IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Mkuu,

Unalalamika kwamba mimi nalalamika sana.

Lakini wewe unanizidi kulalamika.

Unalalamika kwamba nitalalamika kuhusu vitu ambavyo sijalalamikia bado!

Kama vile umekuwa time traveler uliyeenda katika alternate universe na kuona nalalamika halafu ukarudi hapa kutoa ripoti.

Stick to the facts please.
Sawa.

Nitajie mtu mmoja ambaye angeteuliwa na Rais Magufuli kuwa katibu mkuu kiongozi mpya ambaye wewe ungemkubali na ambaye angekubaliwa na wanaJF wote na wananchi wote kwa ujumla.
 
View attachment 1712543Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Katibu Mkuu Kiongozi)
Hivi hakuna watanzania wengine wenye sifa ya kushika hiyo post?

Naona Magu anacheza na hao hao makada waaminifu wa CCM!

Mara kampa ubunge Polepole, wakati akiendelea kushika nafasi yake ya ukatibu mwenezi wa CCM!

Hii nchi kweli yule aliyenacho huongezewa na yule ambaye hana, hata kile kidogo atapokonywa!
 
Hatimaye pengo limezibwa.
Hongera Balozi. Dr. Bashiru kwa uteuzi huo natumaini utamsaidia Mh. Rais kutrkeleza majumuku ya Katibu Mkuu Kiongozi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Uchama kila Rais amefanya ila huyu hana aibu hata kidogo. Ngoja tuone kama ataenda kuwa mtumishi wa mwanasiasa
Hata Rais Biden anafanya u chama.

Kateua watu wa chama chake kwenye serikali yake.

Na ikitokea nafasi ya ujaji kwenye mahakama kuu akiwa bado ni Rais, atateua jaji mwenye itikadi kama yake.

Hakuna cha ajabu wala kibaya alichokifanya Magufuli hapo.
 
Akimiliza au akiondolewa ukatibu mkuu ataendelea kuwa balozi.
Amechaguliwa kuwa balozi na katibu mkuu respectively

anatumikia kipi hapo sasa hivi??

Kama atakuwa balozi akiondolewa kwenye ukatibu mkuu ni kwanini akapewa ubalozi sasa hivi? Si angesubiri akishamuondoa kwenye ukatibu mkuu ndio amteue balozi?.
 
Katibu mkuu kiongozi ndo sawa na White House Chief of Staff?

Yeep

Mara nyingi vyeo vya namna hii ni lazima na muhimu kwa Rais kumpa mtu ambaye ni swahiba na mwanausalama...

Hawa makatibu wakuu wa marais huwa wanajua siri nyingi sana za nchi...

Hivyo watu waache kulalama
 
Hivi huwezi kuwa Chief Secretary bila kuwa balozi? alafu I'm thinking out loud ..... Pale lumumba iyo nafasi atapewa nani obviously lazima ajiuzulu ukatibu wa CCM.

..unaweza kuwa chief secretary bila kuwa balozi.

..kwa mfano, Joseph Namata, Dickson Nkembo, na Timoty Apiyo, walikuwa chief secretary bila kuwa mabalozi.
 
Hivi hakuna watanzania wengine wenye sifa ya kushika hiyo post?

Naona Magu anacheza na hao hao makada waaminifu wa CCM!

Mara kampa ubunge Polepole, wakati akiendelea kushika nafasi yake ya ukatibu mwenezi wa CCM!

Hii nchi kweli yule aliyenacho huongezewa na yule ambaye hana, hata kile kidogo atapokonywa!
Wewe ungependa ateuliwe nani?
 
Katibu Mkuu Kiongozi na wakati huo huo Balozi? Kivipi? Ataiwakilisha nchi kwenye nchi gani? Mbona kuna utata hapa? Tafadhali fafanulieni kabla wananchi hawajahoji!!!
Jf ya siku hizi ina vilaza sana. Balozi Kijazi alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Balozi Sefue alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Vipi kuhusu Balozi Mahiga alipokuwa waziri alikuwa balozi wa nchi gani pia?
 
Ubalozi wa Tanzania siku hizi umeshuka thamani sana, usishangae hata Msigwa akateuliwa Balozi.

Si kama ule wa enzi za Balozi Magombe, Balozi Mbapila, Balozi Mahiga, Balozi Nyang'anyi, Balozi Malecela, Balozi Mwinyi, Balozi Mkapa.

Nimejiuliza sababu ya ubalozi mpaka sasa sijaelewa, au labda wanataka akienda nje kufanya deals awe na "Diplomatic immunity".
Japo Mkapa alikuwa balozi lkn sijawahi kusikia mtu akimwita balozi sijui kwa nini
 
Jf ya siku hizi ina vilaza sana. Balozi Kijazi alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Balozi Sefue alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Vipi kuhusu Balozi Mahiga alipokuwa waziri alikuwa balozi wa nchi gani pia?
Sefue alikua balozi USA kabla ya kua katibu mkuu....kasome wasifu wake kabla ya kuleta undezi wako hadharani
 
Jf ya siku hizi ina vilaza sana. Balozi Kijazi alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Balozi Sefue alipokuwa KM alikuwa balozi wa nchi gani? Vipi kuhusu Balozi Mahiga alipokuwa waziri alikuwa balozi wa nchi gani pia?
Before walikuwa balozi ndio maana wanaitwa hivyo hata waliostaafu wanaitwa balozi....
 
Back
Top Bottom