Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 5,319
- 10,416
Hii miradi bila kujipanga matokeo yake ndio haya sasa tunakamuliwa kodi kwenywe kila kitu.
Miradi mpaka ikamilike, wabongo mtakuwa hohehahe huku uchumi ukiwa taabani(mtakuwa kama waethiopia)
Msisahau zoezi la kujenga mji wa kiserikali Dodoma nalo linaendelea.
Serikali imejitwika mzigo isio na uwezo nao japo baadhi ya hiyo miradi michache ni muhimu ila utekelezaji wake na gharama zake ni lazima tutuumie tena sio kidogo na hata uchumi unaweza kuyumb maana baadhi ya miradi inapeleka fedha nyingi nje ya nchi..
Hauwezi kujenga nchi kwa kuongeza expenditure,kukopa kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo mapato ya nchi yanaporomoka.
Ni swala la muda tu itawabidi mbuni kodi za ajabu ajabu ili kujaribu kujikwamua.
Mkuu mimi nakuheshimu sana. Lakini naomba at times uwe objective.
Kuna sehemu serikali inafanya madudu na ni haki yetu kuikosoa kama tunavyofanya humu kila siku. Lakini hebu tuwe wakweli kidogo, tunaweza kupinga juhudi za kuwa na umeme wa uhakika kusukuma gurudumu la maendeleo yetu mbele?
Yes, najua kuna nadharia nyingi hapa (mradi huu ni mkubwa, pesa hatuna, tungewekeza kwenye umeme wa maji, umeme wa gesi, upepo na mengine mengi!). Lakini Ukweli ni kwamba tunahitaji umeme. Sijaona juhudi za watangulizi wa jiwe kutupa umeme wa uhakika kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru. Kila kitu ni ujanja ujanja tuu....(refer akina net group, akina Rugemarila nk). Kama huu ndo mradi utatupa umeme, tumsupport JPM!
Tusiwe watu wa kupinga kila kitu..Tunapoteza maana ya neno lenyewe na mwisho wa siku..hata mtu ukipinga kitu cha maana unaonekana ni yule yule.
Umeme ni muhimu kwa maendeleo ya taifa!