Inabidi tukubali na kupongeza chochoko zilizotolewa na mhe. Tundu Lisu kuhusiana na uwepo wa hati ya muungano.
Kwa jinsi navyoijua serikali ya ccm ni mabingwa wa kuficha nyaraka.
Isingekuwa mhe. Lisu kutoa hoja nzito , nadhan labda baada ya miaka mingine 50 ndo tungeonyeshwa.
Wapo pia wajumbe wengine waliohoji uwepo wa hati ya muungano...hii imekuwa chachu kuifanya ccm ionyeshe hati japo kwa shingo upande.
Vile vile imepelekea hadi wajumbe hasa hasa wa ccm wakiwabeza waanze kuuliza kuhusu hati muungano wa unguja na pemba, inaonyesha serikali ya ccm haiwaskilizi wabunge wake.
Hii inadhihirisha maoni ya wachache yameskika.