IKULU: Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji

IKULU: Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji

Tabia za kutoa watu "kafara" ili kutafuta kiki za kisiasa siyo nzuri.

Mkuu wa nchi kukagua vyoo sokoni is too low, hata kwa waziri wa TAMISEMI bado ndogo kwake

Magufuli anataka kutafuta kura kupitia kiki za kujifanya muwajibishaji

Ni kitu kibaya sana hicho!
Ulisikiliza mwenyewe au umesoma sehemu? Aliyesikiliza kaelewa
 
Wivu unapata faida gani akitenguliwa,wananchi wana majungu sana
Hapana si majungu.
Kwa mtu mwenye akili ya kawaida ukisikiliza zile kero na utetezi wake unajua kuna shida kaika uongozi wa wilaya.
Yeye hana gari, gari za wagonjwa mbovu, maji hakuna na maelezo si mazuri.... the list goes on.
 
Itakuwa ni sababu ya yule mtoto wa shule ya msingi Somanga kuchoma utambi kuwa shule yao ni mbovu nini,huyu Mkuu wa Wilaya aliyetumbuliwa tulikuwa nae chuo kabla hajakuwa mbunge,maneno na porojo nyingi ingawa mwenzetu alitoboa mapema kutoka afisa ugani wa `kilimo ,akaenda uboharia, ubunge ,uDC
 
Aliyestahili kufukuzwa ni yule aliyeshindwa kuwajengea wananchi Choo. Huwezi kuendesha soko bila Choo... No wonder cholera haiishagi Bongo.
 
Dah Magufuli mkatili, kamwambie achape kazi. Akamtumbua.

Ila jamaa naye mweupe sana ingawa anajiamini.
 
Mngejua ilivyoshida kupata pesa za kumfanyia service msingekua mnasema......

Wakurugenzi wanatumia hadi pesa zao hii serikali ya kishetani ipo kwa ajili ya kukomoa watendaji wake.

We nani hataki gari itembee na kufanya shughuli zinazotakiwa kufanywa.....

Hii ni serikali ya kukomoana na ukiangalia ujio wa Lissu umempa sn presha sasa ukiunganisha ma mawe ya Kikwete jana Basi anajaribu kuhamisha mjadala lkn haiwezekani........

NI MIHASIRA TU YA HOVYO
Nimefika utete yalipo makao makuu ya wilaya ya rufiji ..kwanza ofc za mkuu wa wilaya ni za kizamani na zimechoka kwelikweli , barabara zote za wilaya ni mbovu hatari ..gari ya mkurugenzi wa wilaya choka mbaya hivyo hvyo na mkuu wa wilaya pia..Rufiji iko hovyo hovyo kbsaa ..ukiingia kuanzia mwaseni kuja ndundunyimikanza hadi ngorongo uje mpk mkongo ni shida tupu ..yaani kiukweli ni wilaya masikini mnooo mnoo ...mkuu was wilaya Juma Njwayo ni mmakonde wa Tandaimba alinisumbua sana sana wkt nafanya shughuri za kichama kwenye hiyo wilaya acha apumzishwe tu japo sio vzr kufurahia matatizo ya mwenzio ...
 
Hiyo Wilaya magari yote mabovu, Mkuu wa Wilaya hana gari, Mkurugenzi Hana gari, DAs hana hana gari.

Sijui kosa la nani hapo.
Kwa sababu hao wote wapo UPINZANI tu, wangekuwa chama chetu wangepewa kitambo sanaaa
 
Mkuu hio video umeweka hapo ,mbona huyo nimkuu wa wilaya ya kibiti nasi Rufiji?. Au Rufiji ndio wilaya ya kibiti?. Na huyo mkuu wa wilaya ya kibiti anaonekana kwenye video anaitwa GULAM HUSSEIN SHABAN KIFU, alikua mbunge 2000/2005 jimbo la Kigoma kusini kupitia NCCR MAGEUZI hata diploma hana huyo jamaa.@Moderator JamiiForums wekeni taarifa sawa huyu jamaa anapotosha , video haiendani na utenguzi.
Upo sawa mkuu.Mtoa mada amechanganya taarifa.
 
Unakusanya 1.8Billion+pesa za miradi unashindwa kufanya maintenance ya magari?
1.8bn hiyohiyo itengeneze magari, hiyohiyo ijenge madarasa, hiyohiyo ijenge stendi, hiyohiyo ijenge vyoo vya shule na masoko, hiyohiyo ilipe posho za mwezi na za vikao za madiwani,hiyohiyo ijenge kiwanda...

Hela hiyo ni ndogo, sema ndio hivyo siku ya kufa nyani...
 
Acha kuposha uma jeneza la Mkapa lilibebwa na Generals hasa Brigedia Generals hukuona vile vidude vyekundu kwenye Kola?
Ulivyobisha kwa confidence kama unajua vile...kuanzia cheo cha kanali huanza kuvaa vijogoo na waliobeba walikuwa ni makanali ila Brigadier Generals walikuwa pembeni yao wakisindikiza
 
Back
Top Bottom