakwa ya Boss, hata kama akikalia kiti cha Urais basi asivuke mipaka ya Boss aliemuweka pale (Boss anasahau kwamba hata yeye alivokalia kiti kile, alimsahau na kumgeuka aliemteua).

4) Kuonyeshwa kwamba Boss anamuamini sana, hivo afanye juu chini katika njia yake ya Siasa kumkumbuka Mtakatifu Boss na asivunje uaminifu kwa Boss.

5) Ajue kwamba u-Communist ndani ya damu yake ndio uatakao mpa Urais wa nchi hii, ila amepewa nafasi ile aweze kubalance U-communist na U-socialist katika kuendesha taifa (Nchi hii ni ya Kikomunist nyuma ya pazia).

#Wana CCM wanaosaka Urais (Dr. Mwigulu & Co LTD) kwa nguvu sasa wapate akili na waache kuusaka Urais, Rais ajae ndio Dr. Bashiru Ally Kakurwa.
 
Back
Top Bottom