Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Hiyo hati ya ukweli au baada ya kusikia wajumbe wanaidai ndo wakaamua kwenda kuitengeneza?
Siku zote ilikuwa wapi kuoneshwa mpaka leo ama wakati huu ndo ioneshwe?
Waandishi wa habari nao ni sehemu ya Bunge la Katiba?
Uhakika uko wapi kama hiyo ndio hati yenyewe?

HAYA FANYENI YOTE LAKINI MKUMBUKE KUDUMISHA AMANI YA NCHI YETU.
 
Lisu for president 2015 via chadema dr slaa awe waziri mkuu, moto utawaka tu huko ufisadini.
 
Hii ni sifa mojawapo ya Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Kuwa huru na mwenye kuthubutu kwa mambo ambayo wengi wanadhni hayana haja ya kuthubutu. Kama si yeye hata katiba tusingeijadili, kwani alishindwa kukataa? Hongera sana Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Haya tujadili sasa.
 
Hatimae wameitoa kwa aibu, tunamshukuru Tindu Lissu na wengine kwa kuilazimisha serikali kufanya hivyo. Good strategy,huu ndio mwanzo wa ushindi!
 
Hahahahahahaha Tanzania zaidi ya uijuavyo"......... Kama kitaani tu tunawezapata academic certificates feki, barua feki tena zenye mihuri ya ikulu, itakuwa hati ya muungano? Haha
 
Huoni bila Lissu isingeonekana,Lissu ni kichwa who knows may be hata hiyo yenyewe fake
 
Hii ni sifa mojawapo ya Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Kuwa huru na mwenye kuthubutu kwa mambo ambayo wengi wanadhni hayana haja ya kuthubutu. Kama si yeye hata katiba tusingeijadili, kwani alishindwa kukataa? Hongera sana Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Haya tujadili sasa.
Katiba ni madai ya Watanzania,kukubali au kukataa hukuondoi madai ya Watanzania is a matter of time,msijifariji kwa ujinga..
 
Kimsingi aliuliza maswali 3 ambayo ni muhimu katika mikataba kisheria na zaidi yanategemeana na katika yote hakuna ambapo serikali itatoka salama. .kwamba,hati ya makubaliano ya muungano haipo,Pili kama ipo ni halali? na tatu muungano ni halali kulingana na mkataba unavoelekeza na kuainisha?patamu hapo. .lets wait n' see. .
 
Hati ya Muungano imetolewa, na imeshapelekwa Bungeni dodoma. Tundu Lissu alisema HATI hiyo haipo hivyo Muungano huu ni feki, na taifa hili ni feki.
Kama kweli hati hiyo aliyoionyesha leo Katibu mkuu Kiongozi ni yenyewe.....Kuna watu wataabika sana kwa hoja za jazba bila kuzifanyia uchunguzi.
Natamani iwe uongo ili huu umaarufu tuliompa leo Tundu Lissu uweze kudumu, kinyume na hapo itakuwa aibu sana.

Hiyo ya kufoji? Halafu hata kufoji kwenyewe hawajui! Data zote zilishanyakwa
 
Kweli ccm comedy mtupu, wanaoimba hati hio ni wengine, nyie mnawapelekea waandishi wa habari, wakati huohuo waandishi wa habari mmewazuia kuingia bungeni, so hao wabunge wanaoitaka waisome kwa magazeti au!!! Hamna jipya, jipangeni safari hii!!!!
 
we mleta hoja vipi?? unafikiri bila Tundu Lissu kutamka maneno, hii inayosemekana kutwa ndo HATI ingetolewa???, kumbe uko kishabiki zaidi, aisee acha hizo bwana
 
Kabla ya hata kudhani kuwa 'kina lisu' wataaibika, jielize kwanza ilikuwa wapi hadi itolewe sasa pamoja na kelele zote hizo za siku zote. Kuna maswali mengi mno kwenye hili kuliko majibu!
 
Hati ya Muungano imetolewa, na imeshapelekwa Bungeni dodoma. Tundu Lissu alisema HATI hiyo haipo hivyo Muungano huu ni feki, na taifa hili ni feki.
Kama kweli hati hiyo aliyoionyesha leo Katibu mkuu Kiongozi ni yenyewe.....Kuna watu wataabika sana kwa hoja za jazba bila kuzifanyia uchunguzi.
Natamani iwe uongo ili huu umaarufu tuliompa leo Tundu Lissu uweze kudumu, kinyume na hapo itakuwa aibu sana.
Naomba nikuulize maswali yafuatayo:-
1. Kuna hati ngapi za Muungano?
2. Kama hii ni halali je zile zilizowasilishwa hapo Mwanzo zikiwa na Saini za Nyerere na Msekwa tu na saini zenyewe feki ni nani alizipeleka kule?
3. Na Lengo la Mpelekaji wa hizo za awali lilikuwa nini?
4. Je msukumo huo wa kuionyesha hati hiyo na kuipeleka Bungeni umetokana na nini? (Jibu ni TUNDU LISSU)

Tambua kuwa kama hiki kilichoonyeshwa ni sahihi hapa ndipo CCM walipoingia CHOO CHA KIKE kwani waliyokuwa wakiyaficha katika hati hiyo yatabainika hadharani na ukweli utajulikana.
 
nazidi kuamini kuwa nchi hii tunaongozwa na watu wasiojitambua kabisa,,,kwani waandishi wa habari waliitaka hiyo hati ya muungano????
 
Hii ndio ile forgery ambayo ilikuwa ichapishwe cap chap kisha wakawabambikizie wabunge wa bunge maalum?
 
Huoni bila Lissu isingeonekana,Lissu ni kichwa who knows may be hata hiyo yenyewe fake

Tundu Lissu anahoja nzuri sana.Tatizo ni kusema kuwa HATI hiyo haipo...nahisi kuna namna ya utunzaji wa Vitu muhimu na kuna utaratibu wa kuvitoa...Siyo kila kitu kukiweka weka hovyo tu. Pili kama hiyo hati ni Original huoni kuwa Tundu Lissu na kundi lake watakuwa wameaibika? Kwa jinsi tulivyo mpa sifa leo halafu ije onekana tumetoa sifa kipumbavu aisee itaniuma sana.
 
1609585_617648764977500_7970301950690104449_n.jpgHati ya Muungano ikisainiwa
 
Lisu kama kawaida kawapeleka chaka wenzake poor chadema.
 
Back
Top Bottom