IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Kuna kipindi nilikuwa nafikiri Magufuli anaharibu mambo kwa ushamba tu, kwa ujinga, kwa kutojua, kwa ubishi, na kwa kutosikiliza watu..
Hapo amemsokomeza Dr.Bashiru kuwa civil servant na foreign service office kwa wakati mmoja.

Magufuli amekaa serikalini muda mrefu lakini inaelekea hajui jinsi civil service inavyoongozwa na miiko yake.

Ndio maana tulikuwa tunashuhudia wanajeshi wanateuliwa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali.
 
Jf ya siku hizi ina vilaza sana. Balozi Kijazi alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Balozi Sefue alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Vipi kuhusu Balozi Mahiga alipokuwa waziri alikuwa balozi wa nchi gani pia?
Ninadhani wale walihudumu kwenye ubalozi kabla ya kuwepo katika hizo nafasi,kwa hiyo walitoka na vyeo hivi huko walikokuwa.Nisahihishe
 
Maswali yangu ya msingi kuhusu hadhari ya kuchanganya siasa na utumishi wa umma bado yapo pale pale.
Unakumbuka ziara alizokuwa akizifanya kukagua miradi ya serikali na maagizo aliyokuwa akiyatoa kwa wakandarasi na mawaziri? .. sasa amekuwa km kiongozi.. yetu macho
 
Kama ilikuwa hivyo, hakujawahi kuwapo na rais aliyefanya hilo kwa wazi kabisa kwa ngazi ya kumteua Katibu Mkuu wa Chama kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hii ndiyo mara ya kwanza mnaambiwa wazi kabisa kwamba "utumishi wa umma unaenda kuongozwa na kada wa juu kabisa wa chama sasa"
Duh! Najua unajua, ila unataka kujua zaidi.

Hakuna wa kumfananisha na "jiwe" nchi hii, yeye yuko kivyake vyake ilimradi tu aweze kuandika historia mpya
Na ndiyo maana kaanzisha somo la historia ili naye pia aandikwe katika vitabu kama wakina chief Mkwawa, Mirambo n.k.
Lol! Yajayo yanafurahisha.
 
Jf ya siku hizi ina vilaza sana. Balozi Kijazi alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Balozi Sefue alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Vipi kuhusu Balozi Mahiga alipokuwa waziri alikuwa balozi wa nchi gani pia?
Wewe ni mpumbavu kweli, Halafu unaita watu vilaza.
Soma ulichokiandika hapo halafu rejea hao uliowataja hapo ni kipindi gani walikuwa mabalozi na ni kipindi gani walikuwa na majukumu mengine ya kitaifa.

Huu ubalozi wa Bashiru hauna unafanano wowote na hao uliowataja.

Kijazi, Sefue, Mahiga wote washaiwakilisha Tanzania kweli balozi tofauti.. Huyu Bashiru ni nchi gani ataiwakilisha kama balozi na wakati huo huo ni CS?
 
Excellent, Excellent ... Safiiiiiiii...!!! 👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏💚💚💚💚💚💛💛💛💛💛💛🔰✅🗽
 
Kwa hiyo anakuwa Katibu Mkuu wa Chama na Katibu Mkuu Kiongozi kwa wakati mmoja au anaacha kuwa katibu mkuu wa CCM?

Vipi kuhusu muongozo wa utumishi serikalini unaotenganisha mambo ya chama na utumishi wa umma serikalini?

Hata kama atajiuzulu Ukatibu Mkuu CCM, huu uteuzi unaonesha kwamba utumishi serikalini unaenda kupelekwa kichama chama zaidi.
Ulitaka katibu mkuu kiongozi awe salum mwalimu?
 
Katibu Mkuu Kiongozi na wakati huo huo Balozi? Kivipi? Ataiwakilisha nchi kwenye nchi gani? Mbona kuna utata hapa? Tafadhali fafanulieni kabla wananchi hawajahoji!!!

..Balozi ni ngazi ya juu kabisa ya watumishi wa wizara ya mambo ya nje.

..sasa wapo mabalozi ambao huwa wanakuwa makao makuu ya wizara ya mambo ya nje, na wapo mabalozi ambao wanatuwakilisha nje ya nchi.

..mara nyingi wakuu wote wa idara za makao makuu ya wizara ya mambo ya nje huwa ni maofisa wa ngazi ya balozi.

..kwa mfano, mkuu wa itifaki, mkuu wa idara ya asia na afrika, etc etc huwa ni maafisa[foreign service officers] wa wizara ya mambo ya nje waliofikia ngazi ya balozi.

..pia wakati mwingine Raisi huteuwa mabalozi toka nje ya wizara ya mambo ya nje, yaani nje ya foreign service officers. Mfano wa mabalozi hao ni Balozi Chief Lukumbuzya, Balozi Chief Erasto Mang'enya, Balozi Paul Bomani, Balozi Amir Jamal, Balozi Omar Mapuri, Balozi Wilson Masilingi, na wengine.



cc sengobad, Naipendatz, UncleBen
 
Humphrey anaweza kupata ukatibu
Hivi huwezi kuwa Chief Secretary bila kuwa balozi? alafu I'm thinking out loud ..... Pale lumumba iyo nafasi atapewa nani obviously lazima ajiuzulu ukatibu wa CCM.
 
Kumbuka huyo alikataa hata kuitwa Mtukufu, vile vile alikataa sura yake kuwekwa kwenye Sarafu ama noti...
Vilevile alikataa habari zake sio lazima ziwe za kwanza kusomwa kwa tv/ radio
 
Hata Rais Biden anafanya u chama.

Kateua watu wa chama chake kwenye serikali yake.

Na ikitokea nafasi ya ujaji kwenye mahakama kuu akiwa bado ni Rais, atateua jaji mwenye itikadi kama yake.

Hakuna cha ajabu wala kibaya alichokifanya Magufuli hapo.

Mkuu hivi vitu vina traditions. Na ndio maana hata Marekani na uliberali wao wote, kuna baadhi ya mambo walikuwa wanamshangaa Trump kufanya.

Shida ya urais karibu dunia nzima, inategemea sana busara na kujiheshimu, mambo mengi ni unwritten.

Bashiru ataweza kufanya kazi, kama ameweza CCM hatashindwa, lakini inawaambia nini Civil Servants? Kwamba hakuna hata mmoja wao aliyeonekana anafaa? Huyu jamaa juzi tu katoka kusema "CCM inatumia dola kubaki madarakani". Leo anaenda kupewa madaraka makubwa ambayo yanasimamia pia vyombo vya dola, loyalty yake iko wapi Chama au Serikali?

Katika miaka ya hivi karibuni, this will be the most political CS ever
 
Back
Top Bottom