Ukiangalia hati hii iliyotolewa, na picha hii, ambayo wengine wanadhani ndiyo kumbukumbu ya utiaji saini wa hati hii, yafuatayo yanatia mashaka:
1. Mkono ulioandika: 22nd siyo mkono ulioandika APRIL, kutokana na utofauti wa miandiko au uumbaji wa herufi
2. Chini ya Saini ya Mwalimu, kuna mstari ambao umefutika kidogo, kuashiria kuchoka kwa karatasi pamoja na wino, lakini mstari jinsi ulivyochoka unatia mashaka, kwa sababu ya ANGLE. kwani uchovu (deterioration) umefuata mstari sio Karatasi.
3. Kama kuna madai kwamba picha hii ndiyo kumbukumbu ya kusaini hati hii iliyotolewa, huo sio ukweli. Kulingana na picha hii, kwa MKAO (Positioning) ya
wahusika yaani Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume, ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere alisaini upande wa KULIA na Abeid Karume alisaini KUSHOTO, Sasa kuwa makini kumuangalia Mwalimu Nyerere. Angalia Picha kwa makini, angalia mkao wa mikono yao, pia waweza kujaribu kuifanya wewe mwenyewe kujiridhisha.
Pia tazama mtu aliyeko kulia kwa Mwalimu Nyerere, angalia mwelekeo wa macho yake (direction of his eyes) kwenye Karatasi ni upande gani.
4. Typewriter za nyakati hizo zilikuwa hazina uwezo wa kuweka space, ila ungeweza kutumia dotted line (.............) au dashed line (----------) kama hizo dotted au dashed line zimefutika kutokana na muda mrefu, basi na ile alama ya mkato (comma) (,) baada ya neno APRIL nayo ingefutika.
5. Neno "me" la mwisho katika neno Karume kwenye saini liko chini ya mstari kutia mashaka limeongezwa, na maneno yalikuwa yanaungwa katika saini yake wakati kwenye "me" haina hicho kiungo.