IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Jiwe anataka kudistabilize system ili afanye lolote atakalo maana system itakua vulnerable.
Miiko na taratibu zinavunjwa makusudi hakuna wa kuhoji. Anateua watu wasio na taaluma husiki kushika nafasi nyeti ili awe na nguvu ya kuamua kila kitu
Kabisa, mimi mwanzo nilifikiri anafanya hivyo kwa ushamba, ujinga, kutojua.Nikaja kuona kuwa huu ni mkakati mahususi.
 
You are missing the context with regards to El Chapo.
I don’t see what I’m missing!

El Chapo is a criminal. Bashiru as far as I know, is not.
Nimekuuliza hivi, kwa kuwa hakuna mtu ambaye anakubalika na watu wote, basi ni sawa Rais amteue El Chapo, muuza madawa ya kulevya, raia wa Mexico, mfungwa aliye gerezani Marekani?

Nimemchagua El Chapo kama mfano to make a very specific point hapa.

Please do not miss the point.
El Chapo ndo umemwona hawezi kukubalika na wote?
 
..nadhani watu wanashangaa kwamba Raisi amekwenda kinyume na utamaduni wa kuteua ma-chief secretary.

..kilichotokea naweza kukifananisha na mtu is not an academic halafu ateuliwe kuwa VC ktk chuo kikuu.

..iliwahi kutokea huko nyuma lakini kwa muda mrefu ma-VC wamekuwa na watu waliolelewa kama wahadhiri ktk vyuo vikuu.
Ok, so there is no big deal then....or is there?
 
Katibu mkuu kiongozi ndo sawa na White House Chief of Staff?

Kama ni sawa, tatizo liko wapi endapo Rais aliyepo madarakani atamteua mtu kutoka kwenye chama chake?

You would think wako sawa, lakini kuna tofauti kubwa. Chief Secretary ni mkuu wa civil service (kwa upana wake wote). Unlike WH Chief of Staff, kazi ya Chief Secretary haiishi automatically pindi Rais aliyemteua anapomaliza muda wake. WH Chief of Staff almost ni kama msaidizi mkuu binafsi wa POTUS.
 
Hongera sana Dr. Bashiru kwa majukumu hayo mapya.
 
I don’t see what I’m missing!

El Chapo is a criminal. Bashiru as far as I know, is not.

El Chapo ndo umemwona hawezi kukubalika na wote?
Wewe unamkubali El Chapo kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Tanzania?

Mara paaap, El Chapo kapewa diplomatic immunity ya ubalozi wa Tanzania!
Si kazi ya kuuza sembe hiyo.
 
Nafasi yoyote ya chama cha kisiasa ni nafasi ya kisiasa by definition. Hata nafasi ya utendaji ndani ya chama ni nafasi ya utendaji katika muktadha wa kisiasa.

Maana yake, Katibu Mkuu wa Chama atakuwa mtendaji katika kueneza itikadi ya Chama, hivyo hiyo ni nafasi ya kisiasa.

Katibu Mkuu Kiongozi ni mtu anayeongoza watumishi wa umma ambao hawana open affiliation na chama chochote.Na yeye anaongoza kwa maadili ya utumishi wa umma yanayokataza ushabiki wa vyama.

Sasa Bashiru aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM aende kuongoza utumishi wa umma na kukataza ushabiki wa vyama?

Kumfanya Katibu Mkuu wa CCM kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ni kama kumfanya Kocha wa Yanga ajiuzulu ukocha wa Yanga, halafu aende kuwa refa katika mechi ya Simba na Yanga!

Kazi kubwa ya katibu mkuu( General Secretary) wa CCM, ni kuwa msimamizi mkuu wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kupitia nafasi yake kama mwenyekiti wa sekretarieti ya CCM

Kwa sasa chama cha mapinduzi ( CCM) ndio kinaongoza serikali, baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliopita

Baada ya watanzania wengi kuridhishwa na ilani ya uchaguzi ya CCM( 2020- 2025), watanzania waliamua kuipa kura CCM

Sasa baada ya uchaguzi, ilani ya CCM( chama kilichoshinda uchaguzi) ya miaka 5, upelekwa bungeni na kuwa mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka 5( mpango wa taifa wa maendeleo utengenezwa kutokana na ilani ya chama kilichoshinda uchaguzi mkuu)

Sasa katibu mkuu kiongozi( Chief Secretary) kwa nafasi yake kama mkuu wa utumishi wa umma kwa niabaya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, yeye ndie msimamizi mkuu wa watumishi wote wa umma, ambao utekekeza majukumu yao kulingana na mpango wa maendeleo wa taifa unavyoelekeza

Sasa kwa mheshimiwa Rais kumteua katibu mkuu wa chama tawala, ambaye ndie alikuwa msimamizi mkuu wa ilani ya chama tawala, ambayo kimsingi ndio mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka 5( 2020-2025), kwenda kuwa katibu mkuu kiongozi ( Chief Secretary) na kuwa mkuu wa watumishi wote wa umma, ambao watakuwa wanatekeleza mpango wa maendeleo wa taifa,

B³inafsi naona ni jambo sahihi kabisa kwa sababu Dr Bashiru Ally atakuwa anaujua upasavyo mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5, ambao umetokana na ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo yeye ndio alikuwa msimamizi mkuu wa ilani hiyo
 
Hivi hakuna watanzania wengine wenye sifa ya kushika hiyo post?

Naona Magu anacheza na hao hao makada waaminifu wa CCM!

Mara kampa ubunge Polepole, wakati akiendelea kushika nafasi yake ya ukatibu mwenezi wa CCM!

Hii nchi kweli yule aliyenacho huongezewa na yule ambaye hana, hata kile kidogo atapokonywa!
Kama Mtanzania yupi ambaye unaona anafaa? Mtaje tumuone tafadhali
 
Back
Top Bottom