Ikulu ya Chamwino: Nani hasa anastahili credits?
Hauoni Ikulu imekamilika? Bwawa nalo walitudanganya kuwa lingeshakuwa limekamilika kumbe vitu kibao vilisimama mama Samia ndiyo ameenda kulikwamua.
SGR nayo kumbe ilikua imeshaanza kufa, mama Samia ndiyo ameiokoa.

Hela za Plea bargaining kumbe zilishatoroshewa China wakati hatujui, sisi tunaambiwa ndiyo hela zetu za ndani zinajenga nchi. Kumbe wameshazipiga, mama ndiyo anapambana azirudishe.

Bado uchaguzi wetu wa 2020 ulivyoharibiwa na kuivuruga nchi. Sasa hivi mama ndiyo anapambana kuwarudisha watanzania wawwze kukaa pamoja, otherwise nchi ilikua imeshapasuliwa kitambo.
Accounts za watu zikafungwa hovyo na pesa kuchukuliwa, mama ameweza kuwarudishia.

Makinikio yalizuiwa kwa mbwembwe, lakini aliyeyazuia akayaachia kimyakimya kigiza kilipoingia.

Watu wakaondolewa kazini kikatili na mafao yao kuzuiwa, mama sasa hivi yupo kutibu majeraha.

Hivi nyie hebu tuambiane hapa, tuwe wa kweli kabisa. Yule Kamaa alifanikisha kipi kwenye nchi hii?
Ujinga mtupu.
 
Zuhura yunisi ambaye ni mwandaaji wa simulizi ya ikulu naona anaowataja ni Nyerere, Mwinyi na Kikwete. hivi mnafikri watanzania bado wapo zama za giza Magufuli hata msipomtaja mawe yatamtaja, Kikwete sioni mchango wake hapo.

Jiwe ameondolewa kwenye orodha ya watu waliowahi kuwa marais wa nchi hii kwasabb aliinajisi nchi hii.
 
Viongozi wetu wanadhidi kupapalia chuki kwa Watanzania, chuki dhidi ya viongozi inazidi kuongezeka kwa Watanzania. Imani ya watanzania kwa serikali ya awamu hii ni kama kudeki kwenye bahari.

Tunajua JPM ndo alithubutu kujenga hio Ikulu ila hawakutaka kumtaja wamezunguka wee na hawajiamini kabisaaa. Watanzania sisi sio wajinga tunajua aliyethubutu kujenga ikulu na Serikali kuhamishiwa Dodoma,
 
Hivi watz mtaacha lini upumbavu wa kutilia maanani vitu vidogo vidogo visivyo na faida kwenye maisha yenu na taifa kwa ujumla?

Kwani jina la Magufuri linge tajwa nchi ingeingeza bilion ngapi na baada ya kutotajwa nchi imepata hasara na billion ngapi?
Wewe ni mpumbavu pamoja na genge lako.
 
Unaweza kweli kuandaa makala ya serikali kuamia Dodoma wakati alietekeleza hilo agizo umuache.

Mbowe ameiuwa CDM, Lissu nae kastuka late kumtukana Magufuli akumjengei kaamua attack zake kwa juzi peleka kwa Samia na CCM kwa ujumla.

Hatua za Lissu zimekuja too late, isitoshe narrative anayoongea ni yeye peke yake, wenzake wameshaua credibility ya chama chao kuaminika kama mbadala wa CCM; wananchi wanawaona waganga njaa tu.

CCM ishukuru hakuna chama cha kutembelea upepo wa Magufuli 2025, halafu safu yao yenyewe ilivyo nyepesi sasa kwenye hoja na uwezo; wangesambaratishwa kama upepo.
Mbona unaanzisha mada ndani ya mada?

Uzi huu unahusu ujenzi wa Ikulu ya Chamwino - Dodoma.

Swali ni Rais wa awamu pili ndo serikali yake imejenga Ikulu hiyo?

Cha ajabu wewe umeacha kujadili hoja iliyo mezani umeanza kuishambulia CHADEMA, Lissu na Mbowe..!

Kwani hao ndiyo wanazindua Ikulu??

You are off the topic!!
 
Hivi hilo jengo litawasaidia watanzania kupunguza nini kwenye ugumu wa maisha yao? Hivi hilo linazidi kasri ya ufalme la Uingereza? Mbona waingereza wengi hawalipendi? Yako mambo hayahitaji kupoteza muda kwa kubishana kusiko na msingi.
Kwani ikulu ya Dar es salaam ilikuwa na mapungufu gani? Nyerere alipofikiri makao makuu yawe Dodoma 1973, Teknolojia ya mawasiliano ilikuwa chini sana.Leo mnafanya mkutano ya kimataifa na kila mtu yuko kwake.
 
Basi wote kwa pamoja kila mmoja angepanda mti mmoja ili libaki kwa Jina lake
Kuanzia marais na wake zao pia
Hapo tutasema huo mti aliupanda fulani badala ya kuwapa masifa wao wa kujenga utafikiri walibeba zege
 
Ndio imejengwa na Samia kwa sababu yeye ndo ameikamilisha kuijenga.

Kwa hata huyo JPM si alikuta miradi iliyo anzishwa na kikwete yeye akaja kuimalizia akaita ni ya kwake?
Watu wamagufuli wanaunga alichokifanya yeye kwa kikwete ila wanapinga mama samia anachokifanya kwa magufuli.
Maana miradi mingi ilikuwa planned na mingine ikaanza kutekelezwa wakati JK, magufuli akaja kuimalizia halafu akachukua credit ila hizo credits hawataki ziende kwa mama samia kwa kumalizia mirqdi iliyopangwa na kuanzishwa wakati wa jpm
 
Zuhura Yunus ambaye ni mwandaaji wa simulizi ya Ikulu naona anaowataja ni Nyerere, Mwinyi na Kikwete.

Hivi mnafikri watanzania bado wapo zama za giza? Magufuli hata msipomtaja mawe yatamtaja, Kikwete sioni mchango wake hapo.

Sema Watanzania Siyo Wajinga Sasa Hivi
 
Viongozi wetu wanadhidi kupapalia chuki kwa Watanzania, chuki dhidi ya viongozi inazidi kuongezeka kwa Watanzania. Imani ya watanzania kwa serikali ya awamu hii ni kama kudeki kwenye bahari.

Tunajua JPM ndo alithubutu kujenga hio Ikulu ila hawakutaka kumtaja wamezunguka wee na hawajiamini kabisaaa. Watanzania sisi sio wajinga tunajua aliyethubutu kujenga ikulu na Serikali kuhamishiwa Dodoma,
Hii imefikia wapi?

NDC hasara tzs bil. 11.9
Mkulazi hasara tzs bil.14.4
TRC- hasara tzs bil. 31.5
ATCL- hasara tzs bil. 35.2
NHIF- inajiendesha kwa hasara bil.189.7.

Kuna mtu kachukuliwa hatua hadi sasa? Au kazi za CAG ni ceremonial?


Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom