Nimejiuliza sababu ya ubalozi mpaka sasa sijaelewa, au labda wanataka akienda nje kufanya deals awe na "Diplomatic immunity".
Kwema Mkuu?
Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma, Rais ni mamlaka ya nidhamu ya Katibu Mkuu Kiongozi.
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa sheria hiyo pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi ni mamlaka ya nidhamu kwa makatibu wakuu wa wizara, manaibu katibu wakuu, wakuu wa idara zinazojitegemea, katibu wa bunge, makatibu tawala wa mikoa, mkurugenzi wa uhamiaji, mabalozi, n.k.
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi anaweza kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote niliyemtaja hapo juu kwa kadri atakavyoona inafaa. Mtumishi au mamlaka yoyote isiyoridhika na uamumzi wa Katibu Mkuu Kiongozi inaweza kukata rufaa kwa Rais.
Naona kama Rais kamteua Dkt Bashiru kuwa Balozi ili kuepusha insubordination. Labda bila kuwa balozi, Bashiru asingeweza kumchukulia hatua balozi yoyote kwa kadri anavyoona inafaa. Other than this sioni sababu nyingine ya msingi. Historia inaonyesha kuwa waliowahi kushikilia nafasi hiyo walikuwa mabalozi pia possibly for the very same reason.
Swali linakuja: kati ya Katibu Mkuu Kiongozi (ambaye pia ni Cabinet Secretary) na Balozi who is the most powerful? Mie nilidhani Katibu Mkuu Kiongozi ndiye kinara wao lakini kwa appointment ya leo inaonyesha wazi kuwa hana lolote kwa balozi unless nae awe balozi. Hii inachanganya ukiangalia jinsi appointments za mabalozi zinavyofanyika siku hizi.