Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano


Mimi nilifikiri nakala za hati ya Muungano zingekuwa kwenye kila maktaba ya vyuo vya elimu ya juu kama sehemu ya rejea kwa law students. Nchi ya ajabu kweli kweli hii.
 

kaka hujaelewa kuna jambo linatafutwa kwenye hizo hati kabla ya kujadili muungano. Hujasikia kwamba muundo wa muungano unatokana na hati ya muungano? Sasa hati haipo ili kionekane nini kilikubaliwa! Muungano wa serikali mbili ulikuwa udumu kwa muda gani? Kuna mabo ya msingi kwenye hati kwa sababu imetamkwa kwamba ndio msingi wa muungano. umeelewae!
 
Aibu gani hii ya mwaka kwa ccm na serekali yake. Kumbe ndio maana watu walipigwa na kuumizwa juu ya huu mkataba ambao ni fake. Hili ni moja, je kama suala nyeti kama hili kuna hati fake hyo mikataba ambayo ni siri kuna uchafu kiasi gani? Kwahiyo sasa ndio tumezidi kujua hata matokea ya kura wakati wa uchaguzi huwa ni fake na ndio maana askari hutumika kulazisha matokeo. Sasa ndio hatima yenu inawadia. Uwongo unafikia tamati sasa.
 
Mimi nilifikiri nakala za hati ya Muungano zingekuwa kwenye kila maktaba ya vyuo vya elimu ya juu kama sehemu ya rejea kwa law students. Nchi ya ajabu kweli kweli hii.

Nina hamu sana kuisoma hiyo hati nione ninini kinafichwa namna hiyo!
 
We need to go one step further. kama hati imepatikana, je baraza la wawakilishi lilishiriki kuijadili na kuiptisha km bunge la JMT lilivyofanya?

Then another step kuona kama hao wawakilshi walipigiwa kura, na wakati wanaenda bungeni walioga n.k #cheap politics
 
Safi sana Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.

Kwa sasa kelele za hati ya muungano zimekatwa. Tuendelee na mijadala ya msingi yenye maslahi kwa taifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itadumu ingawa ina maadui wengi. Pamoja tutashinda.

Una Elimu gani ndg?
 
Mkuu hakuna wanaokubaliana kuhusu muungano hii sintofahamu ndio inaleta malumbano.
Kama hata waliokuwa waandamizi serikalini nyakati hizo wanakiri kutokuiona hati hiyo au kushuhudia inasainiwa, je huyu Ombeni Sifue na washarika wake wameipata wapi hiyo hati?!
 
Kuna mtu aliuliza kama hii analogy ya ndoa ni sahihi kati ya Zanzibar na Tanganyika nani mke nani mme?

Then who is Transmitter and who is Receiver? shukran Mkuu umenifanya nitabasam mwenyewe!!! Binafsi nadhani msisitizo ungewekwa kwenye Maboresho ya kero za muungano zaidi ya kudai Hati na sahihi za waasisi... Iwe serikali 1, 2 au 3 siyo issue kwetu, Issue ya msingi ni kuondoa mapungufu yaliyoko kwenye Muungano kwa maslahi mapana ya Wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani
 
Noted with Thanks Mkuu... Kitendawili hiki kitafumbuliwa soon ...
 

If that was the case, then kwa nini sasa hao "wanandoa" waanze kutoa nyeti feki vya ndoa vyenye sahihi za kughushi?

Kwa nini cheti chao cha ndoa kiwe cha siri hivyo?

Si waseme tuu kuwa hawajawahi kuoana msikitini, kanisani, au kwa msajili wa ndoa lakini wamekuwa wakiishi kama mume na mke kwa muda wa miaka 50?

Halafu kama mnatumia mfano wa ndoa za kawaida kuhalalisha ndoa ya Zanzibar na Tanganyika basi tuambieni kwenye hii ndoa mume ni nani na mke ni yupi? Kwani sheria zetu zinahalalisha ndoa ya jinsia moja, let alone civil partnership?
 

Ina maana hujasikia aliposema hati alipoitoa au ni mgumu wa kuelewa?
 
Nadhani Tundu Lissu ana point nzuri sana sasa hivi kuliko hapo awali. Katumia mbinu ya wanasheria ya kuwatia watu jazba.

Sasa linakuja swali very simple, Jee, huo Muungano ni wa nchi ipi na ipi?

Hapo sasa!
 

Kama hii hati ni fake ina maana kuna hati original ambayo umeshaiona!! Unaeza kutujulisha ilipo?
 
Haha tatizo sio kuonyesha watu hati...issue hapa ni validity ya hiyo hati
 
Fax ya ikulu hii...see hii docView attachment 151404

Kweli kabisa namba ya Fax iliyotumika kutuma hii nakala feki, ni 2117272 ambayo ukiangalia document hii, ni namba ya IKULU. Umefanyika mchezo wa ndani kwa ndani ya Ikulu, asubuhi hii. Imetumwa kutoka fax moja kwenda fax nyingine, ndani kwa ndani Ikulu. NI FEDHEHA KUBWA! UONGO HAULIPI!
 
Waandishi wa habari wanakabidhiwa nakala kila mmoja...

wAANDISHI WETU BANA hivi nao kwa nini hawakutumia wito huu kuonyesha mgomo hadi waruhusiwe kuingia ndani ya bunge na kupata habari.Wamepewa kisu wakate nyama badala yake wameondoka na kipande cha ngozi.poor waandishi
 
Jamani nakiri kuwa usanii unachanganywa na mambo mazito ya kuongoza nchi!!,Hivi kama hati walikuwa nayo na ni halali,kulikuwa na ugumu au ubaya gani wa kuitoa pale ilipohitajika na wajumbe ambao kisheria wamepewa mamlaka ya kupitisha Rasimu ya katiba?. Haya hiyo na ile iliyotolewa mwanzoni Dodoma ina tofauti gani? kwa nini ile nayo iligushiwa? na kwa maslahi ya nani, ili kuficha nini?.Bado hawawezi kunishawishi kama kuna ukweli wowote ule zaidi ya uongo ambao karibuni tu tutaubaini.
 
Nadhani Tundu Lissu ana point nzuri sana sasa hivi kuliko hapo awali. Katumia mbinu ya wanasheria ya kuwatia watu jazba.

Sasa linakuja swali very simple, Jee, huo Muungano ni wa nchi ipi na ipi?

Hapo sasa!

Halafu hiyo hati original ni moja tuu? Zanzibar nao wana original yao? If so, wao huwa wanaihifadhi wapi?

Maana inadaiwa kuwa UN wala SMZ hawana Hati ya Mkataba wa Muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…