IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Katibu mkuu kiongozi ndo sawa na White House Chief of Staff?

Kama ni sawa, tatizo liko wapi endapo Rais aliyepo madarakani atamteua mtu kutoka kwenye chama chake?
Hapana... Chief of Staff analingana na Katibu wa Ikulu hapa Tanzania. Chief Secretary US hawana, ipo sana Commonwealth countries. CS ni mkuu wa Civil Service, naamini itabidi aachie ukatibu CCM
 
Hapana... Chief of Staff analingana na Katibu wa Ikulu hapa Tanzania. Chief Secretary US hawana, ipo sana Commonwealth countries. CS ni mkuu wa Civil Service, naamini itabidi aachie ukatibu CCM
Shukran jazilan.
 
Kama ataachana na siasa kwa kuacha kuwa katibu mkuu wa CCM, nini mbaya?

Magufuli kakiuka katiba kwa kumteua?
Kwenye sheria kuna msemo, justice must not only be done, it must also seem to be done.

Rais alikuwa na watu wengi sana wa kuwateua katika nafasi hii ya kiserikali isiyotakiwaa kuongozwa kisiasa, akachagua katibu mkuu wa chama chake ambaye ni mtu wa kisiasa.

Katibu Mku huyu ana historia tayari, historia mabayo hawezi kuikana na itamfuata tu huko kwenye civil servant.

Hivi Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ashatoa matamko kibao ya kishabiki kwa kuishabikia CCM leo akiwaambia wafanyakazi wa serikali, watumishi wa umma, wasiendekeze siasa sehemu za kazi atachukuliwa serious?

Hivi, watu wakisema Magufuli ana mkakati wa kuingiza siasa za vyama kwenye civil service, atakuwa na point za kujitetea?

Hivi, hakuna watu wengine ambao hawana historia ya chama ambao wangefaa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi?

Umeongelea Katiba. Ukweli kwamba kitu hakikatazwi kikatiba haumaanishi kwamba kukifanya ni busara na jambo zuri.

Magufuli kama last custodian of the land hakatazwi kikatiba kuiuza nchi nzima iwe shamba la Emir of Qatar.

Hakuna sehemu ambapo katiba inamkataza kufanya hivyo.

Lakini je, kufanya hivyo itakuwa haki? Itakuwa sawa? Itakuwa busara?
 
Akimiliza au akiondolewa ukatibu mkuu ataendelea kuwa balozi.
Sijaelewa mantiki ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu na hapo hapo kuteuliwa kuwa balozi

Atatumikia kipi kati ya hivi viwili?
 
Hata Trump hakukiuka katiba kukataa matokeo ya uchaguzi na kusababisha uvamizi Capitol Hill Jan 6.
Kama ataachana na siasa kwa kuacha kuwa katibu mkuu wa CCM, nini mbaya?

Magufuli kakiuka katiba kwa kumteua?
 
Back
Top Bottom