Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Mkuu naunga mkono hoja yako kwa 100%... Kama kuishi na mwanamke kwa miaka 2 inatambulika kisheria kuwa ni ndoa halali iweje watu walioishi zaidi ya miaka 50 wamezaliana, wameendesha mambo yao pamoja, wamekabiliana na changamoto mbalimbali kwa umoja wao IWEJE leo tuseme eti Muungano ni batili kwakuwa eti cheti hakipo! Makubaliano au muungano ni zaidi karatasi yenye maandishi ya watu wawili! Muungano huu Unawakilisha Muungano wa Jamii ya watu wa Znz na Watu wa bara na umedumu kwa nusu karne mpaka sasa! Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa pande zote mbili yaani CCM na UKAWA wote wako bias ile mbaya! Mifumo wanayopendekeza yanajikita kwenye political gain zaidi! CCM wajua kuwa ndani ya mfumo wa dola mbili wataendelea kutawala milele daima, UKAWA wanajua kuwa ndani ya dola tatu CCM itakosa nguvu na kuachia ngazi! Kama kweli wote wangekuwa na dhamira ya kweli ninauhakika leo hii Tanzania Ingekuwa Moja chini ya Serikali Moja yenye kuendeshwa kwa mfumo wa Majimbo kama zilivyo nchi za wenzetu..
Mkuu, ninakushukuru kwa andiko lako!.

Wewe umekisema kile ambacho watu wengi hapa hawataki kukisema.

Ukivichambua vyama vya siasa utaona kuwa hoja zao za muungano zinachagizwa na nguvu zao za kisiasa kwa mtazamo wa kupata madaraka ya nchi katika sanduku la kura. Hakuna chama cha kisiasa kinachomwangalia mwananchi katika hii hoja ya Muungano. Sijakiona bado!.

Hoja ya Muungano katika aina ya serikali inazifanya vyama vya siasa kudhani itavisaidia kujipenyeza kwa urahisi ili vipate madaraka ya nchi au viendelee kutawala.

Mimi ninashindwa kuelewa hii dhana ya kutaka kwa nguvu zote hati ya Muungano. Hivi kama hati ya Muungano isingekuwepo wangefanya nini wakati kwa sasa wameishapewa fursa ya kuamua kupitia mchakato wa Katiba. Kama ni kuachana na Muungano, kwani lazima kuwepo na hati ya Muungano.

Kwa sasa wametumia siku nyingi wakiulizana hati ya Muungano kama vile Muungano ndiyo umefanyika jana.

Crimea wameachana na Ukraine pamoja na kuwepo kwa makaratasi ya Muungano ambayo kwa sasa hayo makaratasi ni kaput.

Muungano wa nchi siyo karatasi bali matakwa ya wananchi. Kama wananchi wakitaka kuachana na Muungano kama ilivyofanyika Crimea, hayo makaratasi yanakuwa ni sentimental.
 
Hahahaha shida tupu,wizi mtupu

Mi sitaki muungano kutokana na KERO ZISIZOISHA ZA MUUNGANO si vinginevyo. Zanzibar ndio hawataki hii kitu nashangaa wawakilishi MSHo et el nini maana yake. Then tunaomba document yote sio kipande tujue yaliyomo.
 
Kwanini mnaonesha SAINI tu? sehemu inayohusu makubaliano kwanini inafichwa? our interest ni kufahamu nini kilikubaliwa baina ya hayati Mwl J.K Nyerere na Abeid Karume. Kila mtandao ninaojaribu kusearch umeonesha sehemu yenye saini tu kitu gani kinafichwa?

hata hizo sahihi zinaonekana zimebandikwa! jk na serikali yake bana bonge la wasanii!
 
......True Mkuu changa la mmacho hata hapa chini inaonekana wanasaini karatasi zaidi ya moja !!!!

Muungano+2.jpg
Nimeipenda hiyo picha. Wanaonekana vijana machachari wenye mapenzi kwa nchi yao. Linganisha hiyo picha na viongozi walioko sasa kwenye nafasi waliyokuwa nazo hao vijana wa 1964. Hawana suti za kuhongwa,wamevaa nguo za kawaida kabisa,hawana viriba tumbo.
 
nakumbuka Pasco aliwahi kuitafuta hati ya Muungano hadi huko UN akaikosa..hii imetoka wapi?
Mkuu Edson, nasubiri kuiona hii hati na haswa vipengele vyake, ili nipate majibu, ni kwanini haikupelekwa bungeni?, kwa nini haikupelekwa UN?!. Kwa nini haipo kwenye idara ya Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa!.

Kumefunguliwa kesi kadhaa watu wakiziomba hizi hati, kwa nini hawakupewa?!.

All and all madam zipo, nikiishaiona nitazifutilia mbali zile thread zangu 5 kuhusu hati za muungano!.

Pasco
 
Hii ni fax ya leo saa tatu na dk 55 nahisi mwaka utakuwa umekosewa kwani leo ni tarehe 14 aprili 2014...sidhani kama ni kutokea tu mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo fax hio imetolewa leo
 
Duh, hii hati ya Muungano ilisainiwa tarehe 22 badala ya 26? Sasa tarehe kamili ya Muungano ni lini? Hii nayo ina mashaka.
 
Naona tunachezewa sana ila basi tu. hii ngoma ni feki kabisa. kwanini walikuwa wanachelea kuitoa.
 
Mmama anang'aka hapa.anawambia wanaotaka serikali mbili wakienda zanzibar wanaongelea chooni na kisimani tu.
 
walioiomba hati siyo waandishi wa habari, ni wabunge wa bunge la katiba tunatakaka ipelekwe huko na wala sii hizi sarakasi.

kama latiba ni ya wananchi basi watoe nakala nyingi wazi sambaze nchinzima imfikie kila mwananchi....wabunge nao uchwara tuu
 
tarehe 14 April 2013 ilikuwa jumapili ......sio siku ya kazi, ??????
 
tarehe 14 April 2013 ilikuwa jumapili ......sio
siku ya kazi, ??????
 
Mh! Wapendwa, mbona Prof. Shivji na mpendwa mmoja Bunge la Katiba alipowasilisha taarifa ya kamati Yake alisema "Republican ya Tanganyika haikuwepo?" Sasa hapa kwenye sahihi ya Mwl. Nyerere mbona jina ni hilo. Ufafanuzi unahitajika. Kwahiyo ndio kusema asili yetu sisi wa Bara ni Tanganyika?

Pia, hivi kwenye picha ya kuchanganya udongo, wale waliopiga magoti walioshikilia vile vibuyu wakati Mwl J.K.N akichanganya udongo wako wapi? Majina yao ni kina nani? Roles zao zilikuwa ni kina nani ktk Serekali wakati huo? Mpaka washike vile vibuyu! Mh! Sio mchezo!

Pia kwanini Karume alikaa pembeni? Kwanini hakushika udongo wa Zanzibar na Mwl. j.K.N ashike wa Tanganyika? Ndio wachanganye?

Naomba ufafanuzi kwa anayejua.

Queen Esther
 
Back
Top Bottom