Katibu Mkuu Kiongozi ndio Bosi wa Watumishi wa Umma wote Tanzania
Ni promotion au demotion?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni promotion au demotion?
We ulitaka ateuliwe nani?Mkuu hivi vitu vina traditions. Na ndio maana hata Marekani na uliberali wao wote, kuna baadhi ya mambo walikuwa wanamshangaa Trump kufanya...
Usistuke, Katibu Mkuu Kiongozi akiwa mgombea Urais wa ccm 2025Katibu mkuu wa CCM ndo katibu mkuu Kiongozi.
Mwenyekiti wa CCM ndo amiri jeshi mkuu wa nchi.
Amini nakwambia, nchi hii ni ya vyama vingi
Kwani nimesema kuna mtu anayekubaliwa na wote?Sawa.
Nitajie mtu mmoja ambaye angeteuliwa na Rais Magufuli kuwa katibu mkuu kiongozi mpya ambaye wewe ungemkubali na ambaye angekubaliwa na wanaJF wote na wananchi wote kwa ujumla.
Akishateuliwa Balozi anapatiwa Diplomatic Passport ili katika misele yake ya Ng'ambo apite expressway...bila hivyo he doesn't qualify to hold one.
Kwa hiyo anakuwa Katibu Mkuu wa Chama na Katibu Mkuu Kiongozi kwa wakati mmoja au anaacha kuwa katibu mkuu wa CCM?
Vipi kuhusu muongozo wa utumishi serikalini unaotenganisha mambo ya chama na utumishi wa umma serikalini?
Hata kama atajiuzulu Ukatibu Mkuu CCM, huu uteuzi unaonesha kwamba utumishi serikalini unaenda kupelekwa kichama chama zaidi.
Hapana, sio sawa. Kulingana na website yake, Chief Secretary ni Kiongozi Mkuu wa Civil Service yote ( zamani ajira zote za watumishi wa umma wa kudumu zilikuwa chini yake) na anasimamia utendaji wa TISS na PCCB. Aidha, ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, yeye ndie Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mawaziri. Ni zaidi ya Chief of Staff wa White House. Kwetu sisi Chief of Staff ni kama Private Secretary to the President.Katibu mkuu kiongozi ndo sawa na White House Chief of Staff?
Kama ni sawa, tatizo liko wapi endapo Rais aliyepo madarakani atamteua mtu kutoka kwenye chama chake?
Humphrey anaweza kupata ukatibu
El Chapo ni muuza madawa ya kulevya.Kwani nimesema kuna mtu anayekubaliwa na wote?
Angemchagua El Chapo kuwa KATIBU mKUU Kiongozi, halafu watu wakalalamika, ungesema uteuzi wa El Chapo ni sahihi kwa sababu hakuna mtu ambaye atakubalika na wote?
Mpeni pole kwani huko anakokwenda atakayokutana nayo ni ya kuhuzunisha muda si mrefu!!!Kongole kwa katibu mkuu kiongozi balozi yake😂🙏!
Mara nyingi watu huwa wanaitwa kwa vyeo vyao vikubwa walivyofikia.Japo Mkapa alikuwa balozi lkn sijawahi kusikia mtu akimwita balozi sijui kwa nini
Hongera kwa Bashiru...Hapana, sio sawa. Kulingana na website yake, Chief Secretary ni Kiongozi Mkuu wa Civil Service yote ( zamani ajira zote za watumishi wa umma wa kudumu zilikuwa chini yake) na anasimamia utendaji wa TISS na PCCB. Aidha, ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, yeye ndie Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mawaziri. Ni zaidi ya Chief of Staff wa White House. Kwetu sisi Chief of Staff ni kama Private Secretary to the President.
Amandla...
Au dini ileee?, kuna watu hadi mnakufa ubongo wenu utakuwa umetumika 0.001% ya uwezo wake!Kanda ya ziwa oyee
Bashiru anajua figisu, anajua kubadilisha maneno halafu anajua kuusoma mchezo kwenda na bosi wake. Hivyo sitegemei apate shida sana.Mpeni pole kwani huko anakokwenda atakayokutana nayo ni ya kuhuzunisha muda si mrefu!!!
Hata mimi zamani nilifikiri hajui, si kwamba hajui, hajali na anapanga mkakati wake bila kufuata miongozo...hapo amemsokomeza Dr.Bashiru kuwa civil servant na foreign service office kwa wakati mmoja.
..Magufuli amekaa serikalini muda mrefu lakini inaelekea hajui jinsi civil service inavyoongozwa na miiko yake.
..Ndio maana tulikuwa tunashuhudia wanajeshi wanateuliwa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali.
Tumelikoroga, sasa tulinywe tu.Unakumbuka ziara alizokuwa akizifanya kukagua miradi ya serikali na maagizo aliyokuwa akiyatoa kwa wakandarasi na mawaziri? .. sasa amekuwa km kiongozi.. yetu macho