Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Nimeona picha za kuchanganya udongo, hivi hakuna picha za kutia sahihi huko maktaba!!?? Wanaamini kabisa tukio la kutia sahihi ni kubwa kuliko la udongo.
 
ilikuwa wapi wote huu ccm watakuwa wameenda kutengeneza ndo maana wassira ameongea kwa kiburi kwamba hati ipo ngoja tuone kesho
 
mkataba huu ulikuwa baina ya NCHI ipi na ipi?
na ni kweli mkataba huu uliuwa tanganyika?
mkataba ulijenga muundo upi wa muungano?
mkataba ulitoa nafasi ya kuongeza mambo ya muungano kwa chombo gani?
JE mkataba ULIRIDHIWA NA BARAZA LA MAPINDUZI?
MKATABA ULIOTOLEWA NDIO HALISI AU FEKI?

HAYA NI MIONGONI MWA MASWALI YANYOHITAJI MAJIBU ndio maana ikabidi lazima utolewe hadharani
 
Hakika mambo ndo yatakuwa magumu zaidi ya tidhaniavyo...

Uhondo ndo kwanza umeshaanza..
 
DVD Ilikuwa in load sasa filamu inaaza na JINA la nchi ILIYOUNDWA 22/4/1964 NA WAASISI jamuhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar. kisha inaeleza wazee wa mtoto muungano wataendelea kuwapo baada ya mtoto kuzaliwa.
filamu inaaza kwa kuonesha mtoto atapofika 10years atafanyiwa mtihani wa kura ya maaoni ........endelea kutazama mpaka mwisho uone CCM Wanavyoaibika...........................
 
Unajua ndio kitu najiuliza kwamba kama muungano ni kwa ajili ya watu, na muungano unahalalishwa na hati, inamaana hiyo hati wananchi wana haki ya kuiona. Sasa hata kama wananchi ambao kimsingi hati hiyo ipo kwa ajili yao hawawezi kuiona, hati hiyo ni kwa ajili ya nani? Na kwa nini kumekuwa na lugha za kutatanisha sana kutoka kwa viongozi wetu kila linapokuja suala la hati ya muungano?

mkataba wa inchi inayoitwa Tanganyika na asili yake wewe unaujua uliko? kina nani walioshiriki kutengeneza Tangayika?
 
Habari

Nina mashaka na hati hii iliyotolewa leo ikulu eti ni hati halali ya muungano.

KATIBU KIONGOZI OMBENI SEFUE amewaambia waandishi kuwa sasa itawekwa ktk makumbusho sehemu mbalimbali nchini.

Mbona mwanzo haikuwekwa?

MBONA awali hati iliyopelekwa bungeni ilikuwa na utata hasa ktk saini ya JKN?

JE IMEKWENDA KUCHAKACHULIWA BAADA YA AKINA TUNDU NA JUSSA KUCHACHAMAA?

TUJADILI.
Wakileta ndo wameumbuka maswali hayajibiki mana hati itaonyesha muungano zanzibar na tanganyika sasa leo tanganyika haipo
 
Nimeona kwa njia ya mtandao saini za waasisi wetu walizoweka katika hati ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 22/4/1964. Nimeridhika kuwa kumbe makubaliano yalifanyika, lakini naomba wajuzi wa mambo mnifahamishe mambo mawili:

1. Mimi tangu nasoma shule za kata, nimeaminishwa kuwa muungano ulifanyika tarehe 26/4/1964, sasa inamaana walisaini tarehe 22/4/1964 halafu wakaenda kufanya taratibu za sherehe au? sasa siku halisi ya muungano ni siku ya kutia saini waraka wa mkataba au siku yoyote ambayo wahusika wanaweza kuamua kutitangazia.

2. Nimeona saini ya Mzee Karume imekuwa ndefu hivyo kwamba haikutosha katika mstari mmoja ikamalizikia katika msitari mwingine, ina maana kuna uwezekano wa saini kutomalizikia katika karatasi moja ikamalizikia katika karatasi nyingine?, tafadhali nielimishe!

Nyongeza tazama kwa ufasaha rangi za maandishi ya hizo saini.

https://www.youtube.com/watch?v=15tUVYimdsY
 
Ni aibu kubwa kuwa na serikali inayojidhalilisha namna hii...
 
attachment.php

attachment.php



Ukiangalia hati hii iliyotolewa, na picha hii, ambayo wengine wanadhani ndiyo kumbukumbu ya utiaji saini wa hati hii, yafuatayo yanatia mashaka:


1. Mkono ulioandika: 22nd siyo mkono ulioandika APRIL, kutokana na utofauti wa miandiko au uumbaji wa herufi


2. Chini ya Saini ya Mwalimu, kuna mstari ambao umefutika kidogo, kuashiria kuchoka kwa karatasi pamoja na wino, lakini mstari jinsi ulivyochoka unatia mashaka, kwa sababu ya ANGLE. kwani uchovu (deterioration) umefuata mstari sio Karatasi.


3. Kama kuna madai kwamba picha hii ndiyo kumbukumbu ya kusaini hati hii iliyotolewa, huo sio ukweli. Kulingana na picha hii, kwa MKAO (Positioning) ya
wahusika yaani Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume, ni dhahiri kwamba Mwalimu Nyerere alisaini upande wa KULIA na Abeid Karume alisaini KUSHOTO, Sasa kuwa makini kumuangalia Mwalimu Nyerere. Angalia Picha kwa makini, angalia mkao wa mikono yao, pia waweza kujaribu kuifanya wewe mwenyewe kujiridhisha.
Pia tazama mtu aliyeko kulia kwa Mwalimu Nyerere, angalia mwelekeo wa macho yake (direction of his eyes) kwenye Karatasi ni upande gani.


4. Typewriter za nyakati hizo zilikuwa hazina uwezo wa kuweka space, ila ungeweza kutumia dotted line (.............) au dashed line (----------) kama hizo dotted au dashed line zimefutika kutokana na muda mrefu, basi na ile alama ya mkato (comma) (,) baada ya neno APRIL nayo ingefutika.


5. Neno "me" la mwisho katika neno Karume kwenye saini liko chini ya mstari kutia mashaka limeongezwa, na maneno yalikuwa yanaungwa katika saini yake wakati kwenye "me" haina hicho kiungo.
 

Attachments

  • Red_Saini.jpg
    Red_Saini.jpg
    30.9 KB · Views: 317
  • Red_utiajisaini.jpg
    Red_utiajisaini.jpg
    37.2 KB · Views: 323
Muungano huu ni kizungumkuti. Haijalishi kama hati ipo au la. Tunachotaka ni Tanganyika yetu.
 
nahofia usalama wa role mode wangu tundu antipas lissu.watu wa aina yake huwa hawaishi mda mrefu.
 
Mkuu hati yenyewe imepigwa solotape.......Mashaka matupu

kwa dunia ya sasa ya kidijitali,ni ngumu sana kuudanganya uma kuhusu hati.kama ni hati batili itabainika tu.yawezekana wamefanya hivyo ili kwenda kupoza bunge la katiba.
 
Mimi binafsi sijaona alichoongea cha msingi...kama huu muungano na halali basi na sisi turuhusiwe kununua ardhi visiwani mbona upepo wa bahari tunaupenda pia?
 
Tanganyika ivue koti la muungano kwanza, waliozoea kuishi kwa uwongo hawawezi kuishi katika kweli!
 
Back
Top Bottom