Kwenye sheria kuna msemo, justice must not only be done, it must also seem to be done.
Rais alikuwa na watu wengi sana wa kuwateua katika nafasi hii ya kiserikali isiyotakiwaa kuongozwa kisiasa, akachagua katibu mkuu wa chama chake ambaye ni mtu wa kisiasa.
Katibu Mku huyu ana historia tayari, historia mabayo hawezi kuikana na itamfuata tu huko kwenye civil servant.
Hivi Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ashatoa matamko kibao ya kishabiki kwa kuishabikia CCM leo akiwaambia wafanyakazi wa serikali, watumishi wa umma, wasiendekeze siasa sehemu za kazi atachukuliwa serious?
Hivi, watu wakisema Magufuli ana mkakati wa kuingiza siasa za vyama kwenye civil service, atakuwa na point za kujitetea?
Hivi, hakuna watu wengine ambao hawana historia ya chama ambao wangefaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi?
Umeongelea Katiba. Ukweli kwamba kitu hakikatazwi kikatiba haumaanishi kwamba kukifanya ni busara na jambo zuri.
Magufuli kama last custodian of the land hakatazwi kikatiba kuiuza nchi nzima iwe shamba la Emir of Qatar.
Hakuna sehemu ambapo katiba inamkataza kufanya hivyo.
Lakini je, kufanya hivyo itakuwa haki? Itakuwa sawa? Itakuwa busara?