Kazi kubwa ya katibu mkuu( General Secretary) wa CCM, ni kuwa msimamizi mkuu wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kupitia nafasi yake kama mwenyekiti wa sekretarieti ya CCM
Kwa sasa chama cha mapinduzi ( CCM) ndio kinaongoza serikali, baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliopita
Baada ya watanzania wengi kuridhishwa na ilani ya uchaguzi ya CCM( 2020- 2025), watanzania waliamua kuipa kura CCM
Sasa baada ya uchaguzi, ilani ya CCM( chama kilichoshinda uchaguzi) ya miaka 5, upelekwa bungeni na kuwa mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka 5( mpango wa taifa wa maendeleo utengenezwa kutokana na ilani ya chama kilichoshinda uchaguzi mkuu)
Sasa katibu mkuu kiongozi( Chief Secretary) kwa nafasi yake kama mkuu wa utumishi wa umma kwa niabaya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, yeye ndie msimamizi mkuu wa watumishi wote wa umma, ambao utekekeza majukumu yao kulingana na mpango wa maendeleo wa taifa unavyoelekeza
Sasa kwa mheshimiwa Rais kumteua katibu mkuu wa chama tawala, ambaye ndie alikuwa msimamizi mkuu wa ilani ya chama tawala, ambayo kimsingi ndio mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka 5( 2020-2025), kwenda kuwa katibu mkuu kiongozi ( Chief Secretary) na kuwa mkuu wa watumishi wote wa umma, ambao watakuwa wanatekeleza mpango wa maendeleo wa taifa,
B³inafsi naona ni jambo sahihi kabisa kwa sababu Dr Bashiru Ally atakuwa anaujua upasavyo mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5, ambao umetokana na ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo yeye ndio alikuwa msimamizi mkuu wa ilani hiyo