IKULU: Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji

IKULU: Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji

Pamoja na mapungufu yake mh Raisi John Joseph Pombe Maghufuli , nimekua ni shabiki mkubwa sana wa Maghufuli , nampenda vibaya mno kutoka moyoni kama nimemzaa
Unatafuta uteuzi
 
Tabia za kutoa watu "kafara" ili kutafuta kiki za kisiasa siyo nzuri.

Mkuu wa nchi kukagua vyoo sokoni is too low, hata kwa waziri wa TAMISEMI bado ndogo kwake

Magufuli anataka kutafuta kura kupitia kiki za kujifanya muwajibishaji

Ni kitu kibaya sana hicho!
Kwani yeye ndio alikuwa anawapangia wananchi maswali ya kuuliza?
 
Mkuu hio video umeweka hapo ,mbona huyo nimkuu wa wilaya ya kibiti nasi Rufiji?. Au Rufiji ndio wilaya ya kibiti?. Na huyo mkuu wa wilaya ya kibiti anaonekana kwenye video anaitwa GULAM HUSSEIN SHABAN KIFU, alikua mbunge 2000/2005 jimbo la Kigoma kusini kupitia NCCR MAGEUZI hata diploma hana huyo jamaa.@Moderator JamiiForums wekeni taarifa sawa huyu jamaa anapotosha , video haiendani na utenguzi.
Dah sisi wenye imani ya kweli kwenye kutumbuliwa na hizi teuzi tunaonewa. Inabidi tuandamane
 
Ujinga wake. Choo cha soko mpaka mhe rais akisemee? Sio sawa.
kweli mzee anafanya vizuri kutengua wale wasiotimiza wajibu wao ila pia waweza kuta watenguliwa wakawa wanashukuru kutengeliwa pia maana kazi za kuteuliwa zimekua ngum sana hata binafsi najua siwezi pata uteuzi ila ikitokea nakataa na kuomba mzee amteue mwingine ,
 
Ujinga wake. Choo cha soko mpaka mhe rais akisemee? Sio sawa.
Hivikwenye ToRs za DC kuna hilo la kujenga vyoo au stand za mabasi? DC ana bajeti ya kutekeleza hayo? Pengine tukubali tu kuwa Rais aliona si busara kubaki na mteule wake ambaye alikuwa amekwisha kumdhalilisha hadharani. Kisha akatengua uteuzi. Pu!
 
Mtela aliyekua DAS kisarawe ni muislam?. Yule DAS mpya alieteuliwa kisarawe ni mkristo?. Mkuu hoja ya Udini ni mfu sana kwenye teua tengua za mhe rais. Achana nayo.
mkuu pia sisi ni waTanzania acheni kutunyanyapaa. Mifano uliyotoa ni michache mno. Tunataka uwiano
 
mkuu pia sisi ni waTanzania acheni kutunyanyapaa. Mifano uliyotoa ni michache mno. Tunataka uwiano
Kama una taarifa yoyote ya Ikulu yenye teuzi au tengua kwa dini moja, kabila moja au ukanda mmoja, naomba unitumie hapa. Hii kuongea vitu ambavyo kiuhalisia havipo, sio sawa mkuu. Nchi ni yetu wote.
 
Kama una taarifa yoyote ya Ikulu yenye teuzi au tengua kwa dini moja, kabila moja au ukanda mmoja, naomba unitumie hapa. Hii kuongea vitu ambavyo kiuhalisia havipo, sio sawa mkuu. Nchi ni yetu wote.
Mkuu heshima kwako. Kusema tu ukweli kabisa hii nchi siyo yetu wote. Kubali kataa
 
Back
Top Bottom