The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Nimeona picha za kuchanganya udongo, hivi hakuna picha za kutia sahihi huko maktaba!!?? Wanaamini kabisa tukio la kutia sahihi ni kubwa kuliko la udongo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajua ndio kitu najiuliza kwamba kama muungano ni kwa ajili ya watu, na muungano unahalalishwa na hati, inamaana hiyo hati wananchi wana haki ya kuiona. Sasa hata kama wananchi ambao kimsingi hati hiyo ipo kwa ajili yao hawawezi kuiona, hati hiyo ni kwa ajili ya nani? Na kwa nini kumekuwa na lugha za kutatanisha sana kutoka kwa viongozi wetu kila linapokuja suala la hati ya muungano?
Wakileta ndo wameumbuka maswali hayajibiki mana hati itaonyesha muungano zanzibar na tanganyika sasa leo tanganyika haipoHabari
Nina mashaka na hati hii iliyotolewa leo ikulu eti ni hati halali ya muungano.
KATIBU KIONGOZI OMBENI SEFUE amewaambia waandishi kuwa sasa itawekwa ktk makumbusho sehemu mbalimbali nchini.
Mbona mwanzo haikuwekwa?
MBONA awali hati iliyopelekwa bungeni ilikuwa na utata hasa ktk saini ya JKN?
JE IMEKWENDA KUCHAKACHULIWA BAADA YA AKINA TUNDU NA JUSSA KUCHACHAMAA?
TUJADILI.
Nimeona kwa njia ya mtandao saini za waasisi wetu walizoweka katika hati ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 22/4/1964. Nimeridhika kuwa kumbe makubaliano yalifanyika, lakini naomba wajuzi wa mambo mnifahamishe mambo mawili:
1. Mimi tangu nasoma shule za kata, nimeaminishwa kuwa muungano ulifanyika tarehe 26/4/1964, sasa inamaana walisaini tarehe 22/4/1964 halafu wakaenda kufanya taratibu za sherehe au? sasa siku halisi ya muungano ni siku ya kutia saini waraka wa mkataba au siku yoyote ambayo wahusika wanaweza kuamua kutitangazia.
2. Nimeona saini ya Mzee Karume imekuwa ndefu hivyo kwamba haikutosha katika mstari mmoja ikamalizikia katika msitari mwingine, ina maana kuna uwezekano wa saini kutomalizikia katika karatasi moja ikamalizikia katika karatasi nyingine?, tafadhali nielimishe!
Wakuu ebu tuangalie kwa umakini na tutafakari juu ya Hati hii hususani kwenye Muonekano wa Saini katika video hii kama ilivyoonyeshwa na Mh. Ombeni Sefue.
https://www.youtube.com/watch?v=15tUVYimdsY
Mkuu hati yenyewe imepigwa solotape.......Mashaka matupu
"Monotype Corsiva" imehusika hapa, hakuna saini